Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali [GCLA] ipo katika
mkakati wa kuanzisha Kanzi Data ya taifa ya Vinasaba vya Binadamu
[DNA] ambayo itakuwa ikitambua asili ya kila Mtanzania na kuweza
kusaidia chunguzi mbalimbali ikiwemo majanga na kupata majibu kwa kina.
Hayo
yameelezwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko wakati
wa ziara ya kampeni ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano
inayojulikana kama ‘Tunaboresha Sekta ya Afya’ ambapo amesema kuwa;
Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha wanafikia malengo ya kusaidia jamii katika upande huo wa vinasaba.
"Kwa
sasa tupo katika mpango wa kuanzisha Kanzi Data ya Taifa ya Vinasaba
ambapo eneo hilo kwa sasa tutaliwekea kipaumbele katika bajeti ya fedha
ya mwaka huu na tayari tumeshaanza kutengeneza mpango kazi wazo dhana
ya utengenezaji wake na itajumlisha wadau mbalimbali na Serikali
kupitia Wizara ya Afya na wadau wengine". Alisema Mkemia Mkuu wa
Serikali Dkt. Mafumiko.
Mkurugenzi anayesimamia Idara ya Huduma ya usimamizi wa vinasaba, David Eliasi akizungumza katika tukio hilo. |
Dkt. Mafumiko
amebainisha kuwa, kutokana na mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano kwa
kuboresha rasilimali watu, miundombinu ya utendeajji kazi na vifaa vya
kisasa ndio maana wamepewa jukumu hilo la kuanzishwa kwa Kanzi data
hiyo sambamba na kujumuisha wadau mbalimbali.
Nae
Mkurugenzi anayesimamia Idara ya Huduma ya usimamizi wa vinasaba,
David Eliasi akizungumzia suala hilo la Kanzi data, amesema kuwa, Mkemia
wa Serikali ndio atakuwa msimamizi na inajengwa na watanznia wenyewe
huku akiwataka watanzania wajivunie juu ya hilo.
"Serikali
ya awamu ya Tano imeweza kuongeza chachu na sasa tunajenga kanzi data
ya Kitaifa ya Vinasaba na inajengwa na Watanzania wenyewe.
Ni
kitu cha kujivunia na timu ya Kitaifa inasimamia huu ujenzi wakiwemo
Wizara ya Afya ambayo ni mlezi wetu, pia wapo EGav- Serikali mtandao,
NIDA, RITA, NEC na taasisi nyingi tu na wote hao wamekaa pamoja na
wamekuja na dhana ya uanzishwaji wa Kanzi data hii ya Kitaifa" alisema
David Eliasi.
Ameongeza kuwa kuanzishwa kwa
kanzi data hiyo, itarahisisha upatikanaji wa haraka wa majibu ya
vinasaba kwani tayari sampuli zitakuwa zinapatikana kwenye data.
"Tutachukua
muda mfupi na wa haraka zaidi. Mfano lile janga la Morogoro la moto,
ndugu wa marehemu wangepatikana kupitia kanzi data hii na tungelipata
majibu kwa haraka na kwa wingi zaidi" alisema Davidi Eliasi.
Aidha,
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imenunua mitambo tisa
kwa gharama ya shilingi bilioni 9.5 kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa
kemikali, sumu, madawa ya kulevya na viambata.
Ambapo pia imeweza kusajili wadau 2426 mwaka 2019 kutoka wadau 4340 mwaka 2015/2016.
Mpaka
sasa Mamlaka hiyo ya Mkemia Mkuu imeendelea kuboresha huduma zake
ikiwemo katika Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Nyanda za Juu Kusini na maeneo
mengine ya Kanda.
No comments:
Post a Comment