Mganga mfawidhi wa
hospitali ya rufaa ya mkoani Iringa Dr Alfredy Mwakalebela akiwa anapita katikaFULL BODY MACHINE
Afisa Usalama, Afya, Mazingira na Ubora wa
kampuni ya Asas Cosmas Charles akiwa anapita katikaFULL BODY MACHINE
|
Afisa Usalama, Afya, Mazingira na Ubora wa
kampuni ya Asas Cosmas Charles akimkabidhi ndoo maalum kwa mganga mfawidhi wa
hospitali ya rufaa ya mkoani Iringa Dr Alfredy Mwakalebela
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Kampuni ya Asas ya mkoani Iringa imekabidhi msaada wa mashine ya
kutakasa mwili na vifaa vingine vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya
Corona katika hospitali ya rufaa ya Mkoani Iringa.
Akikabidhi msaada huo kwa mganga mkuu wa
hospitali ya rufaa mkoani Iringa, kwa niamba ya mkurugenzi
uzalishaji wa kampuni ya Asas ,Afisa Usalama, Afya, Mazingira na Ubora wa
kampuni ya Asas Cosmas Charles alisema kuwa lengo LA kutoa msaada huo ni
kuhakikisha wananchi wote wanaenda katika hospitali hiyo wanajikinga na
maambukizi ya virusi vya Corona ambavyo vimekuwa vinahatarisha maisha ya
binadamu kote duniani.
Alisema kuwa kampuni ya Asas
imekuwa ikiwakumbuka mara kwa mara wananchi katika njia tofauti ndio maana
baada ya kutokea kusambaa kwa virusi vya Corona Kampuni imekuwa ikijitoa
kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Iringa wanajikinga vilivyo.
Kampuni imekuwa inaendelea kutoa
elimu juu ya maambukizi ya virusi vya Corona katika sekta mbalimbali hapa mkoani
Iringa kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanaendelea kuwa salama.
Aidha Charles alivitaji vitu ambavyo
kampuni ya Asas imevitoa katika hospitali ya Rufaa ya Iringa ambavyo ni mashine
ya kutakasa mwili mzima,ndoo maalum 80 na barakoa 1200
Kwa upande mganga mfawidhi wa
hospitali ya rufaa ya mkoani Iringa Dr Alfredy Mwakalebela aliipongeza kampuni
ya Asas kwa msaada huo walioutoa kwa kuwa ni mkubwa kulingana na mahitaji ya
kujinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
Mwakalebela alisema mashine hiyo ya
kutakasa mwili mzima yawezekana nyanda za juu kusini ndio imekuwa ya kwanza
kupatikana katika hospitali za rufaa kutoka na uhitaji wake.
"Leo tumepokea mashine hii
ambayo ni bora na nzuri katika kuhakikisha tunapambana vilivyo na maambukizi ya
virusi vya Corona ambvyo vimekuwa vikishia uhai wa binadamu kote duniani"
alisema
Mwakalebela alisema kuwa licha ya
kutoa mashine hiyo lakini kampuni ya Asas imetoa pia ndoo maalum 80 kwa ajili
ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona pamoja barakoa 1200.
No comments:
Post a Comment