Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki, ametoa ushauri kwa wafanyabiara wa Tanzania wanaoagiza barakoa kutoka China kuhakikisha wananunua barakoa zenye viwango na ubora kutoka kwa Makampuni yaliyopewa idhini ya kuzalisha kwa madhumuni ya kuuza nje ya nchi yaan Surgical Mask zenye ubora ni zile zenye ngazi tatu (3 layers)
Mask zenye ngazi tatu (3 layers) |
Balozi
kairuki ametoa ushauri huo katika mtandao wake wa twitter ambapo
amesema kuwa ni vyema wafanyabiasha kuwa makini kwani uwepo wa
Makampuni yasiyo na sifa wala idhini ya kuzalisha barakoa kwa ajili ya
soko la nje na ambayo yanazalisha na kuuza barakoa zenye viwango duni
na hivyo kutoweza kufanya kazi iliyokusudiwa ya kumkinga mvaaji.
Waziri
Kairuki amesema kuwa barakao zisizo na sifa ni zile ambazo zina layer
moja ndani na kuongeza kuwa barakoa zinazotakiwa ni zile zenye layer
mbili ndani.
Mask yenye layers mbili ndani |
"Ukiagiza barakoa kutoka China hakikisha muuzaji anakupatia taarifa muhimu zifuatazo:jina la kampuni, leseni ya biashara, leseni ya usafirishaji, Lab test result, BFE at least 95% & FDA licence. Aidha, hakikisha kampuni inayotaka kukuuzia ipo kwenye orodha ya makampuni yanayoruhusiwa kusafrishwa" amesema Balozi Kairuki
No comments:
Post a Comment