Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle
akimuonyesha kitu Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Khalid Songoro
kulia wakati wakikagua moja ya milango ya kivuko cha MV. MAFANIKIO
kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Songoro Marine katika yadi yake
iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kivuko hicho kinachotoa huduma
kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara kinatarajiwa kurejea Mtwara
baada ya wiki tatu kuendelea kutoa huduma. Katikati ni Mkuu wa Kivuko
Magogoni Kigamboni Mhandisi Samuel Chibwana
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle
(wa tatu kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro
Marine Khalid Songoro (wa tatu kulia) wakati akikagua maendeleo ya
kivuko cha MV. MAFANIKIO ambacho kimeletwa katika yadi ya Songoro
Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati. Kivuko
hicho kinachotoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara
kinatarajiwa kurejea Mtwara baada ya wiki tatu kuendelea kutoa huduma.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle
(wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Khalid
Songoro (wa pili kulia) na Mkuu wa Kivuko Magogoni Kigamboni Mhandisi
Samuel Chibwana kulia wakikagua kivuko cha MV. MAFANIKIO kinachofanyiwa
ukarabati na Kampuni ya Songoro Marine katika yadi yake iliyopo
Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kivuko hicho kinachotoa huduma kati ya
Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara kinatarajiwa kurejea Mtwara baada ya
wiki tatu kuendelea kutoa huduma.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Songoro Marine Khalid Songoro akimuonyesha kitu Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle
wakati akikagua kivuko cha MV. MAFANIKIO kinachofanyiwa ukarabati na
Kampuni ya Songoro Marine katika yadi yake iliyopo Kigamboni jijini Dar
es Salaam. Kivuko hicho kinachotoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo
Mkoani Mtwara kinatarajiwa kurejea Mtwara baada ya wiki tatu kuendelea
kutoa huduma. Kulia ni Mkuu wa Kivuko Magogoni Kigamboni Mhandisi Samuel
Chibwana
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA DAR ES SALAAM)
*****************************
Huduma
za Kivuko kwa wakazi wa Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara zinatarajiwa
kurejea baaada ya takribani wiki tatu kutoka sasa, hayo yamebainishwa na
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y.
Maselle leo wakati alipotembelea eneo la Yadi ya Songoro Marine
Kigamboni jijini Dar es Salaam kukagua maendeleo ya ukarabati huo
unaofanywa na kampuni ya Songoro.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kukagua ukarabati wa
kivuko hicho, Mtendaji Mkuu Maselle amesema kivuko hicho kipo mbioni
kukamilika kwani Mkandarasi ametakiwa kukamilisha kazi hiyo ndani ya
muda mfupi ili wakazi wanaotegemea kivuko hicho Mkoani Mtwara waweze
kurejeshewa huduma zake mapema iwezekanavyo.
‘’Tumekisafirisha
kivuko hiki kutoka Mtwara kuja hapa Dar es salaam kwakuwa ni gharama
ndogo kukileta hapa kuliko kusafirisha vifaaa vyote vya matengenezo
kwenda kufanyia Mtwara ndio maana mkandarasi akaamua kukivuta kivuko
hiki kije hapa ili muda wa matengenezo uwe mfupi zaidi’’.
Mhandisi
Maselle amesisitiza kuwa utaratibu wa kufanya matengenezo kwa vivuko
vya TEMESA ni muhimu sana kwa vyombo vya maji kwakuwa maji ya bahari
yana chumvi nyingi na kali hivo kama kivuko kitakuwa hakijafanyiwa
ukarabati kwa muda mrefu kitakuwa kinaharibika na kitashindwa kufanya
kazi kwani chuma chake kitaliwa na maji ya chumvi na hivyo kushindwa
kudumu kwa muda mrefu.
‘’Ni
utaratibu wa kawaida kwa TEMESA kila ambapo kivuko kinafikia muda wake
wa matengenezo kinga, lazima kitolewe na kupelekwa kufanyiwa ukarabati
na matengenezo na hii ni hatua mojawapo ambayo tumefanya na tunaendelea
na ukarabati wa vivuko vingine ambavyo muda wake wa ukarabati
umefika’’. Alisema Mhandisi Maselle ambapo amewaomba wakazi wa Mtwara
wavumilie wakati kivuko hicho kikiendelea kufanyiwa ukarabati ambapo
wakazi hao wamepelekewa boti mbili za MV. TANGAZO na MV. KUCHELE ambazo
zinatoa huduma kwa sasa kwa wakazi hao.
Naye
Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Khalid Songoro akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya tukio hilo la ukaguzi amesema,
ukarabati wa kivuko hicho umefikia asilimia 85% na ameongeza kuwa
wanatarajiwa kumaliza ukarabati wake ifikapo Tarehe 15 mwezi Agosti.
‘’Kazi kubwa zote tulizozifanya ziko kwenye hatua ya mwisho ili kuweza kukamilisha ukarabati wa kivuko hicho,’’ amesema Songoro.
Kivuko
cha MV. MAFANIKIO kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na
tani 50 na kinatoa huduma zake kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara
mjini.