Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Patrobas
Katambi amezindua Baraza la Wafanyakazi Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na
kutoa wito kwa wafanyakazi kuchapa kazi kwa bidii kwani ndio nguzo kuu katika
mafanikio ya Mfuko.
Mhe.
Katambi ameyasema hayo mjini Morogoro Februari 10, 2021 wakati akizindua
baraza la Wafanyakazi WCF kwenye ukumbi wa Magadu.
“Lazima
tujue uwajibikaji ni nguzo kuu ya mafanikio katika sehemu yoyote ya kazi, hivyo
wajumbe mnaowawakilisha wafanyakazi wa Mfuko mnapaswa kuwahimiza wenzenu kuhusu
swala hilo.” Alifafanua Mhe. Katambi.
Alisema
Serikali inatambua mchango wa wafanyakazi wote nchini lakini vile vile inatambua
sana na kuheshimu mchango wa Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi katika kukuza uchumi wa nchi yetu kwa kuhakikisha kuwa nguvu
kazi ya wafanyakazi wanaougua au kuumia kutokana na kazi haipotei kwa wakati
wote kupitia huduma ya matibabu inayotolewa kwa waathirika.
“Napenda
niwahakikishie kuwa Serikali ya awamu ya tano inaendelea kushirikiana na Mfuko
katika kuhakikisha unanufaisha watu walio wengi na kufanikisha malengo ya
kuanzishwa kwake.”
Naibu
Waziri Katambi pia aliupongeza Mfuko huo kwakuwa na wafanyakazi wachache lakini
waliouwezesha Mfuko kupiga hatua kubwa katika utekelzaji wa majukumu yake.
“Mnatupa
heshima kubwa sana Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri mama Jenista Mhagama, tangu mmeanza kutekeleza majukumu haya mmeanzia ziro baada ya mwaka mmoja
mkalipa shilingi bilioni 1.5 na bado mnaendelea kufanya vizuri kwakweli habari hizi zilifurahisha na hata kamati ya bunge ilishukuru na kuwapongeza hongereni sana
sana.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Katambi.
Alisema hata baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge wametoa ushuhuda jinsi Mfuko huo umekuwa ukihudumia vema katika suala la fidia na HUDUMA za utengamao (rehabilitation aervices).
Awali
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba alisema
katika kipindi cha miaka sita ya uhai wa Mfuko kumekuwepo na mafanikio kadhaa
chini ya nguvu kazi ya wafanyakazi 129 ambao wameweza kutekelza vema majukumu yao
“Sambamba
na hilo tumekuwa tukiwapatia mafunzo ya mara kwa mara ili kuongeza weledi
katika utendaji wa kazi.” Alifafanua Bw. Mshomba.
Bw.
Mashomba pia alisema miongoni mwa maeneo ambayo Mfuko umeboresha sana HUDUMA zake ni kuweka
mfumo wa utoaji taarifa kwa njia ya mtandao.
“Huduma
zetu hivi sasa zinatolewa kwa kiasi kikubwa sana kwa njia ya mtandao karibu
asilimia 85 ya shughuli zetu, kujisajili, kuwasilisha michango, uchatakati wa
malipo lakini pia muhimu zaidi ni kutoa taarifa pale mfanyakazi anapougua au
kupata ajali ya kikazi na hata inapotokea bahati mbaya akafariki kutokana na
kazi tumeweka mfumo mzuri unaowezesha taarifa hizo kutufikia kwa haraka
kupitia mtandao.” Alifafanua Bw. Mshomba.
Alisema
Mfuko unatambua kuwa nchi ni kubwa na sio sehemu zote mtandao unapatikana kwa
urahisi hivyo Mfuko umefungua ofisi za kikanda, kuna ofisi Makao makuu ya Serikali
Dodoma, Mbeya, Arusha, Morogoro, Mtwara na mwisho wa mwaka huu wa fedha Mfuko
utafungua ofisi kwenye mikoa ya Tabora, Geita na Shinyanga hususan maeneo ya
migodi kama Kahama.
“Ukiacha
hayo Mfuko wetu kifedha tumejenga uwezo wa kutosha kwa mujibu wa hesabu
zilizokaguliwa na CAG tarehe 30/06/2020 tulikuwa na ukubwa wa thamani (Assets)
wa Bilioni 333, lakini pia hesabu ambazo hazijakaguliwa na CAG hadi Desemba
2020 tumefikia bilioni 389.” Alifafanua Mkurugenzi Mkuu Mshomba.
Lakini
pia Mfuko umeboresha sana huduma za tathmini kwa kutoa mafunzo kwa madaktari
wapatao 1,085 ambao ndio wanaofanya kazi ya kutathmini pale mfanyakazi anapougua au kuumia kutokana na kazi.
Naye
Katibu Mkuu wa chama cha Wafanyakazi wa
Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Heri Mkunda alisema Mafanikio yaliyopatikana
WCF ni kutokana na wafanyakazi kufanya kazi kwa kujituma kushauri vizuri
uongozi na kushirikishwa katika masuala mbalimbali yanayohusu taaisi.
“Niipongeze
Menejimenti na kuwaomba waajiri wengine kujifunza kutoka WCF, hawa wafanyakazi
ndio walio jikoni wanaweza kushauri vizuri kuhusu masuala mbalimbali inayohusu
taasisi ili kufikia malengo.”
Awali kabla ya uzinduzi wa baraza hilo, wajumbe walifanya uchaguzi wa kuchagua Katibu wa Baraza na Katibu Msaidizi, ambapo Bw.Mbarikiwa Masinga alichaguliwa kuwa Katibu wa Baraza na Bi.Irine Mngure alichaguliwa kama Katibu Msaidizi.
No comments:
Post a Comment