Mbunge
wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akiwa ameongozana na
Kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Dodoma Mjini, jana amefanya mkutano wa
kuwashukuru wananchi kwa kuichagua CCM 2020 sambamba na kusikiliza
kero,changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Baada ya kusikiliza Changamoto za wananchi wa eneo husika,Mbunge Mavunde alieleza haya yafuatayo;
-Katika
kutatua changamoto ya maji mtaa wa Chididimo,tumeshapata fedha za
uchimbaji wa kisima kipya cha maji, kazi ambayo itaanza mapema mwezi
Agosti.
Kusambaza umeme maeneo yote ya mitaa iliyosalia katika kata ya Zuzu hasa mitaa ya Chididimo na Sokoine.
Kufuatilia
malipo ya fidia ya barabara ya mzunguko(Outer Ring Road) kwa wananchi
ambao bado hawajahakikiwa na kuingizwa kwenye malipo.
Kufuatilia
kwa ukaribu malipo ya fidia kwa wananchi wanaopisha maeneo yao kwa
ajili ya uwekezaji,mashamba darasa na hifadhi ya wanyama(Zoo).
Kusimamia uwasilishwaji mapema wa fedha Tsh 20,000,000 za ujenzi wa miundombinu ya vyoo Shule ya Msingi Chididimo
Ujenzi
wa Sekondari Mpya kata ya Zuzu kwa nguvu za Mbunge na wananchi
kuwapunguzia mwendo watoto wa shule kutembea umbali mrefu.
Kurasimisha vikundi vya wavuvi na kuviwezesha mikopo vikundi vya wakina Mama,Vijana na watu wenye ulemavu.
Kutoa magodoro 30 kwa ajili ya Hostel ya Wanafunzi wa Sekondari wanaotoka maeneo ya mbali.
No comments:
Post a Comment