Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo
akimpongeza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali
Charles Mbunge baada ya kuzindua Makao Makuu ya Jeshi hilo Wilayani
Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo amezindua Makao Makuu
ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Akizungumza Februari 26, 2020 wakati akizundua
makao makuu hayo Jenerali Mabeyo amesema kuwa, JKT imekuwa yakupigiwa mfano kwa utendaji unaotokana na utekelezaji mzuri wa miradi yote waliyokabidhiwa.
“Nawapongeza JKT kwa kutekeleza kikamilifu miradi ya
ujenzi wa ukuta wa Mirerani, Ujenzi wa ukuta wa Ikulu ya Chamwino, Ujenzi wa
ukuta wa uwanja wa ndege Ngerengere,Ukamilishaji wa nyumba za Jeshi la Magereza
Ukonga Jijini Dar es Salaam na miradi yote mliyokabidhiwa mlitekeleza kwa
wakati, ubora na viwango hali iliyowajengea heshima “, Alisisitiza
Jenerali Mabeyo
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo akipanda
mti ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT) Wilayani Chamwino mkoani Dodoma Februari 26, 2020.
Akifafanua Jenerali Mabeyo amesema kuwa ni wakati
muafaka kwa JKT kujipanga kwa kujiimarisha kwa kununua mitambo na vifaa zaidi
ili kujenga uwezo wa kuendelea
kutekeleza miradi mikubwa pasipo kutegemea vifaa na nyenzo za kukodi au
kuazima.
Aliongeza kuwa ili kuendelea kujenga heshima ya
JKT kwa Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. John Pombe Magufuli ni vyema utekelezaji wa miradi yote
ukaendelea kuwa katika ubora unaotakiwa, uzingatiaji wa Sheria ya manunuzi na
taratibu zote zilizowekwa na Serikali.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo akikata
utepe kuzindua Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilayani
Chamwino mkoani Dodoma Februari 26, 2020.
Aidha, Jenerali Mabeyo amewaasa Maafisa na Watumishi
wa Umma watakaotumia majengo ya makao makuu hayo kuyatunza ili yaweze kudumu
kwa kuwa ujenzi wake umetumia rasilimali nyingi.
Katika hatua nyingine Jenerali Mabeyo amesema kuwa
JKT inapaswa kujipanga kwa kuwa itahusika katika kutekeleza mradi wa ujenzi wa
Makao Makuu ya Ulizi wa Taifa katika Wilaya hiyo.
Sehemu ya Maofisa wa ngazi mbalimbali wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo Wilayani
Chamwino Mkoani Dodoma.
Uzinduzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa
JKT umefanyika Bwigiri Wilayani Chamwino mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Wakuu
wa Jeshi hilo wastaafu, Maafisa wa ngazi mbalimbali,ss Watumishi wa Umma,
Wananchi na viongozi wa Wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment