Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami
unaendelea zikiwemo barabara kuu, barabara
za mikoa na wilaya ambapo hadi Desemba 2019 mtandao wa barabara kuu umefikia km
8,67.
Amesema hayo
jijini Dodoma na kuongeza kuwa mtandao wa barabara za mikoa umefikia kilometa
1,808 ambapo barabara ya njia nane
kutoka Kimara hadi Kibaha ya kilometa 19
ujenzi wake umefikia asilimia 63 ameongeza kuwa ujenzi wa Ubungo Interchange ujenzi wake umefikia asilimia 65.
Akizungumzia
ujenzi wa madaraja amesema kuwa Serikali imeanza maandalizi ya ujenzi wa daraja
la Kigongo – Busisi Mkoani Mwanza lenye
urefu wa mita 3,200 na upana wa mita 28.45 ambapo malipo ya awali ya shilingi
bilioni 61.4 yamefanyika.
Waziri
Mpango amesema kuwa ujenzi wa daraja jipya la Selander unaendelea na umefikia
asilimia 25, ambapo ujenzi wa madaraja ya Mfugale na Mlalakuwa Dar es Salaam, daraja
la Magufuli katika mto Kilombero mkoani Morogoro
ambapo madaraja menginge ni daraja la Momba mkoani Rukwa, daraja la Sibiti mkoani Singida,
Mara mkoani Mara, daraja la Ruhuhu Ruvuma, ambapo madaraja mengine ni daraja la
Msingi mkoani Singida, daraja la Lukuledi
mkoani Lindi na daraja la Kavuu mkoani Katavi.
Aidha, amesema
kuwa ujenzi unaendelea wa madaraja ya Mangara mkoani Manyara ujenzi wake
umefikia asilimia 94, New Wami mkoani Pwani asilimia 35, na Kitengule mkoani
kagera Kagera ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 42.
Aidha,
Waziri Mpango amesema kuwa jumla ya
shilingi trilioni 3.60 zimetolewa katika kipindi cha Novemba 2015 hadi Januari
2020 kugharamia miradi ya barabara na
madaraja ikijumuisha shilingi bilioni 703.6 zilizotolewa katika kipindi cha
Julai 2019 hadi Januari 2020.
No comments:
Post a Comment