Waziri wa
Nishati Dkt Medard Kalemani amewaagiza wakandarasi wanaotekeleza mradi wa ujenzi
wa kituo cha kupoza umeme kilichopo Nyakanazi wilayani Biharamulo, kukamilisha
kazi hiyo ifikapo Novemba mwaka huu badala ya Januari 2021, kama ilivyo kwenye
mkataba.
Pia, ameagiza
mradi mwingine unaotekelezwa sambamba na huo ukihusisha ujenzi wa njia ya
kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Geita hadi Nyakanazi, ukamilike
Januari 2021 badala ya Machi mwaka huo.
|
Waziri wa Nishati Dkt
Medard Kalemani (katikati), akiangalia mchoro wa ramani ya kituo cha kupoza
umeme kinachojengwa Nyakanazi, wilayani Biharamulo alipotembelea eneo hilo
Februari 25, kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi husika. |
Alitoa maagizo hayo
Februari 25 mwaka huu, alipotembelea eneo kinapojengwa kituo hicho cha kupoza
umeme, ambacho ni sehemu ya mradi mkubwa wa kusafirisha na kusambaza umeme
unaotekelezwa na serikali kutoka Kigoma – Nyakanazi – Geita – Bulyanhulu kwa
gharama ya shilingi bilioni 93.27 za Tanzania.
Akifafanua
sababu za kutoa maelekezo hayo, Dkt Kalemani alisema ni kutokana na umuhimu wa
kukamilika kwa mradi huo mapema ambao unatarajiwa kutatua changamoto mbalimbali
za upatikanaji umeme ambazo wamekuwa wakizipata wakazi wa maeneo husika.
|
Msimamizi wa Mradi wa
Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme Nyakanazi, Mhandisi Elias Makunga (wa
tatu-kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kulia)
kuhusu maendeleo ya mradi huo. Waziri alitembelea eneo hilo kujionea maendeleo
yake, Februari 25, 2020.
Sambamba na
hilo, pia Waziri alisema ni kutokana na imani aliyonayo kwa Mkandarasi husika (M/s
Kalpataru Power Transmission Limited – India) kutokana na historia ya kazi
alizotekeleza awali hapa nchini.
“Hii kampuni
inayojenga mradi wa kusafirisha umeme, ndiyo ilijenga mradi wa Makambako –
Songea na walikamilisha kazi mwezi mmoja kabla ya mkataba kuisha kama
nilivyowaelekeza. Kutokana na uzoefu walionao, naamini hata kazi hii wana uwezo
wa kuikamilisha kabla ya muda.”
| |
|
Waziri wa Nishati Dkt
Medard Kalemani (katikati), akitoa maelekezo kwa uongozi wa TANESCO na
wakandarasi wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Nyakanazi,
Februari 25 mwwaka huu, alizuru eneo hilo lililopo wilayani Biharamulo kujionea
maendeleo yake. |
Akieleza zaidi
kuhusu mradi husika, Waziri Kalemani alisema ni kati ya miradi mikubwa ya
vielelezo katika masuala ya kuzalisha, kufua, kusafirisha pamoja na kusambaza
umeme ambayo inatekelezwa na serikali.
Kuhusu
utekelezaji wake, Waziri alieleza kuwa umegawanyika katika sehemu tatu, ya
kwanza ikihusisha mikoa ya Iringa – Mbeya mpaka Tunduma (kilovoti 400), ambapo
utekelezaji wake umeshaanza.
Alisema sehemu
ya pili ni kutoka Sumbawanga kupitia Mpanda hadi Kigoma ambapo kwa upande wa
Kigoma (Kidahwe) kutajengwa Kituo kikubwa cha kupoza umeme.
|
Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Raymond Seya (katikati), akijadiliana jambo na Meneja
wa shirika hilo Kanda ya Ziwa, Mhandisi Maclean Mbonile (kushoto) na Meneja wa
Wilaya ya Biharamulo, Ernest Milyango wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati Dkt
Medard Kalemani (hayupo pichani), eneo kunapojengwa kituo cha kupoza umeme
Nyakanazi, wilayani Biharamulo, Februari 25, 2020.
“Sehemu ya tatu
ya mradi ndiyo hii kutoka Kigoma kuja hapa Nyakanazi umbali wa kilomita 280 na
kutoka hapa mpaka Geita umbali wa kilomita 144, pamoja na kutoka Geita hadi
Bulyanhulu, umbali wa kilomita 57.”
Aidha,
aliongeza kuwa, mradi huo pia utaungana na mradi wa kuzalisha umeme wa maji wa
Rusumo wenye megawati 27 kwa kila nchi husika (Tanzania, Rwanda na Burundi).
Alisema, itajengwa njia ya kusafirisha umeme kutoka Nyakanazi hadi Rusumo,
umbali wa kilomita 96.
|
|
Msimamizi wa miradi
ya Umeme Vijijini (REA) Kanda ya Ziwa, Mhandisi Ernest Makale (kushoto)
akiongozana na wakandarasi na wataalamu wengine kutoka TANESCO, wakati wa ziara
ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), eneo kunapojengwa
kituo cha kupoza umeme Nyakanazi, wilayani Biharamulo, Februari 25, 2020.
Vilevile,
Waziri Kalemani alieleza kuwa, Mradi huo utasambazia umeme vijiji takribani 31
ambako unatekelezwa kutoka Nyakanazi kupitia Bwanga (Chato) na maeneo
mbalimbali kwenda Katoro/Buseresere hadi Bulyahulu na kuongeza kuwa wananchi
wataunganishwa kwa gharama ya umeme vijijini (REA), ambayo ni shilingi 27,000
tu.
Alitumia fursa
hiyo kuwaalika wawekezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kujitokeza
kuwekeza katika maeneo yote
unakotekelezwa mradi akiwahakikishia kuwa kutakuwa na umeme wa uhakika,
unaotabirika na baadaye wenye gharama nafuu.
|
|
Kazi ya ujenzi wa
kituo cha kupoza umeme Nyakanazi wilayani Biharamulo ikiendelea. Taswira hii
ilichukuliwa wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani kujionea
maendeleo ya mradi huo, Februari 25 mwaka huu.
Kwa upande
wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Biharamulo Venance Martin, akimwakilisha Mkuu
wa Wilaya, alipongeza mikakati ya kusambaza umeme inayotekelezwa na serikali
huku akitolea mfano wa mradi huo ambao alisema mbali na kuwanufaisha wananchi,
utawezesha kukuza uchumi wa viwanda katika ukanda husika.
|
|
Kazi ya ujenzi wa
kituo cha kupoza umeme Nyakanazi wilayani Biharamulo ikiendelea. Taswira hii
ilichukuliwa wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani kujionea
maendeleo ya mradi huo, Februari 25 mwaka huu. | |
Veronica Simba – Biharamulo
Msimamizi wa
Mradi huo (Geita-Nyakanazi), Mhandisi Elias Makunga, alisema maagizo ya Waziri
yanatekelezeka na alimhakikishia kuwa atasimamia utekelezaji wake ipasavyo.
Katika ziara
hiyo Waziri alifuatana na viongozi na wataalamu mbalimbali akiwemo Mwakilishi
wa Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Dauson Kamaka, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Raymond
Seya, na Msimamizi wa Miradi ya REA
Kanda ya Ziwa, Mhandisi Ernest Makale.
No comments:
Post a Comment