Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Josephat Kandege ameelezea kuridhishwa kwake na miradi ya
barabara iliyotekelezwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tarura
katika Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.
Aliyasema hayo wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya
maendeleo Mkoani Mwanza ambapo ameeleza kuwa mafanikio yanayopatikana katika
Manispaa hiyo hasa katika miradi ya barabara yanatokana na ushirikiano
mkubwa uliopo kati ya wataalam wa TARURA na watumishi wengine wa Manispaa
kwa kufanya kazi pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi.
‘‘ Wote tumeshuhudia barabara hizi zilivyo kwenye kiwango, mafanikio
haya yanatokana na Umoja uliopo kwa watumishi wote wa Manispaa ya Ilemela
pamoja na watumishi wa TARURA kwani wanafanya kazi kwa pamoja ili
kuwaletea wananchi wetu maendeleo, kiujumla wanafanya vizuri’’Kandege.
Aidha amesisitiza kuwa miundombinu ya barabara inapokamilika ilindwe kwa
nguvu zote na amewaagiza viongozi husika huhakikisha barabara hizo zinafanyiwa
usafi mara kwa mara na kulinda miundombinu ya barabara hizo.
Naye Meneja wa TARURA Manispaa ya Ilemela Mhandisi Clement Kihinga
amesema kuwa barabara hizo zilizotekelezwa chini ya mradi wa Tanzania Strategic
Cities Project (TSP) zimekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kuinua uchumi wa
wananchi na kuboresha kiwango cha maisha ya wananchi.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanailinda miundmbinu
ya barabara ilizidumu na ziendelee kuboresha maisha yao na kurahisisha suala la
usafiri na usafirishaji katika Manispaa ya Ilemela.
‘‘Serikali inatumia gharama kubwa sana kujenga barabara hizi hivyo nitoe
wito kwa wananchi kuhakikisha kila mmoja wetu anashiriki kulinda miundombinu
hii ya barabara ’’ amesema Mtaalam huyo.
Mmoja wa wananchi wa Kiseke A Ilemela Issa Shabani alisema awali usafiri
ulikuwa changamoto sana Katika barabar yao kwani miundombinu ilikuwa mibovu
sana ila baada ya baraba ya kiseke Busweru kukamilika maisha yamepanda kiuchumi
“Sasa nafanya biashara yangu ya matunda hapa Busweru, nayabeba salama na
hayaharibiki kwani barabara ni nzuri na hata kipato changu kimeongezeka
hivyo naishukuru sana Serikali kwa kujenga barabara hii”Alisema
Shabani
Ziara ya Mhe, Kandege inaendelea Mkoani Mwanza ambapo miradi mbalibali
ya maendeleo zikiwemo barabara zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini
na Mijini TARURA inatarajiwa kukaguliwa.
No comments:
Post a Comment