Kituo
cha tiba ya Magonjwa ya mlipuko kilicho kabidhi wa kwa Serikali baada
ya kumalizika, kilichopo Buswelu Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza chenye
thamani ya shilingi Bilion 1.1
Mhandisi
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Eng.
Francis Mbuya (aliyeinama) pamoja na Wataalamu mbalimbali wa Sekta ya
Afya, wa kiendelea na ukaguzi katika eneo la kusafishia garikwa kutumia
dawa za kudhibiti maambukizi, baada ya kumshusha mgonjwa.
Moja
kati ya kituo cha tiba ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola
na Kipindupindu chenye thamani ya shilingi Bilion 1.1 kilichomalizika na
kukabidhiwa kwa Serikali, kilichopo Mawenzi Kilimanjaro.
Baadhi ya vitanda.
Na Rayson Mwaisemba WAMJW- KILIMANJARO, MOSHI
WANANCHI wametakiwa kuondoa hofu, pindi wakikutana na magonjwa ya mlipuko au mhisiwa mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola.
Wito huo umetolewa na Mhandisi Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Francis Mbuya wakati wa kukabidhi majengo ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Ebola Mkoani Mwanza na Kilimanjaro.
"Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea na jitihada za kuimarisha mikakati ya kudhibiti magonjwa ya milipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu,hivyo mnapo muhisi mtu ana dalili,toeni taarifa" Amesema Mhandisi Mbuya
Aidha, Amesema kuwa Wizara ya Afya, imekuwa ikitekeleza ujenzi wa miradi mbali mbali nchini ya ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika Hospitali mbali mbali za Rufaa nchini pamoja na za kanda lengo ni kupambana na magonjwa aina yoyote ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu.
"Miradi hii imejengwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Mawenzi Mkoani Kilimanjaro na Buswelu Mkoani Mwanza inalenga kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu.
Miradi yote miwili (Buswelu Mwanza na Mawenzi Kilimanjaro) imegharimu jumla ya shilingi Bilion 2.2 kutoka Milion 897 iliyotengwa kwa kila mradi, hii ni kutokana na maboresho yaliyofanyika katika miradi hiyo ili kuweza kutoa huduma bora kwa Wananchi.
"Kwa Buswelu mradi umegharimu kiasi cha shilingi Billion 1.1 kutoka Milion 897 iliyotengwa, hii inatokana na sababu ya maboresho kutoka na kutembelewa na Wataalamu mbali mbali kutoka Bank ya Dunia ili kuhakikisha tunakuwa na viwango ambavyo vinakubalika kimataifa, sawa na mradi wa Mawenzi Kilimanjaro", alisema.
Mbali na hayo, Mhandisi Mbuya amewaasa Watumishi wa Hospitali kuhakikisha wanatunza miundombinu ya vituo hivi katika kipindi chote cha kutoa huduma, ambavyo umeigharimu Serikali pesa nyingi.
No comments:
Post a Comment