Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jmaii, Jinsia, Wazee
na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amesema Serikali imeichukua Kampeni ya kuhamisha
wananchi kujenga nyumba bora iitwayo “Piga
Kazi: Boresha Makazi” kuwa Agenda ya kitaifa kwa miaka mitatu ijayo.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo jijini Ddooma mara
baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu na Bajeti kwa kipindi
cha nusu Mwaka (Julai-Disemba 2019) kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma na
Maendeleo ya Jamii kwa upande wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
Waziri
Ummy amesema kuwa Kampeni ya Makazi Bora ni jambo ambalo Wizara
imelihamasisha katika kipindi cha nusu mwaka na katika utekelezaji
walichagua baadhi ya mikoa
kuanza kwa mfano kujenga nyumba bora kwa wasiojiweza na kuhamasiaha
wanaojiweza
kujenga na kuisambaza nchini nzima ili kuwezesha wananchi kuboresha
makazi
yao.
“Kampeni hii yenye Kauli mbiu “Piga Kazi: Boresha Makazi” inalenga kupunguza Kaya zenye makazi duni kwa
silimia 50 kutoka asilimia 15.9 ya sasa hadi kufikia asilimia 8 ifikapo mwaka
2022” alisema Waziri Ummy
Aidha Waziri Ummy amesema wananchi wakiboresha makazi
itasaidia kuondokana na maradhi mablimbali ikiwemo kifua kikuuu na kuwezesha
jamii kuwa na sehemu salama za kulala hivyo kupunguza magonjwa yanayotokana na
uchafu na kukosa hewasafi.
“Nisema tu tatizo sio wananchi kuwa masikini ila
bado hatujapanga kuwa na vipaumbele gani sisi kama Wizara tutahamasisha suala
la ujenzi wa Nyumba Bora kuwa kipaumbele kwa wananchi katika maeneo yao.” Alisema
Waziri Ummy.
Akifafanua kuhusu Kampeni ya kuhamasisha Makazi
Bora kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Katibu Mkuu
Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu
amesema kuwa kampeni hiyo ikibebwa na viongozi wa mikoa na wilaya husika
itasaidia kuhamaisha wananchi walio wengi katika kuboresha makazi yao kwani
viongozi hao wanazungumza na wananchi kila siku.
“Agenda hii ya ujenzi wa Makazi Bora tutaipeleka
hadi kwa viongozi wa dini ili wawe wanahubiri kwa waumini faida za kuwa na
nyumba bora itasaida kubadilisha wananchi na tutafanikiwa katika hili” alisema
Dkt. Jingu
Kwa upande wake Mbunge wa Temeke Mhe. Abdallah
Mtolea amesema kuwa Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa kati itawezekana ikiwa
wananchi watahamasishwa kujenga nyumba bora kwani uchumi wa viwanda na wa kati
unaanza na wananchi kuwa katika mazingira bora ya malazi.
Naye Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia alisisitiza
Serikali kuipa nguvu Kampeni hii ya kuboresha makazi kwani wananchi walio wengi
wamekuwa na kipato kizuri ila bado hawana elimu ya umuhimu wa kuwa na nyumba
bora.
Kampeni ya kuboresha makazi imewezesha kufikia
wakazi wa Kata ya Mzenga Kisarawe mkoa wa Pwani , Mpandandogo na Kabungu mkoani
Katavi, Ikungi na Chibumagwa mkoani Singida na imelenga kufikia mikoa 26 ya
Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment