Balozi Seif Ali Iddi wan ne kutoka Kulia akiwa katika Picha ya
pamoja na Timu ya Msanii wa Kizazi Kipya Tanzania King Ali Kiba pamoja
na wenyeji wake wa Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema
Wasanii Nchini lazima wakumbuke kwamba wanabeba jukumu kubwa ndani ya
Jamii katika sanaa yao wanayopaswa zaidi kuifanya katika misingi ya
Kuelimisha.
Alisema sanaa licha ya kuchukuwa nafasi kubwa katika njia ya kutoa
burudani lakini pia ina nafasi pana zaidi iwapo itatumiwa katika kutoa
Taaluma ambayo hufika kwa haraka kwa Wananchi waliowengi.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar
wakati akizungumza na Msanii Maarufu Tanzania King Ali Kiba aliyepo
Zanzibar kusaidia Jamii akiwa katika Kampeni yake Maalum aliyoianzisha
iitwayo Ali Kiba un forgettable.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akizungumza na
Msanii Maarufu wa Kizazi Kipya Tanzania King Ali Kiba wa kwanza Kushoto
aliyepo Zanzibar na Kampeni yake ya Un Forgettable. Aliye katiu kati ni
Mkurugenzi Mkuu wa Zanzibar Cable Television {ZCTV} Mohammed Abdullah Al
– Jabir.
“ Itapendeza zaidi kama Jamii itaendelea kushuhudia Sanaa inatumiwa
vyema katika kuelimisha Jamii kwa vile ni moja ya sehemu inayoweza
kufundisha kwa urahisi”. Alisisitiza Balozi Seif.
Alisema Wasanii wengi wa Kikazi Kipya hivi sasa wamekuwa wakilenga
zaidi kujishughulisha na nyimbo zinazokiuka maadili hasa eneo la mavazi
jambo ambalo ni hatari kuigwa mara moja na Watoto Wadogo wanaotegemewa
kuwa Taifa la hapo baadae.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimpongeza na kumshukuru Msanii
huyo wa Muziki wa Kizazi Kipya King Kiba kwa ubunifu wake wa kuisaidia
Jamii na kuamua kutenga sehemu ya Kipato chake kutokana na Sanaa
anayoiendeleza.
Msanii
Maarufu wa Kizazi Kipya Tanzania King Ali Kiba akielezea azma ya
Kampeni hiyo katika lengo la kuendelea kusaidia Jamii katika Huduma
muhimu za Afya.
Balozi Seif alimuhakikishia Msanii huyo kwamba Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar kwa vile inafahamu mchango mkubwa unaotolewa na Wasanii wa
fani mbali mbali Nchini kwa Jamii itaendelea kushirikiana nae katika
kuona Kampeni yake inafanikiwa na kufikia Malengo yake.
Balozi Seif ambae pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na
Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar alitoa pongezi Maalum kwa Msanii huyo
kwa uamuzi wake wa kushiriki kwenye Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 kutimia Miaka 56.
Mapema Msanii huyo wa Muziki wa Kizazi Kipya Nchini King Ali Kiba
alisema uamuzi wa kuunda Kampeni hiyo umelenga kuondoa dhana
iliyojengeka kwa baadhi ya Watu kufikiria kwamba Muziki ni sehemu ya
uhuni.
King Kiba alisema Muziki hutoa ajira nyingi kwa kundi kubwa la Vijana
walioamua kuendesha maisha yao kupitia Sanaa zilizomo ndani ya sekta ya
ujasiri Amali.
Alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Kampeni yao kwa
jamii iliyolenga zaidi kutoa huduma za Afya katika upimaji bure pia
huwatembelea Wanafunzi wa Vyuo Vikuu katika dhana nzima ya kuwajengea
uwezo zaidi wa kukabiliana na Mafunzo yao.
Naye Meneja wa Kampeni hiyo Anti Esi Mgimba alisema watafuaria kuona
wanaendelea kushikwa mkono katika Kampeni hiyo inayowagusa moja kwa Moja
Wananchi wa Maisha ya kawaida.
Esi alisema King Ali Kiba amepewa Ubalozi wa Utalii Zanzibar kazi
aliyoikubali na kuiridhia kutokana na mapenzi yake makuwa kwa Wananchi
wa Zanzibar lakini bado amekuwa na ushirikiano mdogo kwa baadhi ya wadau
katika kufanikisha jukumu hilo kubwa la Taifa.
King Ali Kiba yupo Zanzibar na Kampeni yake ya Ali Kiba Un
forgettable chini ya uenyeji wa Mkurugenzi Mkuu wa Zanzibar Cable
Television {ZCTV} Mohammed Abdullah Al - Jabir.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
13/01/2020.
No comments:
Post a Comment