Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula |
Rais Dkt. John Magufuli amemteua Dkt. Zainab Abdi
Seraphin Chaula kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano.
Kabla ya uteuzi huo,
Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na amechukua nafasi iliyoachwa na Dkt.
Maria Sasabo ambaye amestaafu.
Wakati huo huo,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Mabula Daudi Mchembe kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Kabla ya uteuzi huo,
Prof. Mabula Daudi Mchembe alikuwa Msaidizi wa Rais katika masuala ya afya.
Katika hatua nyingine,
Rais Magufuli amemteua Prof. Abel Makubi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali (Chief Medical Officer).
Kabla ya uteuzi huo,
Prof. Abel Makubi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda
Bugando na amechukua nafasi iliyoachwa na Prof. Mohamed Bakari Kambi ambaye
amestaafu.
Uteuzi wa viongozi
hao umeanza leo tarehe 22 Aprili, 2020.
No comments:
Post a Comment