Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akionesha zawadi
ya fremu ya nembo ya Taifa iliyotengenezwa kwa madini alipotembelea mabanda
katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020,
uliofanyika JNICC Jijini Dar es Salaam, kulia ni Waziri wa Madini, Mhe. Doto
Biteko na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Simon Msanjira.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akiangalia
madini ya Tanzanite katika moja ya banda la mjasiriamali wa madini
alipotembelea mabanda hayo katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika
Sekta ya Madini Tanzania 2020, uliofanyika JNICC Jijini Dar es Salaam, kulia ni
Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Simon
Msanjira.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akipata maelezo
katika moja ya banda la mjasiriamali wa madini alipotembelea mabanda hayo
katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020,
uliofanyika JNICC Jijini Dar es Salaam, kulia ni spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai na kushoto ni Waziri wa Madini, Mhe. Doto
Biteko.
Waziri
wa Madini, Mhe. Doto Biteko akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa
Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, uliofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari, 23,
2020.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Madini kutoka Uganda, Mhe. Sara Opendi,
akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini
Tanzania 2020, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
leo Februari, 23, 2020.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akikata utupe
kuzindua Cheti cha uhalisia wa madini ya Bati katika Mkutano wa Kimataifa wa
Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania uliofanyika JNICC na kuhudhuriwa na
Nchi za Maziwa makuu 11 zinazozalisha madini ambazo zilikutana kujadili
mikakati ya kulinda rasilimali hiyo, kulia ni spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai na kushoto ni Waziri wa Madini, Mhe. Doto
Biteko.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akikabidhi cheti
kwa wawakilishi kutoka Nchi 11 za maziwa makuu zinazozalisha madini, mara baada
ya kuzindua cheti hicho katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Sekta ya
Madini uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere
Jijini Dar es Salaaam leo Februari 23, 2020.
Mhadhiri
kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi Kenya,
Prof. Patrick Lumumba akiwasilisha
mada katika Mkutano wa Kimataifa wa
Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, Prof.Lumumba aligusia jinsi
Afrika inaweza kunufaika na rasilimali ya hiyo, ambapo Tanzania imezindua rasmi
cheti cha uhalisia wa madini ya bati.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof.Adolf Mkenda akiwasilisha mada
katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini ulifanyika katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Prof.
Mkenda aligusia jitihada za Serikali katika kulinda rasilimali hiyo.
Mhadhiri
kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi Kenya, Prof. Patrick Lumumba akijibu swali kutoka kwa washiriki wa Mkutano
wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, lililotokana na
mada yake, Prof.Lumumba alizungumzia
kuhusu jinsi Afrika inaweza kunufaika na rasilimali ya hiyo, ambapo
Tanzania imezindua rasmi cheti cha uhalisia wa madini ya bati, kulia ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo.
Washiri
wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini wakifuatilia hotuba
ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipowakuwa akihutubia kufunga
mkutano huo JNICC Jijini Dar es Salaam, Februari 23, 2020.Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.
No comments:
Post a Comment