Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti
Rebeka Msambusi akiongea na waandishi wa habari wa mikoa ya Mbeya na Iringa juu ya fursa za kiutalii zinavyokuza uchumi wa mwananchi moja moja na jamii kwa ujumla.
Paulina Boma mfanyabiashara wa Mugumu Serengeti akizungumza waandishi wa habari mikoa ya Mbeya na
Iringa juu ya fursa za kiutalii zinavyokuza uchumi wa mwananchi moja moja na jamii kwa ujumla.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Rebeka Msambusi akiongea na waandishi wa habari wa mikoa ya Mbeya na Iringa juu ya fursa za kiutalii zinavyokuza uchumi wa mwananchi moja moja na jamii kwa ujumla.
NA
FREDY MGUNDA,IRINGA.
Wananchi
wanaozungukwa na hifadhi za taifa wametakiwa kutumia fursa za kiuchumi ambazo
zinapatikana katika hifadhi hizo ili kuleta
maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.
Akizungumza
waandishi wa habari mikoa ya Mbeya na Iringa Paulina Boma mfanyabiashara wa Mugumu
Serengeti alisema kuwa amefanikiwa kupata mafanikio mengi kutokana na biashara
ya bidhaa za kitalii katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.
“Nimefanikiwa
kupitia uuzaji wa bidhaa za kitalii kwa kuwasomesha watoto wangu wane kwa ngazi
ya chuo kikuu na wengine wanaendelea kusoma ngazi za chini za elimu ya
sekondari,lakini pia nimewasidia vijana wengine kuwaongezea elimu kwenye vyuo
mbalimbali kulingana na vipaji vyao” alisema Boma
Boma aliongeza
kwa kusema kuwa kupitia biashara ya kuuza bidhaa za kitamaduni kwa watalii
wanatembelea hifadhi hiyo amefanikiwa kujenga nyumba nne na amenunua gari kwa
ajili ya shuguli zake binafsi na ndoto zake ni kuhakikisha anakuwa na kampuni
ya utalii ambayo itamuongezea kipato na kuleta maendeleo kwa taifa kwa ujumla.
Aidha Boma
aliwataka wananchi wa mikoa ambayo inazungukwa na hifadhi za taifa kuchangamkia
fursa zilizoko kwenye hifadhi hizo ili kuleta maendeleo binafsi na taifa kwa
ujumla.
“Kwenye
hifadhi hizi kuna kila aina ya fursa za kibiashara ambazo zipo wazi kwa kila
mtanzania anaweza kuzitumia hivyo watanzania wanatakiwa kuwa wabunifu tu,labda
ukiangalia bidhaa nazoziuza hapa nazinunua katika mikoa ya nyanda za juu
kusini,Iringa,Mbeya,Njombe na songwe na nakuja kuziuza huku hivyo hata wao
wanaweza kuziuza kwa watalii wanaotembelea vivutio vya mikoa yao” alisema Boma
Lakini
Boma aliwataka wanaume kuwaruhusu wanawake kufanya shughuli za kiamendeleo kwa
kuwa wanauwezo wa kufanya kazi na kuongeza kipato kwenye familia hivyo ukimpa
fursa mwanamke basi umeikomboa jamii kwa ujumla.
“Niwaombe
wananchi wa nyanda za juu kusini waje huku kaskazini wajifunze shughuli hizi za
kitamaduni ambazo tumekuwa tukiwauzia watalii mbalimbali na kupata faida ambayo
imekuwa inaendesha maisha yangu vizuri na kuchangia maendeleo ya taifa” alisema
Boma
Kwa upande
wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Rebeka msambusi alisema
kuwa utalii umesaidia kukuza uchumi kwa wananchi wa wilaya hiyo kutokana na
kuuza bidhaa mbalimbali kwa watalii.
“Saizi wanauza
vyakula mbalimbali kwenye hotel na kambi za kitalii ambazo zipo hifadhi ya
taifa ya Serengeti na usafiri pia umechangia kukuza uchumi wa wananchi” alisema
Msambusi
Msambusi
aliwataka wananchi wa nyanda za juu kusini kuchangamkia fursa zilizopo katika
hifadhi ya taifa ya Ruaha ili kukuza uchumi kama ilivyo katika mikoa ya
kaskazini ambao wamekuwa wakitumia vizuri fursa ya utalii kwa kujipatia
maendeleo.
Ikumbukwe
kuwa Hifadhi ya Ruaha ndiyo hifadhi kubwa kuliko
zote Tanzania ambapo ina ukubwa wa kilomita za mraba 20,226 na ni ya pili kwa
ukubwa katika Bara la Afrika baada ya hifadhi ya Kafue iliyopo nchini Zambia.
Ni maarufu kwa kuwa na
wanyama aina ya Kudu wakubwa na wadogo ambao hupatikana kwa wingi ambapo
hustawi wa hifadhi hii unategemea mto ruaha ambao aina mbalimbali za Samaki,
Mamba na viboko hupatikana katika mto huu.
Wanyama kama Pofu na swala
hunywa maji katika mto huo wa Ruaha ambao ni mawindo makubwa ya wanyama wakali
wakiwemo Simba, Chui, Mbweha, Fisi na Mbwa mwitu. Pia eneo hili Tembo
hukusanyika kwa wingi kuliko eneo lolote la hifadhi zilizopo katika nchi za
Afrika Mashariki.
Katika hifadhi hii utajionea
Magofu yanayosadikiwa kuwa yalikuwa makazi ya watu wa kale katika Kijiji cha
Isimila kiasi cha Kilomita 120 kutoka Iringa. Magofu haya ni miongoni mwa
historia ya kale barani Afrika.
Wakati mzuri wa kutembelea
hifadhi hii ili kuangaliwa wanyama wakubwa ni wakati wa kiangazi kuanzia Mei
hadi Desemba, lakini kuangalia ndege na maua wakati wa masika ni Januari –April
.
No comments:
Post a Comment