Meneja wa Shirika la World Vison kanda ya Kati, Faraja Kulanga akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye sherehe za kufunga mradi wa Kisiriri-ADP.
Shirika
la World Vision Tanzania kupitia wafadhili kutoka Uingereza limetumia
zaidi ya shilingi bilioni 8.4 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za
mradi wa kuboresha sekta za Elimu, Afya, Maji, Usafi wa mazingira na
kuongeza uchumi wa kaya pamoja na usalama na ulinzi wa mtoto katika kata
tano za Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Akitoa
taarifa ya kufunga mradi ADP–Kisiriri ulioanza mwaka 2003, Meneja wa
Shirika hilo Kanda ya Kati, Faraja Kulanga, amesema pamoja na
kumalizika kwa ufadhili wa shughuli katika kata za Kidaru, Tulya,
Kisiriri, New Kiomboi na Old Kiomboi lakini bado wanatafuta miradi
mingine, Katika kipindi cha miaka 17 ya utekelezaji wa shughuli
mbalimbali, Mradi huo wa Kisiriri-ADP umeweza kuwafikia na kubadilisha
maisha watu zaidi ya 37,000 wakiwemo watoto 4,800.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia wananchi.
“Naishukuru
Serikali ya Tanzania kwa kukubali sisi pamoja na wafadhili wetu wa
Uingereza kuwa ni sehemu ya kuchochea maendelo kwa wananchi wetu hapa
nchini natumaini kwa miaka hii 17 tuliyokaa tumefanya kazi kwa weledi
mkubwa ndio maana tumeleta mabadiliko makubwa kwenye sekta zote
tumezigusa kwa karibu sana, mimi nawatakia kila la kheri wananchi wa
kisiriri na kata zote tulipokuwa tukitekeleza mradi huu, tutarudi tena
kwa miradi mingine” alisema Kulanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wananchi wa Kisiriri
kutosikitika kutokana na Shirika la World Vision kuondoka kwa kuwa
tayari limewajengea uwezo wa kutegemea kupitia Serikali hii ya awamu ya
tano tunawashukuru sana kwakua nanyi kwenye kusukuma maendeleo ya wana
Singida na watanzania pia.
Mkuu wa Mkoa Dkt Rehema Nchimbi akitembelea mabanda ya Wanufaika wa mradi wa Kisiriri-ADP.
“Hatupaswi
kunungunika kutosikitika kikubwa hapa tunatakiwa kuwashukuru sana World
Vision kwa miaka yote 17 kuwa na sisi inatubidi kuvitunza, kuvilinda na
kuvithamini hasa kwa umakini mkubwa sana na kutumia maarifa tuliyo
achiwa na wadau wetu wa maendeleo kuviendeleza zaidi maana kama maarifa
wametuachia yakutosha ”.alisema Nchimbi.
Baadhi
ya wananchi walionufaika na mradi huo wanakiri kuleta mabadilko makubwa
katika maeneo yao hasa kwenye Elimu Afya Mazingira na Maji na kwa
watoto wetu pia tunawashukuru kwa kujitowa kwa ajili yetu na sisi
tunaahidi kuyaendeleza yote yaliyo mema na kutumia ujuzi mlio upandikiza
kwetu kwa muda wote wa miaka 17 .
Wanufaika wa mradi kwenye upande wa elimu wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi, uoni hafifu na ulemavu wa viungo wakiwa wanafuatilia hotuba ya mgeni rasmi kwenye
sherehe hizo.
Wa kwanza kulia ni Afisa Habari wa World Vision kutoka Makao Makuu, Agness Mwafifi, akiwa na Afisa Habari wa Mkoa wa Singida, John Mapepele wakiwajibika.
Wanufaika kwa upande wa kilimo wa mradi wa Kisiriri-ADP wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye baadhi ya mabanda yalipo kwenye sherehe za mabidhiano ya mradi.
Sherehe ikiendelea.
Na Ismail Luhamba, Singida
Katika miaka 17 hiyo mradi umeweza kuchimba visima (5) na visima vifupi (10) katika vijiji vyote vya eneo la mradi, kwa kushirikiana na Halmashuri ya Wilaya ya Iramba wamefanikiwa kusambaza mifumo ya maji katika Kijiji cha Meli na Hospitali ya Wilaya ya Iramba.
Kwenye upande wa elimu mradi umefanikiwa kujenga madarasa (19) katika shule ya msingi Ndurumo 7, Migilango 3, Doromoni 1, Kisiriri 4, Mampanta 2 na Kinambeu 2.Tumeweza kujenga nyumba 8 za walimu katika shule za msingi Ndurumo 2, Dolomoni 1, Kisiriri 2, Migilango 1, Mampanta 1, Kinambeu 1 na ofisi 2 za walimu zilijengwa, hayo ni baadhi tu mafanikio ya Kisiriri-ADP.
No comments:
Post a Comment