Wednesday, February 26, 2020
BOTI YA ZANZIBAR 2 KUWASILI MACHI 2020
Kampuni ya usafirishaji baharini Ukanda wa Afrika Mashariki, Zanzibar Fast Ferries inatarajiwa kupokea boti yake mpya na ya kisasa yenye kasi (Speed boat ) Zanzibar 2 katikati ya Mwezi wa Tatu (Machi) mwaka huu.
Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Zanzibar Fast Ferries, Eng. Haji Vuai amebainisha kuwa, tayari boti hiyo imeshapakiwa na imeanza safari ya kuja Zanzibar.
"Tuna furaha kuwajulisha wateja wetu wote kwamba boti yetu mpya ya pili kutoka Coco Yatch, Zanzibar 2, imeshapakiwa hapo jana jioni na meli iliyoibeba imeshaondoka nchini China na iko safarini kuja Zanzibar." Alisema Eng. Vuai.
NA ANDREW CHALE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment