Serikali imetangaza bei kikomo ya sukari nchini ambapo bei ya
rejareja haitazidi Sh 2600 kwa mikoa ya karibu kama Dar es Salaam na Sh 3200
kwa mikoa ya mbali kama Katavi.
Waziri wa Kilimo, Joseph Hasunga wa kulia akiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa |
Akitangaza bei hizo leo jijini Dodoma, Waziri wa Kilimo,
Joseph Hasunga amesema bei hizo zimezingatia umbali wa kila eneo katika mikoa
yote nchini.
Waziri Hasunga amesema serikali imefikia hatua hiyo baada ya
kubaini kuwa wafanyabiashara wa sukari wamepandisha bei kiholela kinyume na
utaratibu huku akitoa onyo kali kwa yoyote ambaye atakaidi bei iliyotolewa.
Waziri Hasunga emtangaza bei hiyo mpya ya sukari nchini baada
ya sukari kupanda ghafla katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Corona,
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent
Bashungwa ametoa onyo kwa wafanyabiashara ambao watapandisha bei kiholela.
No comments:
Post a Comment