Na Mathias Canal, Wizara
ya Kilimo
Waziri wa Kilimo Mhe
Japhet Hasunga (Mb) ametoa taarifa ya uzalishaji wa zao la Korosho katika
kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais
Dkt John Pombe Magufuli ambapo amebainisha kuwa uzalishaji wa korosho umefikia
Tani 1,036,698
Waziri Hasunga amesema
kuwa kiasi hicho kimepelekea serikali kuingiza zaidi ya Trilioni 3.3 na fedha
za kigeni zaidi ya Dola Milioni 1139 za Marekani kwa kipindi cha miaka mitatu
(2017-2019) hivyo zao hilo kuongoza kwa uzalishaji kuliko mazao yote nchini.
Katika kutekeleza sera ya
Viwanda ya serikali ya awamu ya tano Waziri Hasunga amesema kuwa viwanda vya
kubangua korosho vimeongezeka kufikia 30 kutoka viwanda 21
Kadhalika katika taarifa
hiyo ameeleza kuwa uzalishaji wa korosho nchini umeongezeka kwani mpaka sasa
jumla ya mikoa 20 inazalisha korosho ukilinganisha na mikoa mitano pekee kabla
ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani.
Watanzania wengi
wamehamasika na kilimo hicho ambapo mikoa hiyo imeamua kujishughulisha na zao
hilo kutokana na umuhimu wake katika mapato ya wakulima na watanzania kwa
ujumla wake.
Kwa mujibu wa Waziri
Hasunga amesema kuwa Takribani watanzania wanaokadiriwa kuwa 1,200,000 mpaka
1,600,000 wameajiriwa katika zao hilo jambo ambalo limewanufaisha na kuweza
kujipatia kipato chao.
Hata hivyo amesema kuwa
Mafanikio hayo yametokana na namna ambavyo serikali imetoa elimu kwa kina
kuhusu namna bora ya kutumia viuatilifu, kuongeza uzalishaji na Tija, kadhalika
uwekezaji katika eneo la utafiti kupitia kituo cha Taasisi ya Utafiti wa kilimo
cha Korosho cha Naliendele kilichopo Mkoani Mtwara.
Amesema kuwa kituo hicho
kimefanya kazi kubwa na nzuri ya kuhakikisha kuwa wakulima wanapata miche bora
ya mikorosho, yenye uwezo wa kuongeza uzalishaji, zenye uwezo wa kustahimili
ukame, na zenye uwezo wa kukinzana na magonjwa mbalimbali hivyo kuwa kitovu cha
uzalishaji wa miche ya mikorosho nchini.
Waziri Hasunga amesema
kuwa katika kipindi hicho ubora wa korosho umeimrika hivyo kupelekea Korosho ya
Tanzania kupendwa na kuvutia wanunuzi wengi Duniani.
Kuhusu sekta ya Ushirika,
Waziri Hasunga amesema kuwa sekta hiyo imekuwa muhimu kwa watanzania kwani
manufaa ya zao la korosho yanatokana na
uwepo wa ushirika hivyo ushirika huo utaendelea kuimarishwa ili kuwa na
mafanikio makubwa zaidi katika sekta hiyo.
No comments:
Post a Comment