Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mussa Azzan Zungu ameiagiza Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani
kufanya uhakiki wa viwanda vyote vilivyopo wilayani hapa kubaini endapo
vinaendeshwa kihalali au la.
Zungu ametoa agizo hilo leo wilayani hapa alipofanya ziara
ya kukagua kiwanda cha Exel Chemical Ltd. kinachojishughulisha na kusaga mawe
kwa ajili ya kutengenezea rangi kufuatia malalamiko kutoka kwa wadau wa mazingira
pamoja kufanya zake shughuli kinyume cha taratibu.
Alisema kuwa Serikali inachunguza kubaini kiwanda hicho kinavyofanya
shughuli zake kama inalipa kulipa kodi au leseni na kama wakibaini hailipi kodi
hatua stahiki zitachukuliwa.
Katika ziara hiyo akiwa ameambatana na viongozi wa Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) uongozi wa Wilaya hiyo Zungu
alibaini jina la kiwanda ni Exel Chemical wakati bidhaa inayozalishwa ni
Watercraft jambo ambalo linakwenda kinyume cha sheria.
Aidha, waziri huyo alisisitiza kuwa nchi inataka wawekezaji
katika sekta ya viwanda wafanye kazi bila kubughudhiwa wala kuonewa na wala
Serikali haitafunga kiwanda lakini sharti lazima wafuate sheria za nchi
zikiwemo za mazingira.
“Viwanda hivi vinafanya kazi bila leseni na wakifanya hivi Serikali
inakosa mapato, na Serikali ikikosa mapato halmashauri mtakosa ‘on source’ za
kuendesha shughuli zenu sasa fanyeni auditing kubaini viwanda gani viko
kihalali na vipi vipo kiharamu ili sasa tuanze kuchukua hatua ili walipe leseni
kwa mafunfaa ya Taifa,” alisema Zungu.
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
Kwa upande wake Mkurugenzi wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka
alisema kuwa imebaini kiwanda hicho ambacho kipo karibu na makazi ya watu kinafanya
shughuli zake kinyume cha taratibu za mazingira.
Dkt. Gwamaka alibainisha kuwa kutokana na ukaguzi
uliofanyika imebainika kuwa kiwanda hicho kimekuwa kikichafua hewa kwa kutoa
vumbi na kuwa ni chanzo cha kelele jambo ambalo linatishia afya za wakazi wa
eneo hilo.
Hata hivyo bado uchunguzi kuhusu tuhuma mbalimbali
zilizotolewa dhidi ya kiwanda hicho unaendelea ili kubaini ukweli na kuchukua
hatua stahiki kwa mmiliki huyo.
Aidha Serikali kufuatia tuhuma hizo inaendelea kufanya
uchunguzi ili kubaini ni jina gani halisi la usajili wa kiwanda hicho pamoja na
mwenendo mzima wa ulipaji kodi.
No comments:
Post a Comment