Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu
Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama ameutaka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kufungua
vituo vidogo katika Wilaya zote nchini ili kuondoa usumbufu kwa wastaafu na
wazee wasiojiweza kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kufanya uhakiki wa taarifa
zao.
Waziri
Mhagama ametoa agizo hilo Jumatano, Januari 15, 2020 Mkoani Manyara wakati wa ziara
yake ya kukagua utekelezaji wa majukumu ya sekta ya hifadhi ya jamii Mkoani
humo, na kusema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haipo tayari kuona wastaafu na
wazee wakipata usumbufu kwa ajili ya malipo ya pensheni zao
Aliongeza
kuwa Serikali inatambua kuwa uhakiki ni zoezi endelevu na wastaafu na wazee wanapaswa
kutii agizo hilo, hivyo ni wajibu kwa mameneja wa Mikoa wa mifuko ya NSSF na
PSSSF kuhakikisha wanaweka utaratibu mwepesi na rafiki kwa wastaafu hao kwani
wapo ambao hawawezi kutembea umbali mrefu kutokana na changamoto mbalimbali.
‘Mnapokwenda
kuwahakiki wagonjwa, nawaomba pia mfungue vituo vya kuwahakiki watu wazee na
watu wazima sana, wahakikiwa waende kukutana nanyi maeneo ya wilayani, hivyo
nawaomba mtengeneze ratiba na kuweka utaratibu mwepesi na rafiki kwa wastaafu,
na agizo hili ni kwa nchi nzima si hapa Manyara pekee’’.
Waziri
Mhagama alitolea mfano kwa Mkoa wa Manyara ambao wazee na wastaafu wengi
wamekuwa wakitembea umbali kwa ajili ya kufika Makao makuu ya mifumo hiyo
iliyopo Mkoani, suala ambalo limekuwa likiwaumiza wazee na wastaafu wengi
hususani wale wasio na watoto au wasaidizi wa kuwafikisha katika Ofisi hizo.
Aidha
Waziri Mhagama alisema kufunguliwa kwa vituo hivyo kutasaidia kuokoa muda wa
kufanya uhakiki na taarifa za wastaafu na wazee wote kupatikana kwa haraka na
kuwasilishwa mapema katika Makao makuu ya mikoa na hivyo kuharakisha
upatikanaji wa mafao ya wastaafu hao kwa wakati.
Akifafanua
zaidi Waziri Mhagama alisema Serikali inatambua kuwa zoezi la uhakiki wa
wastaafu na wazee katika mifuko hiyo bado linaendelea katika maeneo yote
nchini, hata hivyo Serikali imeendelea kusisitiza kwa mifuko hiyo kuongeza kasi
katika malipo ya pensheni na mafao ya wastaafu na wazee hao kwa wakati.
Kwa
mujibu wa Waziri Mhagama alisema Serikali inaendelea kusisitiza mamlaka zote
zinazohusika nchini kuhakikisha zinashirikiana ili kuweza kubaini changamoto
zinazojitokeza wakati wa mchakato wa malipo mafao ya wastaafu na wazee wote
nchini ili kuweza matatizo ya kimfumo na kiutendaji yaliyopo katika maeneo yao.
Waziri
Mhagama aliitaka mifuko hiyo kuendelea kuchukua hatua kwa Ofisi zote za
Serikali na binafsi zinazodaiwa michango ya wanachama ipo pale pale na hakuna
msamaha unaoweza kutolewa, na kuwasilisha taarifa kwa ofisi zote zinazotaka
kuwa wadaiwa sugu ili kuweza kuzichkulia hatua stahiki.
‘Kama
ndani ya halmashauri kuna kuna matatizo ya kimfumo na kiutendaji, ni wajibu
wetu kutoa taarifa katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wakuu Wilaya na wao
watasaidia kuwasiliana na Wizara husika kutatua matatizo hayo yanayojitokeza
ambayo yanaweza kuchelewesha mafao ya wanachama, taarifa hizi hazina budi
kuwasilishwa haraka iwezekanavyo’’.
Aliongeza
kuwa kwa sasa Serikali ipo katika mchakato wa kipindi cha mpito katika utekelezaji
maagizo ya Rais Dkt. John Magafuli, ambapo Ofisi yake imejipanga kuhakikisha
kuwa Mifuko ya hifadhi ya jamii inatoa mafao yanayoendana na hali halisi ya
nchi pamoja na kuzingatia wakati na viwango endelevu.
Kwa
upande wake Afisa Mwandamizi Matekelezo na Mafao wa (NSSF) Adolfrida Mulokozi
alisema katika kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba mfuko huo tayari umelipa
kiasi cha Tsh. Bilioni 1.036 pamoja na kushughulikia madai 26 ya pensheni za
wazee.
Aidha
alisema kwa upande wa usajili, Mfuko huo kwa Mkoa wa Manyara umeweza kusajili
wanachama 1926 wakiwemo wanachama 1062 kutoka katika sekta rasmi na wanachama
864 wa sekta isiyo rasmi.
No comments:
Post a Comment