Matokeo chanyA+ online




Friday, October 8, 2021

BASHE AITAKA TAASISI YA UTAFITI WA VIUATILIFU (TPRI) KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA KILIMO KUTEKETEZA MAGUGU YANAYOHARIBU ARDHI YA KILIMO NA UFUGAJI

 

Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) nje kidogo ya jiji la Arusha wakati alipotembelea Taasisi hiyo ili  kuona shughuli mbalimbali za kiutafiti zinazofanywa na taasisi hiyo jana , Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa (TPRI). Dkt. Efrem Njau

Waziri Bashe ameitaka Taasisi hiyo kuhakikisha inashirikiana na Wizara ya Kilimo  pamoja na wadau wengine ili kuteketeza magugu ambayo yamekuwa yakisambaa karibu nchi nzima yanayosababisha uharibifu wa ardhi ya kilimo na ufugaji.

Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akisisitiza jambo wakati akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) nje kidogo ya jijini Arusha wakati alipotembelea Taasisi hiyo ili kuona shughuli mbalimbali za kiutafiti zinafanyika katika taasisi hiyo.

Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akimsikiliza Dkt. Efrem Njau Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) alipokuwa akiwasilisha taarifa ya taasisi hiyo nje kidogo ya jijini Arusha wakati alipotembelea maabara za Taasisi hiyo ili kuona shughuli mbalimbali za kiutafiti zinafanyika katika taasisi hiyo.

Afisa  Mtendaji Mkuu wa TAHA Bi. Jaquiline Mkindi akielezea gharama ambazo wakulima wa mashamba makubwa ya Maua na mbogamboga pamoja na matunda wanagharamia ili kufanyiwa tafiti za ardhi, maji na anga kwa kutumia  wataalam kutoka nje ya nchi.

Kikao kikiendelea katika ya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe na Menejimenti ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) 

Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akiongozana  na viongozi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) nje kidogo ya jijini Arusha wakati akikagua maabara za taasisi hiyo ili  kuona shughuli mbalimbali za kiutafiti zinafanyika katika taasisi hiyo jana.

Afisa  Mtendaji Mkuu wa TAHA Bi. Jaquiline Mkindi akiongozana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Kilimo Bw. Hudson Kamoga pamoja na baadhi ya wakuu wa vitengo vya  Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) wakati Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe  alipotembelea taasisi hiyo jana.

Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akimsikiliza Baraka Sendeka Mchambuzi wa Viatilifu katika maabara za  Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) nje kidogo ya jijini Arusha alipokuwa akitoa maelezo kuhusu moja ya mashine zinazotumika kufanya utafiti wakati alipotembelea Taasisi hiyo ili  kuona shughuli mbalimbali za kiutafiti zinavyofanyika , Kushoto ni Dkt. Efrem Njau Kaimu Mkurugenzi wa (TPRI).

Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akimsikiliza Dkt. Efrem Njau Kaimu Mkurugenzi wa (TPRI) wakati akitembelea katika maabara za  Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) nje kidogo ya jijini Arusha alipokuwa akitoa maelezo kuhusu moja ya mashine zinazotumika kufanya utafiti wakati alipotembelea Taasisi hiyo kulia ni Jaquiline Mkindi Aisa Mtendaji Mkuu wa TAHA.

Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akimsikiliza Venace Kasenene Mchambuzi wa Viuatilifu katika maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) nje kidogo ya jijini Arusha wakati alipotembelea Taasisi hiyo ili kuona shughuli mbalimbali za kiutafiti zinafanyika katika taasisi hiyo.

Moja ya majengo ya taasisi hiyo.

Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akisisitiza jambo wakati akizungumza alipokuwa akitembelea maabara za Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) nje kidogo ya jijini Arusha wakati alipotembelea Taasisi hiyo ili kuona shughuli mbalimbali za kiutafiti zinavyofanyika katika taasisi hiyo kutoka kushoto ni Dkt. Efrem Njau Kaimu Mkurugenzi wa (TPRI), Ndeninsia Meena Mchambuzi wa Viuatilifu katika maabara na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TAHA Jaquiline Mkindi.

Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akimsikiliza Bw. Tano Hangali Mkuu wa Kitengo cha Utunzaji wa Viuatilifu na Mazingira TPRI wakati akielezea namna ya kutuza   viuatilifu na mazingira katika njia bora.

Muonekano wa moja ya maabara za taasisi hiyo

Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akizungumza na wafanyakazi wa taasisi hiyo mara baada ya kufanya ukaguzi katika maabara kulia ni Profesa Elinangaya Kweka Mkurugenzi wa Utafiti (TPRI).

Picha mbalimbalizikionesha baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika kikao hicho wakimsikiliza Mhe.Naibu Waziri Hussein Bashe hayupo pichani

NGO'S SINGIDA ZATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA SHERIA ZA NCHI


Msajili Msaidizi wa mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO'S) mkoani Singida Tumaini Christopher akizungumza jana wakati akifungua mafunzo ya siku moja  ya kuyajengea uwezo mashirika hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Msajili Mkuu na Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA) kwa ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society  (FCS).
Afisa Programu Mwandamizi kutoka FCS Makao Makuu Dodoma Nicholaus Mhozya, akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Mwezeshaji Wakili wa Serikali kutoka ofisi ya msajili,  Dennis Bashaka akitoa mada kwenye mafunzo hayo

Mjumbe wa Taifa wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Singida Peter Lissu akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Shirika la Iguguno Development Foundation (IDEFO) Vicky Mwaisakila (kushoto) akiandika wakati wa mafunzo hayo. 
    Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania For Equal Opportunity (TAFEO) Stellah Mwagowa          akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
  Mkurugenzi wa  Shirika la Youth Extended Foundation  (YOEFO)  Martha Nahson  akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Kawawa Munjori, akizungumza kwenye mafunzo hayo
Mafunzo yakiendelea.


Mkurugenzt wa Utu Wangu Organaition, Fatuma Mgeni akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
 Mwezeshaji kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Singida Yusufu Msangi akitoa mada kwenye mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Singida Development Association (SIDAS) akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki wa mafunzo hayo Hassan Rasul kutoka Mtinko Education Development Organization, akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki wa mafunzo hayo Adam Mayo kutoka Manyoni Development Foundation (MADEFO) akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika  la Jiokoe na Umaskini yaani Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF) nchini, Dkt.Suleiman Muttani, akizungumza kwenye mkutano huo.

Picha ya pamoja.



Na Dotto Mwaibale, Singida


Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO'S) mkoani Singida yametakiwa kufanya shughuli zao kwa kufuata kanuni na sheria zilizowekwa na Serikali na si vinginevyo.

Hayo yamesemwa jana na Msajili Msaidizi wa mashirika hayo Mkoa wa Singida Tumaini Christopher wakati akifungua mafunzo ya siku moja  ya kuyajengea uwezo mashirika hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Msajili Mkuu na Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA) kwa ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society  (FCS).

" Mashirika yasiyo ya kiserikali yanawajibu wa kufanya kazi zao kwa kufuata sheria kanuni na sheria za nchi jambo litakalosaidia kuwa tumikia wananchi bila ya bugugha,". alisema.

Mratibu wa mashirika hayo mkoani hapa Patrick Kasango akizungumza kwa niaba ya Serikali alisema Serikali ya mkoa  itaendelea kushirikiana na mashirika hayo.

Kasango alitumia nafasi hiyo kuwaomba wawakilishi wa mashirika hayo kwenda kupata Chanjo ya Uviko 19 pamoja na kuihamasisha jamii juu ya umuhimu wakupata chanjo hiyo ambayo Serikali imetumia fedha nyingi kuiagiza kwa  kupitia Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. 

Akitoa mafunzo hayo  Mwezeshaji Wakili wa Serikali kutoka ofisi ya msajili,  Dennis Bashaka alisema Sheria inayataka mashirika yasiokuwa ya kiserikali kuhakikisha yanafuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu yao sambamba na taarifa ya mapato na matumizi.

Alisema sheria imeeleza wazi kuwa shirika lisipofanya hivyo kuanzia miaka miwili  litafungwa licha ya Serikali kutambua umuhimu wa mashirika hayo kwani kinachohitajika ni kufuatwa kwa taratibu.

 Mwezeshaji kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Singida Yusufu Msangi aliyaomba mashirika hayo kuzingatia maelekezo yote ya TRA kuhusu ulipaji wa kodi kwa wakati ili kuepuka faini zisizokuwa za lazima.

Afisa Programu Mwandamizi kutoka FCS Makao Makuu Dodoma Nicholaus Mhozya alisema mafunzo hayo yalilenga kuzijengea uwezo taasisi hizo ili kukumbushana masuala muhimu hasa sheria ambazo zinayaongoza mashirika hayo kufanya kazi.

Alisema katika mafunzo hayo walikuwa na mada kuu mbili moja ilijikita kuongelea sheria ya Ngo's ya mwaka 2002 pamoja na marekebisho yake na uratibu wa masuala mbalimbali ya kazi za mashirika hayo.

" Mada ya pili ilikuwa ni kuhusu masuala ya ulipaji kodi ambazo zinazihusu asasi za kiraia ambayo iliwasilishwa na mwakilishi kutoka TRA," alisema Mhozya.

Mshiriki wa mafunzo hayo Martha Nahson kutoka Shirika la Youth Standard Foundation  (YSF) aliiomba Serikali ifanyie kazi upande wa kodi zinazotolewa na Serikali kwa kuangalia mashirika madogo na makubwa kuwa na sheria zake ili hayo madogo yakifikia hatua ya kukua yahamie huko ili kuyapunguzia mzigo wa ulipaji wa kodi kutokana ya uwezo wao wa fedha za.kujiendesha kuwa mdogo ukilinganisha na hayo makubwa.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania For Equal Opportunity (TAFEO) Stellah Mwagowa  alisema mafunzo hayo yamewapanua mawazo na kuona jinsi Serikali ilivyojitahidi katika eneo zima la usajili wa taasisi hizo ambao unafanyika kimtandao na kuokoa muda na masuala mazima ya kuendesha miradi na kuzifanya taasisi hizo kuwa endelevu.

"Kuna mambo ambayo bila ya elimu ilikuwa ikionekana kwamba kuziendesha taasisi hizo ni mambo magumu wakati tukijua nchi yetu inazihitaji taasisi hizi kufanya kazi na Serikali katika kuihudumia jamii ukizingatia kuwa zimekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo na masuala mazima ya kupambana na umasikini,". alisema Mwagowa. 

DKT.GWAJIMA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA USWISI NCHINI TANZANIA

 

Na.WAMJW- DSM

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo amekutana na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot ambapo wamekubaliana kuimarisha mahusiano na mashirikiano kati ya Tanzania na Uswisi.

Dkt. Gwajima amemhakikishia Balozi huyo kuendelea kusaidiana na Serikali ya Uswisi na katika mazungumzo yao wote wawili wamekubaliana  kufadhili uimarishaji mfuko wa afya ya pamoja (HBF), mifumo ya afya pamoja na huduma zote za mtandao katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Naye, Balozi Mhe. Didier Chassot amesema Uswisi iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya afya hususani katika swala zima la kuimarisha mifumo ya vituo vya afya na huduma za mtandao.

Viongozi hao wamekutaka na kufanya mazungumzo hayo kwenye ofisi ndogo za Wizara mkoani Dar es Salaam, ambapo kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe OR- TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe na Wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.









Tuesday, October 5, 2021

NEEMA YA MAJI YAWASHUKIA WANANCHI LUDEWA/KULETEWA BILIONI MOJA


 Na Damian Kunambi, Njombe


Kufuatia kuwepo kwa changamoto nyingi za maji katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imepelekea wizara ya maji hapa nchini kuahidi kutoa kiasi cha shilingi bilioni moja ndani ya mwezi huu ili kupunguza changamoto hizo.


Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa maji Merryprisca Mahundi baada ya kufanya ziara katika kata ya Masasi na Iwela na kusikiliza changamoto zao pamoja na kukagua mradi wa maji wa Iwela.


 Kabla ya Naibu Waziri huyo kutoa ahadi hiyo mbunge wa jimbo la ludewa Joseph Kamonga alielezea changamoto wanazozipata wananchi hao na kusema kuwa wananchi wake wamekuwa wakitembea umbali mrefu wa zaidi ya masaa mawili kwenda kuchota maji  kitu ambacho kinawaumiza  huku miradi mbalimbali ikikwama kwa kukosa maji.


 "Mheshimiwa Naibu Waziri mradi huu wa Iwela ni mkubwa sana! hivyo tunaweza kusambaza maji ya mradi huu hata katika vitongoji na vijiji vya jirani kama Kisaula , Lutala na kwingineko",amesema Kamonga.


Aidha kwa upande wa Naibu Waziri huyo amesema kiasi hicho cha fedha kitagawanywa katika baadhi ya maeneo yenye shida zaidi ili kuweza kuwapunguzia adha wanayoipata.


"Mbunge wenu alikuwa akinisumbua sana kwa kunitaka nifike katika jimbo lake na kuona changamoto hii ya maji inayowapata wananchi wake, na sasa nimefika nimejionea kwa macho yangu hivyo serikali haina budi kuleta fedha ili tumtue mama ndoo kichwani", amesema Mhandisi Mahundi


Hata hivyo Naibu Waziri huyo amemuagiza mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Iringa (IRUWASA) David Palangyo kuwasilisha andiko la kuongeza usanifu mpya wa vitongoji ambavyo vimekosa maji ya mradi wa Iwela.


Naibu Waziri huyo amesema mradi huo umejengwa kwa kutumia 'force account' na kuweza kuokoa milioni 500 mpaka kukamilika kwa mradi hivyo kuna uwezekano wa chenchi kubaki ambayo ndiyo itakayosaidia kuongeza mabomba ya maji.

 

Naibu Waziri wa maji mhandisi Merryprisca Mahundi sambamba viongozi mbalimbali wakiangalia maji yanayotiririka kutoka kwenye tenki la mradi
Naibu waziri wa maji Merryprisca Mahundi akiteta jambo na mbunge wa jimbo wa Ludewa wakati wa mkutano na wananchi wa kijiji cha Lihagule
Naibu waziri wa maji mhandisi Merryprisca Mahundi (kulia) akiwa na mbunge wa jimbo la Ludewa(kushoto) sambamba na viongozi mbalimbali wakikagua bomba la maji katika eneo la mradi wa maji wa Iwela.

Naibu waziri wa maji mhandisi Merryprisca Mahundi akicheza ngoma ya mganda baada ya kuwasili katika Kijiji cha Lihagule wilayani Ludewa mkoani Njombe
Baadhi ya viongozi wa chama na serikali waki wakiwa kwenye mkutano na wananchi wa kata ya Iwela kutoka kushoto ni diwani wa kata ya Iwela Joackim Lukuwi, mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba, Naibu waziri wa maji mhandisi Merryprisca Mahundi, mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere, mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Wise Mgina.
Mkuu wa wilaya Andrea Tsere (kushoto) akiongea na naibu waziri wa maji mhandisi Merryprisca Mahundi mara baada ya kuwasili wilayani Ludewa.
Naibu waziri wa maji mhandisi Merryprisca Mahundi (kushoto) akiteta jambo na mwananchi mkazi wa kijiji cha Lihagule wilani ludewa mkoani Njombe.