|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, akisalimiana na Wajumbe wa Mkutano wa Mtandao wa Viongozi
wanawake Afrika kwenye Uzinduzi wa Mtandao wa Viongozi wanawake Afrika
Tawi la Tanzania katika Ukumbi wa St. Gaspar Jijini bin Dodoma leo
Febuari 26,2020 ambapo kauli mbiu ya Mtandao huo ni Wananwake na Uongozi
Twende Pamoja Wakati ni huu. |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Mtandao wa Viongozi wanawake Afrika Tawi la Tanzania katika Ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma leo Febuari 26,2020 ambapo kauli mbiu ya Mtandao huo ni Wananwake na Uongozi Twende Pamoja Wakati ni huu.
|
|
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizindua Mtandao wa Viongozi wanawake Afrika Tawi la Tanzania katika
Ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma leo Febuari 26,2020 ambapo kauli mbiu
ya Mtandao huo ni Wananwake na Uongozi Twende Pamoja Wakati ni huu. |
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassani amesema kuwa katika nchi nyingi Duniani bado usawa wa kijinsia haujafikiwa katika nyanja nyingi ikiwemo katika uongozi na kuongeza kuwa hali hiyo pia inagusa nchi ya Tanzania ingawa kwa kiasi kikubwa inafanya vizuri.
Makamu wa Rais amezungumza hayo leo katika uzinduzi wa Mtandao wa Viongozi wanawake Afrika Tawi la Tanzania
katika Ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.
Aidha Makamu wa Rais amesema kuwa Tanzania inafanya vizuri ukilinganisha na nchi nyingine Barani Afrika na kutolea mfano katika mihimili ya dola "kumekuwa
na mabadiliko makubwa ya uwiano wa kijinsia, Kwa upande wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, kati ya wabunge 393,
wabunge wanawake ni 126 ambao ni
sawa na asilimia 36.7, na Baraza la
Wawakilishi la Zanzibar wanawake ni
asilimia 38" Amesema Makamu wa Rais
Ameongeza kuwa Kiwango hicho ni juu ya
uwiano uliowekwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC) cha angalau asilimia 30.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa Mtandao wa Viongozi
wanawake Afrika kwenye Uzinduzi wa Mtandao wa Viongozi wanawake Afrika
Tawi la Tanzania katika Ukumbi wa St. Gaspar Jijini bin Dodoma leo
Febuari 26,2020 ambapo kauli mbiu ya Mtandao huo ni Wananwake na Uongozi
Twende Pamoja Wakati ni huu. |
No comments:
Post a Comment