Serikali
kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imeanza
kutekeleza zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi ambao wanaguswa na mradi
wa uchakataji na usindikaji wa gesi asilia (LNG) Mkoani Lindi.
Mradi
huo ambao unagusa Mitaa mitatu ya Likong’o, Masasi ya Leo na Mto Mkavu
unachukua eneo lenye ukubwa wa hekta 2,071.7, ambapo Serikali imetoa
kiasi cha Shilingi Bilioni 5.2 kwa ajili ya kufidia wanachi 693 ambao
wanaguswa na mradi huo.
Eneo ambalo kiwanda cha LNG kinatarajiwa kujengwa katika kijiji cha Likong’o katika Manispaa ya Lindi
Akizungumzia
mradi huo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi alisema, “mchakato
wa kuwafidia waathirika wa mradi wa LNG umechukua muda mrefu sana na
nimekuwa nikijibu maswali mengi sana kutoka kwa wananchi hao.
Hatimaye
Serikali imeidhinisha kiasi cha Shilingi Bilioni 5.2 kufidia wananchi
wanaoguswa na mradi huu muhimu. Napenda kutumia fursa hii kuishukuru
Serikali pamoja na Shirika letu la TPDC kufikia hatua hii muhimu.”
Wananchi
watakaopisha mradi wa LNG eneo la Likong’o, Manispaa ya Lindi
wakifuatilia na kusmsikiliza kwa makini Afisa Maendeleo ya Jamii Ndugu
Oscar Mwakasege kutoka TPDC, alipokuwa akiwasilisha mada ya utatuzi wa
migogoro ya wananchi katika mradi huo
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi akitoa maelezo ya mradi wa LNG mbele ya Waandishi wa Habari Ofisini kwake.
Katika
hatua nyingine, Meneja mradi wa LNG kutoka TPDC, Mhandisi Fedister
Agrey aliwahakikishia wananchi na vyombo vya habari kwamba, “mradi upo
na ndiyo maana kikosi kazi kutoka TPDC, Benki ya NMB pamoja na Taasisi
zingine za Serikali wapo hapa.”
“Zoezi
hili linatekelezwa katika hatua mbili, hatua ya kwanza inahusisha
utoaji wa elimu ya fidia, matumizi sahihi ya fedha, sharia na utatuzi wa
migogoro kwa waathirika wote wa mradi.
Na
hatua ya pili itahusisha zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi husika”
alisisitiza Mhandisi Fedister. Wananchi watakaopisha mradi wa LNG eneo
la Likong’o, Manispaa ya Lindi wakifuatilia na kusmsikiliza kwa makini
Afisa Maendeleo ya Jamii Ndugu Oscar Mwakasege kutoka TPDC, alipokuwa
akiwasilisha mada ya utatuzi wa migogoro ya wananchi katika mradi huo.
Akiongea
kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Mtaa wa Masasi ya leo Bwana Saidi
Ismail Lihoka alisema, “Tunaipongeza Serikali na Shirika la TPDC kwa
kutimiza ahadi yao ya kulipa fidia wananchi watakaopisha mradi wa LNG.
Pia,
nitumie fursa hii kuwaasa wananchi wenzangu kwamba, wawe watulivu na
wafuate utaratibu uliopangwa na TPDC katika kufanikisha zoezi hili.”
Mhandisi wa Petroli Kutoka TPDC Ndugu Felix Nanguka akitoa mada ya
masuala ya fidia kwa waathirika wa mradi wa LNG katika Mtaa wa Likong’o,
Manispaa ya Lindi Mnamo Desemba, 2015 Serikali ilitwaa ardhi ya
iliyokuwa shamba la mkonge na kuipatia TPDC hati ya umiliki wa eneo hilo
kwa ajili ya kuendeleza mradi wa LNG.
Aidha,
uthamini wa ardhi ya mradi ulifanyika mwaka 2015 na kufanyiwa
marekebisho madogo mwezi Aprili 2017, ili kufidia eneo la ardhi ambalo
lilikuwa linamilikiwa na wananchi pamoja na maendelezo yaliyofanywa na
wananchi katika eneo ambalo limetwaaliwa na Serikali.
Mradi
huu ni mkubwa na wa aina yake kwa Tanzania, ambao Serikali inajipanga
vyema ili kuhakikisha maslahi mapana yanapatikana kwa Watanzania. Lengo
la mradi huu ni kuiwezesha Tanzania kuzalisha gesi nyingi
iliyogundulika baharini na kuuza rasilimali hii katika soko la Dunia,
pamoja na kuwezesha upatikanaji wa gesi ya kutosha katika soko la ndani
kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme na matumizi mbalimbali ya
viwandani na majumbani.
No comments:
Post a Comment