Akikagua maendeleo ya
ujenzi wa mradi huo jana (Jumatano Januari 15, 2020), Waziri Mhagama alisema
hakuna sababu kwa mradi huo unaotekelezwa kwa ubia baina ya Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Gereza la Karanga, kutokamilika kwa
wakati kwani fedha zote zilizohitajika katika hatua muhimu za mradi huo zimekwishatolewa.
Kwa mujibu wa Waziri
Mhagama alisema kiwanda hicho ni miongoni mwa miradi muhimu ya kimkakati
iliyopangwa kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo mkandarasi hana
budi kuzingatia masharti ya mkataba uliowekwa ili kuhakikisha kuwa kiwanda
hicho kinakamilika kwa wakati na kuweka kuleta tija iliyokusudiwa.
‘’Sijaridhishwa na
kasi ya ujenzi wa mradi huu, na nitoe maagizo kwa Jeshi la Magereza linalosimamia
ujenzi wa mradi huu kuhakikisha kuwa kunakuwepo na vifaa, vitendea kazi na
wataalamu wa kutosha katika maeneo yote ya ujenzi ili kuhakikisha kuwa tarehe 2
Februari mwaka huu mradi huu unakamilika na baadhi ya mashine zinaanza
kusimikwa’’ alisema Waziri Mhagama.
Aidha Waziri Mhagama
alisema iwapo mradi wa ujenzi innaonekana ni mkubwa, Serikali itawaruhusu
wakandarasi mbadala ikiwemo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Shirika la
Mzinga, na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kuifanya kazi hiyo ili kukamilika kwa
wakati na muda uliopangwa kwani Serikali kupitia kiwanda hicho imekusudia
kutengeneza ajira na mapato ya fedha za kigeni.
Akifafanua zaidi
Waziri Mhagama alisema mwishoni mwa wiki hii Ofisi yake inatarajia kupokea
mashine za mradi huo na kuzikagua, hivyo ni wajibu wa mkandarasi wa mradi
kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo kwa kuwa Serikali kupitia PSSSF kwa upande
wake imetekeleza wajibu wake kwa kutoa fedha zilizohitajika hadi kufikia hatua
iliyopo.
Waziri Mhagama pia
alizitaka taasisi zote zinazohusika katika mradi huo ikiwemo PSSSF, Shirika la
Maendeleo ya Utafiti wa Viwanda Tanzania (TIRDO) pamoja na Jeshi la Magereza
Nchini kusimamia kwa ukamilifu vifungu vya kitaalamu ili kuufanya mradi huo
ukamilike kwa wakati, kwani Serikali haipo tayari kulipa fidia ya gharama za usimakaji
wa mashine ikisubiri kukamilishwa kwa ujenzi wa kiwanda hicho.
Kwa upande Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Nchini, Hamis Nkubasi alisema Jeshi
hilo limepokea maelekezo yote ya Serikali na imejipanga kuhakikisha kuwa mradi
huo unakamilika kwa wakati ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Hosea
Kashimba alisema hadi sasa Ofisi yake imetoa kiasi cha Tsh Milioni 200
zilizotumika kwa ajili ya ununuzi wa malighafi zote muhimu zilizohitajika
katika hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi huo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu)
Jenista Mhagama amesema Serikali haijaridhika na kasi ya utekelezaji wa mradi
wa ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga katika Gereza la Karanga Mkoani
Kilimananjaro na kumtaka mkandarasi kuikamlisha kazi hiyo kabla ya tarehe 2
Februari mwaka huu.
Alisema kuwa Ofisi
yake imejipanga kuhakikisha kuwa itatekeleza maelekezo yote yatakayolewa na
Serikali na yanayohitajika kwa mkandarasi ili kuhakikisha kuwa mradi huo
unakamilika katika muda na wakati uliopangwa kwa mujibu wa Mkataba.
No comments:
Post a Comment