Uongozi wa Jiji la Zanzibar umejipanga
kusimamia vipaumbele vyote vya usafi wa mazingira ili hadhi ya kuwa na
jiji liendane na vitendo vya mazingira yalio safi na salama.
Hayo yameelezwaa na Mkurugenzi
wa jiji Ndugu Ali Khamis Juma baada ya shughuli ya uchaguzi wa kumchangua mstahiki Meya wa Baraza la jiji la Zanzibar na Naibu wake.
Hakimu wa mahakama ya mkoa Makame
Mshamba amewaapisha wajumbe wa baraza la jiji,mstahiki Meya na naibu meya wa baraza
la jiji la Zanzibar hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Karikoo.
Akizungumza mara baada ya hafla
hiyo Mkurungezi wa jiji la Zanzibar amesema baraza lake litafanya kazi kwa karibu na
wajumbe wa baraza hilo ili kuona dhamira na malengo ya kuanzishwa kwake
yanafikiwa ikiwa ni pamoja na kuyasimamia mabaraza ya manispaa ya Mkoa wa Mjini
Magharibi.
Aidha Mkurugenzi Ali amesema Serikali inamatarajio makubwa na baraza hilo katika kuona yanakuwepo mabadiliko
makubwa katika miji na manispaa za Zanzibar hususani katika usafi wa mazingira
na miundombinu ikiwemo ya barabara.
Nae mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Saleh Juma Kinana
amekishukuru Chama Cha Mapinduzi kwa kumuamini na kumpa zamana na ridhaa ya
kukiwakilisha chama hicho katika nafasi hiyo mpya ya meya wa jiji la Zanzibar.
baadhi
ya wajumbe wamesema kuwa watashirikiana kwa pamoja katika
kufanya kazi zenye maendeleo hususani katika suala la kufanya
usafi wa mazingira katika mji.
No comments:
Post a Comment