Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa mh. Queen
Sendiga ameigaiza Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa kuwasilisha
ofisini kwake majina ya wafanyabishara walioshindwa kulipa madeni yao baada ya
makubaliano ya kisheria baina ya wafanyabiashara na mamlaka hiyo.
akizungumza kwenye kikao na
wawakilisha wafanyabiashara na machinga wa mkoa wa Iringa alisema kuwa hata
wafumbia macho wafanyabishara wote ambao tayari wamepewa maagizo ya kisheria
kulipa madeni hayo lakini bado wamekuwa wanakaidi agizo hilo kutoka kwa mamlaka
husika.
Akiwa katika kikao hicho mkuu wa mkoa
wa Iringa alimuagiza meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa
kuhakikisha anapeleka majina na kukutana
na wafanyabiashara hao wanaokimbia kulipa madeni yao licha ya serikali kuagiza
kulipa madeni hayo.
Mh: Sendiga alisema kuwa wadaiwa hao wakilipa
kodi inachangia katika kuboresha sekta mbalimbali kama miundombinu, Afya, elimu,
utalii, Ardhi, na kilimo katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya nchi.
Alisema kuwa akaunti za wafanyabisha
wakubwa ambao wanaodaiwa madeni makubwa zilikuwa zimefungwa hapo awali na
kufunguliwa kwa mjibu wa sheria na makubaliano na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
mkoa wa Iringa kulipa madeni hayo ili waendelee na biashara kama iliyokuwa
awali.
Mh:Sendiga alisema kuwa jukumu la
kulipa kodi ni kwa kila mwananchi anaishi nchini kwa lengo la kuchangia juhudi
ya serikali kukuza uchumi wa wananchi na kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla
hivyo wananchi wa mkoa wa Iringa wanatakiwa kulipa kodi kwa wakati ili kuepuka
kuwa na madeni makubwa hapo baadae.
“Ngoja niwaambie kuwa bila kulipa
kodi nchi haiwezi kukuza uchimi wake wala haitaweza kuleta maendeleo kwa
wananchi kwa wakati kwa kuwa itakuwa inakosa fedha za kuanzisha miradi mikubwa
ambayo inafaida kwa serikali” alisema Mh: Sendiga
Mh: Sendiga alimalizia kwa kuitaka
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa kuhakikisha inatoa elimu ya
mlipa kodi mara kwa mara ili kuepusha wafanyabiasha kufunga biashara zao au
kushindwa kulipa madeni ya kodi wanayokuwa wanadaiwa.
Akipokea maagizo hayo meneja wa Mamlaka
ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa Lamson Tulyanje alisema kuwa
wameyapokea maagizo hayo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Iringa na watayafanyia kazi
ili kuwawezesha wafanyabishara hao kufanya biashara kwa uhuru na kukuza mitaji
yao.
Tulyanje aliongeza kuwa
watahakikisha wanaendelea kutoa elimu ya mlipa kodi mara kwa mara ili kuwakumbusha
wafanyabishara kulipa kodi kuwa ni wajibu wao wa msingi kwa maendeleo ya nchini
yao.
Tulyanje alisisitiza kuwa
wananchi kudai risiti pale wanaponunua bidhaa yoyote kwa wafanyabishara hivyo
hivyo kwa wafanyabiashara nao wanatakiwa kutoa risiti kwa wateja wao wanaonunua
bidhaa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo mkoa wa Iringa Edmund Mkwawa
aliwamuomba mkuu wa mkoa wa Iringa kuhakikisha anatatua changamoto za
wafanyabiashara ili kukuza mitaji yao.
Alisema kuwa Iringa kunafursa
nyingi za kibiashara ambazo zinaweza kukuza uchumi wa mkoa kwa haraka endapo
changamoto walizozitoa zitafanyiwa kazi kwa kiwango kinachostahili.
Nao baadhi ya wawakilishi wa wafanyabiashara
mkoa wa Iringa wamtaka mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga kuacha kusikiliza
majungu ya baadhi ya wafanyabisha bali anatakiwa kujikita kutatua changamoto
walizomueleza kwa lengo la kukuza uchumi wa mkoa huo.
No comments:
Post a Comment