Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumza kuhusu malipo ya wakulima wa Kata ya Iglanson kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.
Wakulima
Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, wapongeza Serikali kwa kuelekeza
ununuzi wa mazao yao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.
Pongezi
hizo walizitoa mwishoni mwa wiki wakati wa ulipwaji wa fedha zao baada
ya kuuza choroko kwa njia ya stakabadhi ghalani katika Kata ya
Iglanson.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumza wakati wa utoaji wa malipo hayo alishukuru Serikali kwa kuwajali wakulima.
Afisa Ushirika wa Wilaya ya Ikungi, Gurisha Nsemo akizungumza na Wakulima wa Kata ya Iglanson wakati wa malipo hayo.
"
Kipekee nishukuru Serikali kwa kuelekeza matumizi ya mfumo huu wa
stakabadhi ghalani kwani umekuwa ni mkombozi kwa wakulima wetu." alisema
Mpogolo.
Alisema
katika wilaya hiyo wakulima zaidi ya 500 wamenufaika na mfumo huo
ambapo wameweza kupata zaidi ya sh.milioni 139 na kuokoa zaidi ya
sh.milioni 54 ambazo wangenyonywa wakulima.
Mpogolo
alisema changamoto kubwa iliyokuwepo ni walanguzi hao kujikita kwenye
maeneo ya vijiji na kuupinga mfumo huo kwa kuwa ulikuwa ukiwanufaisha
kwa miaka mingi.
Mkulima, Isack Shango, akimshukuru Rais Magufuli kwa niaba ya wenzake. |
Mkulima, Magreth Magamba, akizungumza. |
Wakulima wa Kata ya Iglanson wakisubiri kulipwa. |
Alisema
wachuuzi walikuwa wanatumia vipimo feki kwani utakuta katika kilo 50
zitazopimwa na mkulima utaona kilo tatu zilikuwa zikikatwa kiujanja na
walanguzi hao. Huku wachuuzi wakinunua kilo moja kati ya sh.400 hadi
600 lakini kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani waliweza kuuza kwa
sh.1075 kwa kilo kwenye mnada wa tarehe 14 mwezi Mei 2020.
Mpogolo
alitaja changamoto nyingine kuwa ni walanguzi hao kuwalaghai wakulima
kuwa vyama vya ushirika vilikiwa havina uwezo wa kuwalipa fedha zao siku
hiyo hiyo wakati sio agizo la mfumo.
Wakulima wa Kata ya Iglanson wakisubiri kulipwa. |
Meneja wa Benki ya NMB, Wilaya ya Ikungi, Osward Kayuni, akizungumzia umuhimu wa wakulima hao kufungua akaunti ili malipo yao yalipwe kwa njia ya simu.
Akimuongelea
mkulima Joyce Nzela ambaye alitoa malalamiko kwa Rais Magufuli wakati
alipo simama kwa muda na kuongea na wananchi wakati akiwa njiani
kuelekea Dodoma akitokea Chato, ambaye alilalamikia mfumo wa ununuzi wa
zao hilo alisema walipofuatilia hakuonekana katika orodha ya wakulima
waliopeleka choroko kwenye AMCOS ya Kijiji cha Mayaha kama alivyodai.
Hata hivyo kumbukumbu zilionyesha kwenye mkutano wa kutoa elimu ya mfumo
uliofanyika Mei Mosi 2020 Kijiji cha Mtavila kuwa Joyce, alikuwa
miongoni mwa wachuuzi walioupinga mfumo na kuwataka wakulima
wasiukubali.
"
Tulifuatilia tuligundua jina lake halikuwepo kwenye orodha ya wakulima
ambao walipaswa kulipwa lakini wenzake, Zuhura na Amina walikuwepo
kwenye orodha ya AMCOS ya Iglanson na malipo yao yalikuwepo." alisema
Mpogolo.
Choroko zikiwa kwenye mnada.
Mkulima,
Isack Shango, alimshukuru Rais Magufuli kwa niaba ya wenzake na kusema
walanguzi walikuwa wakiwanyonya kwa kutumia vyombo vikubwa huku bei
ikiwa ndogo.
Alisema
walanguzi hao walikuwa wakitumia ndoo maarufu kwa jina la Mozambiki
yenye ukubwa wa kuingiza kilo 25 ambayo ikiwa na malighafi walinunua kwa
sh.60,00 na bila malighafi walikuwa wakilipia sh.70,000
Mkulima, Francis Magesa (kushoto) akitafsiri lugha ya kisukuma wakati mama huyo (kulia) alipokuwa akimshukuru Rais Magufuli kwa kuwapelekea mfumo huo. |
Na Dotto Mwaibale, Singida
Wakulima wengine waliompongeza Rais Magufuli kwa kuwawezesha kulipwa fedha zao kupitia Benki ya NMB ni pamoja na Magreth Magamba, Emmanuel Ncheyi na Francis Magesa.
Meneja wa Benki ya NMB, Wilaya ya Ikungi, Osward Kayuni aliwataka wakulima hao kufungua akaunti katika benki hiyo ili malipo yao yaweze kufanyika kwa haraka kupitia simu zao badala ya utaratibu wa kuwapelekea fedha mkononi ambao sio salama.
Wakulima hao wameshukuru mfumo huo kwanza wanapata pesa zaidi kuliko mwanzo, pili kutumika kwa vipimo vya uhakika na tatu pia kuimarishwa kwa vyama vya ushirika ambapo wamemuomba Rais Magufuli mazao mengine ya mpunga na alizeti yaingizwe kwenye mfumo kwani wananyonywa sana kipindi hichi cha mavuno.
No comments:
Post a Comment