Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za
rambirambi kwa familia, Wabunge na Waumini wa Kanisa la Mlima wa Moto kufuatia
kifo cha Askofu Getrude Rwakatare kilichotokea tarehe 20 Aprili, 2020
Jijini Dar es Salaam.
Katika salamu hizo, Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa na kifo cha Askofu Getrude Rwakatare
ambaye amesema alikuwa mcha Mungu, mwenye upendo, asiye na majivuno,
aliyepigania umoja na amani na aliyeipenda nchi yake kwa dhati.
Pamoja na kutoa pole
kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, Mhe. Rais Magufuli amemuomba Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Yustino Ndugai kufikisha
salamu zake za pole kwa Wabunge wote na pia amewapa pole waumini wa Kanisa la
Mlima wa Moto ambalo Askofu Rwakatare alikuwa kiongozi wake.
“Katika kipindi hiki cha
majonzi, tumuombee Askofu Rwakatare apumzike mahali pema peponi, na nawasihi
Waumini wa Kanisa la Mlima wa Moto muendelee kuwa wamoja na muendeleze mazuri
yote yaliyofanywa na Mchungaji Rwakatare wakati wa uhai wake”
amesema Rais Magufuli.
Raha ya milele umpe
ee Bwana, na mwanga wa milele umuangazie, Marehemu Getrude Rwakatare astarehe
kwa amani, Amina.
No comments:
Post a Comment