Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na watumishi wa idara ya Sera na Mpingo katika ukumbi wa Wizara hiyo maarufu kama KILIMO IV Jijini Dodoma leo tarehe 22 Aprili 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na watumishi wa idara ya Sera na Mpingo katika ukumbi wa Wizara hiyo maarufu kama KILIMO IV Jijini Dodoma leo tarehe 22 Aprili 2020, Mwingine pichani ni Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb).
Sehemu ya watumishi wa Idara ya Sera na Mipango ya Wizara ya Kilimo wakifatilia kikao kazi kilichoongozwa na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) katika ukumbi wa Wizara hiyo maarufu kama KILIMO IV Jijini Dodoma leo tarehe 22 Aprili 2020.
Sehemu ya watumishi wa Idara ya Sera na Mipango ya Wizara ya Kilimo wakifatilia kikao kazi kilichoongozwa na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) katika ukumbi wa Wizara hiyo maarufu kama KILIMO IV Jijini Dodoma leo tarehe 22 Aprili 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Idara ya sera na mipango ya Wizara ya
Kilimo imetakiwa kubainisha kiasi gani cha fedha kimewekezwa Kwenye Kilimo
kutoka serikalini, sekta binafsi na washirika wa maendeleo.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa
Kilimo Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 22 Aprili 2020 wakati akizungumza na
watumishi wa idara hiyo katika ukumbi wa Wizara hiyo maarufu kama KILIMO IV
Jijini Dodoma.
Amesema kuwa pamoja na majukumu muhimu
yanayofanywa na Wizara ya Kilimo lakini idara hiyo inapaswa kuongeza juhudi na
weledi katika utendaji kazi wake wa kila siku ili kuongeza Tija na uzalishaji
wa mazao ya wakulima.
Waziri Hasunga ameitaka idara hiyo
kubainisha Takwimu mbalimbali za uzalishaji wa mazao, bei za mazao, uchambuzi,
ikiwa ni pamoja na takwimu za Mazao ya mboga, maua na matunda.
Alisema kuwa pamoja na mafanikio
makubwa ambayo yameonekana katika sekta ya kilimo katika kipindi cha miaka
minne ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe
Magufuli lakini bado sekta ya kilimo inapaswa kuimarishwa zaidi ili kuwa na
mafanikio makubwa zaidi katika kilimo.
“Nchi zilizoendelea Duniani zimefanya
nini na kwa nini Tanzania tupo nyuma Kwenye kilimo, na Kuna viwanda vingapi vya
kuchakata mazao ya Kilimo” Alihoji Mhe Hasunga wakati wa kikao kazi hicho
Katika hatua nyingine Waziri Hasunga
ameitaka idara hiyo kubainisha kuhusu Uongezaji thamani upoje na sera inasema
nini kuhusu uongezaji thamani wa mazao.
Kadhalika, Waziri wa Kilimo Japhet
Hasunga (Mb) ameitaka idara ya sera na mipango kubainisha kuwa Sera ya masoko ipoje
na wataalamu wanasemaje kuhusu hali ya masoko.
Pia ametaka kufahamu hali ikoje
kupitia sera ya usalama wa chakula, Sera ya Ushirika, Sera ya matumizi Bora ya
ardhi na Tunakwama wapi Kwenye kilimo
No comments:
Post a Comment