Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas
Ndumbaro (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi (Head
of Regional Delegation) wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu
(International Committee of the Red Cross – ICRC) katika Nchi za
Tanzania,Kenya na Djibouti Bw. Olivier Dubois.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam,ambapo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini mchango wa ICRC katika utoaji wa huduma na misaada ya kibinadamu hapa nchini hasa katika kambi za wakimbizi zilizopo hapa Nchini.

Amesisitiza
kuwa Tanzania ikiwa ni mwanachama hai wa ICRC itaendelea kutimiza
wajibu wake wa Kitaifa na Kimataifa na kwa kuzingatia Sheria za
kimataifa zilizopo chini ya ICRC,sheria za Tanzania na mkataba wa
uenyeji (Head Quarter Agreement) kati ya Tanzania na ICRC uliosainiwa
mwaka 2001.
Kwa upande wake Bw. Dubois ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuishirikisha ICRC katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali hususani ile inayohusu utoaji wa misaada ya kibinadamu (Humanitarian assistance) kwa kushirikiana na Chama cha Msalaba Mwekundu – Tanzania (Tanzania Red Cross Society – TRCS).

Ameongeza kuwa ICRC itaendelea kushirikiana na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wadau wengine katika utoaji wa
huduma kwa wakimbizi walioko hapa nchini,wafungwa/mahabusu waliopo
magerezani,mafunzo kwa vyombo vya ulinzi na usalama hususani wakati wa
ulinzi wa amani (Training on International Humanitarian Law during peace
keeping mission).
Bw. Dubois ameambatana na Bi. Andrea Heath mwakilishi Mkaazi wa ICRC – Tanzania.

No comments:
Post a Comment