|
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Matiti kutoka nchini Kenya, Dkt. Peter
Bird pamoja na timu ya wataalam bingwa wakishirikiana
kufanya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye titi bila kuharibu muonekano wa titi
(Breast conserving surgery).
Wataalam wa upasuaji,
radiolojia, patholojia, tiba ya mionzi na dawa wamekutana kwa lengo la
kujengeana uwezo ili kuboresha huduma za upasuaji kwa wagonjwa wanaogunduliwa
na saratani ya matiti mapema ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa takwimu
za Hospitali ya Taifa Muhimbili zinaonyesha kuwa wanaogunduliwa na saratani ya
matiti ni kati ya wanawake wenye umri wa miaka 40 hadi 80.
|
|
|
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila,
Dkt. Julieth Magandi akiwasilisha mada kuhusu hali ya saratani nchini katika
mafunzo ya wiki moja yaliyoandaliwa na Hospitali ya Muhimbili kwa kushirikiana
na kampuni ya dawa ya Roche ya nchini Kenya.
|
Hayo yamesemwa na
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt.
Julieth Magandi wakati akiwasilisha mada kuhusu hali ya ugonjwa wa saratani ya
matiti nchini katika mafunzo ya wiki moja iliyoandaliwa na Hospitali ya
Muhimbili kwa kushirikiana na kampuni ya dawa ya Roche ya nchini Kenya.
“Saratani ya
shingo ya kizazi ni ya kwanza ikifuatiwa na saratani ya matiti ambayo ni ya
pili kwa sasa, mwaka 2007 saratani ya ngozi (Kaposi Sarcoma) ilikuwa ya pili na
hivi sasa ni ya tatu kati ya magonjwa ya saratani yanayowapata wanawake” amesema
Dkt. Magandi.
Mtaalam wa
Upasuaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Caspar Haule ameelezea
mafanikio walioyapata kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu walipofanya mafunzo
Aprili, 2019 kuwa ni pamoja na kuweza kufanya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye
titi bila kuliondoa au kuharibu muonekano wake (Breast conserving surgery) kwa
wanawake 20.
|
Baadhi ya wataalam
kutoka hospitali mbalimbali nchini wakifuatilia mada zilikuwa zinawasilishwa
katika mafunzo hayo ya wiki moja.
“Ndani ya kipindi
cha mwaka mmoja toka Aprili 2019 tulipofanya uchunguzi kwa njia ya kisasa kwa
wanawake 162 na kuwafanyia upasuaji 152 ambapo kati ya hao 20 waliondolewa
vivimbe bila kuondoa titi lote” amesema Dkt. Haule.
“Timu ya Madaktari
Bingwa 12 kutoka hospitali mbalimbali nchini pamoja na madaktari wanafunzi 10 tumeanza
kufanya upasuaji mwingine kwa wanawake 8 ambao kati yao sita watafanyiwa
upasuaji wa kuondoa uvimbe bila kuharibu muonekano wa titi (Breast conserving
surgery) na wengine wawili watafanyiwa upasuaji wa kuondoa titi ambapo
tunatarajia baada ya upasuaji kufanyika wagonjwa hawa watapona ndani ya kipindi
cha kuanzia siku 10 hadi 14” ameeleza Dkt. Haule.
Kwa upande wake Daktari
Bingwa wa Tiba Radiolojia wa (MNH), Dkt. Flora Lwakatare ametaja kuwa pamoja na
mafanikio yaliyofikiwa bado kuna changamoto mbalimbali zinazopelekea madaktari
kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi nchini kama vile upungufu wa vifaa tiba na
mashine za kisasa zinazoweza kupima titi kabla ya kufanyiwa upasuaji, upungufu wa
wataalam bobezi na ukosefu wa warsha zinazohusu uchunguzi wa matiti.
Mafunzo hayo
imehusisha wataalam takribani 40 kutoka MNH-Upanga na Mloganzila, Kenya, Bugando,
KCMC, Mbeya, Ocean Road na Besta.
|
No comments:
Post a Comment