Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John Magufuli akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, kwa ajili ya kujadili na kupitisha majina ya wagombea wake wa ubunge katika Uchaguzi Mkuu ambao kampeni zake zinaanza mwishoni mwa mwezi huu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, wakipitia nyaraka tayari kwa kujadili na kupitisha wagombea ubunge wa chama hicho.
Ofisa wa CCM Makao Makuu, Debora Charles akigawa nyaraka kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wakati wa kikao cha kujadili na kupitisha majina ya wagombea ubunge kupitia chama hicho.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole (kulia), akitoa hamasa kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Magufuli kuingia ukumbini kuongoza kikao hicho.
Wajumbe wakifurahia jambo wakati wa kikao hicho
Mwenyekiti wa CCM, Dk. Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ali wakionesha dole ambayo ni alama ya chama hicho kuonesha mambo yanakwenda sawa. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Dk. Ali Mohamed Shein.
Ni furaha ilioje kwa mjumbe huyu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM baada ya kufurahishwa na Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni mgombea urais kupitia chama hicho, Dk. John Magufuli akiwashukuru kwa kumpigia kura nyingi na kumtafutia wadhamini katika mikoa yao.
Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ali akitoa maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Chama, Rais Dk. Magufuli kufungua kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM, Rais John Mwagufuli akiwashukuru wajumbe kwa kumpigia kura na kumtafutia wadhamini waliomuwezesha kushinda kwa kishindo kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho.
Wajumbe wakifurahi baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kuwashukuru kwa kumpigia kura na kumtafutia wadhamini.
Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akiongoza kikao baada ya kutoa maneno ya ufunguzi. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Visiwani), Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Bashiru Ali.
No comments:
Post a Comment