|
Waziri wa
Madini Doto Biteko akiieleza jambo Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini wakati
wizara ilipowasilisha kwa kamati hiyo Taarifa kuhusu Utekelezaji na Hali ya Upatikanaji wa
Fedha za Maendeleo ya STAMICO kwa
Kipindi cha Nusu Mwaka, kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.
Imeelezwa kuwa, Shirika la Madini la
Taifa (STAMICO) lipo katika hatua za awali za uanzishwaji wa Mradi wa Kusafisha
Dhahabu (Gold Refinery) na tayari kampuni ya ubia ijulikanayo kama Mwanza
Precious Metals Refinery Company Limited imeanzishwa.
Hayo
yamebainishwa leo Januari 21, 2020 na Kaimu Mtendaji Mkuu wa (STAMICO)
Dkt. Venance Mwase wakati akiwasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati na Madini Taarifa kuhusu
Utekelezaji na Hali ya Upatikanaji wa Fedha za Maendeleo ya shirika hilo
kwa Kipindi cha Nusu Mwaka, kwa Mwaka wa
Fedha 2019/2020 kwa niaba ya Waziri wa Madini.
|
|
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dustan Kitandula akieleza
jambo baada ya Wizara kuwasilisha kwa kamati hiyo Taarifa
kuhusu Utekelezaji na Hali ya Upatikanaji wa Fedha za Maendeleo ya STAMICO hilo kwa Kipindi cha Nusu Mwaka, kwa Mwaka wa Fedha
2019/2020.
|
Dkt. Venance ameileza kamati hiyo
kuwa, mradi huo utaendeshwa kwa ubia
ambapo STAMICO itakuwa na hisa asilimia
25 na mwekezaji asilimia 75, huku ikilelezwa kwamba, mradi huo utakaojengwa jijini Mwanza utahusisha kujenga
mtambo wenye uwezo wa kusafisha wastani wa kilo 200 hadi 500 kwa siku.
Ameongeza kuwa, makadirio ya fedha
zinazohitajika ni Dola la Marekani
Milioni 58.204 ambazo zimepangwa kwa ajili ya ununuzi wa mtambo wa
kusafishia dhahabu, gharama za awali za mradi, kununua dhahabu kutoka katika
masoko pamoja na gharama zaza uendeshaji na kuongeza‘’ Mheshimiwa Mwenyekiti
tumepanga uwe mtambo wa viwango vya kimataifa,’’.
|
Baadhi ya
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini (mstari wa mbele) na
Maafisa kutoka Wizara ya Madini na Taasisi zake wakifuatilia uwasilishaji wa
Taarifa ya STAMICO kwa kamati hiyo.
|
Aidha, Dkt. Mwase amesema kwamba
katika kipindi cha Julai hadi Desemba, 2019, tayari mradi umetekeleza majukumu
kadhaa ikiwemo kupata leseni ya kujenga na kuendesha mtambo huo, kusainiwa mkataba
wa ubia pamoja na kuanza taratibu za uanzishwaji wa kampuni ya ubia na kupata
eneo la ujenzi wa mtambo chini EPZA.
Ameongeza majukumu mengine
yaliyotekelezwa ni pamoja na kufanyika kwa Athari kwa Mazingira (EIA) kwenye
eneo la mradi upembuzi yakinifu pamoja na kukusanya taarifa za upatikanaji wa dhahabu
katika maeneo mbalimbali yanayokusudiwa.
|
Waziri wa
Madini Doto Biteko akiieleza jambo Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini wakati
wizara ilipowasilisha kwa kamati hiyo Taarifa kuhusu Utekelezaji na Hali ya Upatikanaji wa
Fedha za Maendeleo ya STAMICO kwa
Kipindi cha Nusu Mwaka, kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.
|
Akizungumzia shughuli nyingine
zinazoendeshwa na Shirika hilo amesema linaendelea kutoa huduma za Kibiashara
za uchorongaji miamba wa biashara katika sekta ya mafuta na gesi ambapo katika
Mwaka wa Fedha 2019/20 ambapo limefanikiwa
kupata kandarasi 4 za uchorongaji
kupitia zabuni mbalimbali zenye thamani
ya shilingi bilioni 2.2 .
Kuhusu Mgodi wa Stamigold ambao ni Kampuni
Tanzu ya Shirika hilo ameieleza kamati hiyo kuwa, kuanzia Julai hadi |Desemba,
2019, mgodi huo umezalisha na kuuza wakia
7,133.00 za madini ya dhahabu na wakia
879.19 za madini ya fedha, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 24,172,700,255.34.
‘’ Mhehimiwa Mwenyekiti, katika
kipindi hicho, mgodi umelipa jumla ya shilingi 1,712,455, 550.91 kwa ajili ya malipo ya mrabaha, ada ya ukaguzi na
kibali cha kusafirisha madini nje ya nchi,’’ ameeleza Dkt. Venance.
|
Waziri wa
Madini Doto Biteko akiieleza jambo Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini wakati
wizara ilipowasilisha kwa kamati hiyo Taarifa kuhusu Utekelezaji na Hali ya Upatikanaji wa
Fedha za Maendeleo ya STAMICO kwa
Kipindi cha Nusu Mwaka, kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.
Kuhusu mradi wa makaa ya mawe katika
Mradi wa Kabulo na Kiwira, amesema jumla ya tani 4,359.10 ziliuzwa na kulipatia Shirika kiasi cha shilingi 17,558,184.76 na kuongeza
kuwa, ‘’ shirika lilifanikiwa kulipa mrabaha, ada ya ukaguzi na tozo ya
Halmashauri ya jumla ya shilingi
23,645,000.62
Aidha ameongeza kuwa Mgodi umeendelea
kutoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 400.
Kwa upande wake, Waziri wa Madini Doto
Biteko wakati akitoa ufafanuzi wa hoja zilizoibuliwa na kamati, amewatoa Hofu Wajumbe
wa kamati hiyo kuhusu Maendeleo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambapo
ameeleza pamoja na changamoto zinazolikabili, linakua na linafanya vizuri.
Waziri Biteko ameiomba Kamati hiyo
kuendelea kuilea na kuishauri STAMICO
kwa kuwa mwelekeo wake ni mzuri na kwamba hivi sasa lina uwezo wa
kuzalisha hadi shilingi Bilioni 20
tofauti na ilivyokuwa awali na kuongeza kuwa, Watendaji na Bodi ya Shirika hilo
mara zote wanafanyia kazi ushauri unaotolewa na Kamati pamoja na Wizara.
‘’Mheshimiwa Mwenyekiti, itakuwa
bahati mbaya sana kulifuta shirika hili. Linakua, wanaendelea vizuri na Wana
Bodi nzuri, watendaji wanasikiliza ushauri na kuufanyia kazi na mapungufu
yanafanyiwa kazi, naomba muendelee kuilea na kuishauri STAMICO,’’amesisitiza
Waziri Biteko.
|
No comments:
Post a Comment