Katibu Mkuu wa
wizara hiyo Dkt. Zainabu Chaula
|
Na. WAMJW-Dodoma
Wizara ya afya,Maendeleo ya jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto –Idara kuu Afya imeendelea kuimarisha
upatikanaji wa huduma za kibingwa kwenye mazingira karibu na wananchi
kwenye hospitali zake za rufaa za mikoa hapa nchini
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa
wizara hiyo Dkt. Zainabu Chaula wakati akijibu maswali kutoka kwa
wajumbe wa kamati ya ya kudumu ya Bunge na huduma na maendeleo ya jamii
jijini hapa.
“Katika kipindi cha Julai hadi
Novemba 2019 hospitali za rufaa za mikoa 18 zilitoa huduma za mkoba
katika fani za kibingwa na hii ni katika kuimarisha upatikanaji wa
huduma za afya karibu na wananchi”.Alisema Dkt. Chaula.
Alizitaja huduma za mkoba za
kibingwa zilizotolewa ni pamoja na magonjwa ya macho,watoto ,dawa za
usingizi,upasuaji wa kawaida,afya ya uzazi na magonjwa ya wanawake.
“Zipo huduma zingine ambazo
wananchi walinufaika nazo ikiwemo ya upasuaji wa mishipa ya fahamu na
ubongo,sikio,pua na koo,radiologia,afya ya akili,afya ya kinywa na meno
pamoja na tiba ya ngozi na huduma za tiba kwa mazoezi”.
Hata hivyo alisema katika kliniki hizo jumla ya wagonjwa 13,107 walihudumiwa kati yao wagonjwa 1,762 walifanyiwa upasuaji.
Kwa upande mwingine Dkt. Chaula
alisema jumla ya wagonjwa 2,194,738 walihudumiwa katika hospitali 28 za
rufaa za mikoa ambapo wagonjwa wa nje (OPD) walikuwa 1,891, 713 na
wagonjwa wa kulazwa (IPD) walikuwa 303,025 katika kipindi cha julai hadi
desemba 2019.
No comments:
Post a Comment