|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.
Riziki Shemdoe wa kwanza kulia akiwa kwenye Mkutano wa Watalaam wa Mashirika ya
Viwango kutoka nchi 16 za Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya Video katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam,
Tanzania, wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania
(TBS), Bw.Athuman Ngenya.
|
Wazalishaji
wa Bidhaa mbalimbali nchini wametakiwa kuzalisha
kwa wingi bidhaa zilizokuwa zinaagizwa kutatoka Nje ya Nchi, kutokana na
kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa hizo kulikosababishwa na ugonjwa wa Corona,
pamoja na kuitumia fursa ya uwepo wa Bandari hasa kwaajili ya kuhudumia soko la
SADC.
Wito
huo umetolewa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na
Biashara, Prof. Riziki Shemdoe wakati akifungua Mkutano wa wataalam wa
Mashirika ya Viwango kwa nchi za SADC uliofanyika kwa njia ya Video katika
Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere JNICC.
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.
Riziki Shemdoe wa kushoto akifungua
Mkutano wa Watalaam wa Mashirika ya Viwango kutoka nchi 16 za Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya Video
katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam,
Tanzania, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS),
Bw.Athuman Ngenya.
|
Prof.Shemdoe
amesema kutokana na kufungwa kwa baadhi ya mipaka ya Nchi na upungufu wa upokeaji
wa bidhaa kutoka Nje, wakati sasa umefika kwa wazalishaji wa ndani kutumia fursa
hiyo kwaajili ya kuzalisha bidhaa kwa wingi zaidi.
“Tunatatizo
la Corona nchini, na baadhi ya biashara kupitia mipakani zimepungua hivyo kusababisha
kupungua kwa bidhaa kwenye nchi zinazotegemea bandari zetu, hii ni fursa kwetu
hivyo tuzalishe kwa wingi kwaajili ya nchi hizo ambazo zinatuzunguka na ambazo zinategemea bandari zetu” alisema
Prof. Shemdoe
|
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS),
Bw.Athuman Ngenya, akiendesha Mkutano wa Watalaam wa Mashirika ya Viwango
kutoka nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
uliofanyika kwa njia ya Video katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania.
|
|
Watalaam wa Shirika la Viwango kutoka Tanzania wakiwa
kwenye Mkutano wa Mashirika ya Viwango wa nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya
Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya Video katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania.
|
|
Watalaam wa Shirika la Viwango kutoka Tanzania wakiwa
kwenye Mkutano wa Mashirika ya Viwango wa nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya
Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya Video katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania.
|
|
Watalaam wa Shirika la Viwango kutoka Tanzania wakiwa
kwenye Mkutano wa Mashirika ya Viwango wa nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya
Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya Video katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania.
|
Aidha
Prof. Shemdoe alisema lengo kuu la Serikali ya Tanzania ni kuzalisha kwa wingi
Viwandani bidhaa zenye ubora na zenye
uwezo wa kushindana katika masoko ya nchi za za SADC na Kimataifa ili kuweza kufikia
malengo makuu ya kupambana kiuchumi hasa katika kipindi hiki ambacho maradhi ya
Corona yameenea katika nchi mbalimbali.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania Dkt. Yusuph Ngenya
amewataka wamiliki wa Viwanda na Wazalishaji wa bidhaa kuendelea kuzalisha
bidhaa zenye Ubora na Viwango ili waweze kushindana na kununuliwa kwa wingi na nchi
16 wanachama wa jumuiya ya SADC na Afrika Mashariki kwa ujumla.
|
Watalaam wa Shirika la Viwango kutoka Tanzania
wakifuatilia kwa makini Mkutano wa Mashirika ya Viwango wa nchi 16 za Jumuiya
ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya Video
katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam,
Tanzania. |
|
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.Athuman Ngenya (kushoto),
akizungumza kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda
na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe kufungua Mkutano wa Watalaam wa Mashirika ya Viwango kutoka nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo
ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya Video katika Kituo
cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania. |
|
Na
Erick Msuya – MAELEZO
“Niwaombe
wenye viwanda na watengezaji wa bidhaa ndani ya nchi wajitahidi kutengeza
bidhaa zenye viwango na ubora, sababu kiwango kikishapita hapa Tanzania, basi
soko lote la nchi 16 za SADC bidhaa itaweza kununuliwa, hivyo ni wakati sasa wa
soko kututambua ndani ya Afrika na Nje ya Afrika. Alisema Dkt. Ngenya
Shirika
la Viwango Tanzania TBS ni miongoni mwa mashirika ya viwango yanayotambulika na
kuheshimika kimataifa kwa weledi na utoaji wa viwango vya kimataifa hivyo
bidhaa za ndani zitakazothibitishwa na Shirika hilo zitakuwa na ubora na
viwango vya Kimataifa.
No comments:
Post a Comment