Matokeo chanyA+ online




Monday, August 5, 2019

RAIS DKT JOHN MAGUFULI AFUNGUA MAONESHO YA WIKI YA VIWANDA KWA NCHI ZA SADC JIJINI DAR

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akihutubia katika ufunguzi wa maadhimisho na maonesho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 5, 2019. Yenye kauli mbiu: Mazingira Wezeshi kwa Maendeleo na Jumuishi ya Viwanda, Kukuza Biashara na Ajira ndani ya Jumuiya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika ufunguzi wa maadhimisho na maonesho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Yenye kauli mbiu: Mazingira Wezeshi kwa Maendeleo na Jumuishi ya Viwanda, Kukuza Biashara na Ajira ndani ya Jumuiya.
Katibu Mtendaji Sekretariati ya SADC Dkt Stergomena Tax akizungumzia katika ufunguzi wa maadhimisho na maonesho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akibadirishana mawazo na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Innocent Bashungwa (kulia) wakati wa ufunguzi wa maadhimisho na maonesho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mtendaji Sekretariati ya SADC Dkt Stergomena Tax wakati wa ufunguzi wa maadhimisho na maonesho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar, Mheshimiwa Balozi Amina Ally
 Wageni waalikwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akiangalia burudani ya ngoma wakati wa ufunguzi wa maadhimisho na maonesho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam.

Sunday, August 4, 2019

RAIS DKT MAGUFULI NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WASHIRIKI MISA TAKATIFU YA DOMINIKA YA 18 YA MWAKA "C"

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Paul Haule, Agosti 04,2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Paul Haule, Agosti 04,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakitoa sadaka pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakati wa Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam katika Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Paul Haule leo Jumapili Agosti 04,2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam leo Jumapili Agosti 04, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Janeth Magufuli wakipeana mkono wa Amani na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki walioshiriki Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoka nje na kusalimiana na waumini wenzao baada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 18 ya Mwaka "C" katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Agosti4, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Simon Sirro nje ya kanisa Katoliki mara baada ya Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaamleo Jumapili Agosti 04, 2019.

  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimnunulia  IGP Simon Sirro na kijana fulana maalumu za sherehe ya kutimiza miaka 75 Muadhama Polycarp Kadinali Pengo  baada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 18 ya Mwaka "C" katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Agosti4, 2019
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimnunulia muumini Rosari baada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 18 ya Mwaka "C" katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Agosti4, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaliana na muumini na mtoto wake mara baada ya Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam leo Jumapili Agosti 04, 2019.

Saturday, August 3, 2019

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MSOGA WAMTEMBELEA RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE



Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akiwa amebeba maua ambayo amepewa zawadi na wanafunzi wa Shule ya Msingi Msoga waliomtembelea nyumbani kwakwe Kijijini Msoga,Mkoani Pwani.

Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akiwa amebeba maua ambayo amepewa zawadi na wanafunzi wa Shule ya Msingi Msoga waliomtembelea nyumbani kwakwe kijijini Msoga,Mkoani Pwani.




Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akiwa  na wanafunzi wa Shule ya Msingi Msoga waliomtembelea nyumbani kwakwe Msoga,Mkoani Pwani.

Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akipokea zawadi ya maua kutoka kwa  wanafunzi wa Shule ya Msingi Msoga waliomtembelea nyumbani kwakwe Msoga,Mkoani Pwani.

Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akiwa  na wanafunzi wa Shule ya Msingi Msoga waliomtembelea nyumbani kwakwe Msoga,Mkoani Pwani.

Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akiwa  na wanafunzi wa Shule ya Msingi Msoga waliomtembelea nyumbani kwakwe Msoga,Mkoani Pwani.

Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akiwa  na wanafunzi wa Shule ya Msingi Msoga waliomtembelea nyumbani kwakwe Msoga,Mkoani Pwani.


Wanafunzi wa Shule ya Msingi Msoga

Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akiwa  na wanafunzi wa Shule ya Msingi Msoga waliomtembelea nyumbani kwakwe Msoga,Mkoani Pwani.

LUKUVI AMREJESHEA ENEO LAKE BRIGEDIA JENERALI MSTAAFU BAADA YA KULIHANGAIKIA KWA MIAKA 20

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amemrejeshea eneo lake lililoko Jangwani Beach wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam Brigedia Jenerali Mstaafu Francis Mbena kufuatia kuhangaika kwa miaka 20 kulirejesha eneo alilodhulumiwa.

Akizungumza wakati akimkabidhi hati ya kiwanja chake leo eno la Mbezi Beach Dar es Salaam Lukuvi alisema, Brigedia Mstaafu Mbena alitaka kudhulumiwa eneo lake na Idan Mongi aliyeuziwa eneo hilo na John Rwechungura.

Kwa mujibu wa Lukuvi, kiwanja hicho chenye ukubwa wa takriban mita za mraba 2000 hati yake iligushiwa na baadaye kiwanja hicho kuuzwa kwa Mongi ambapo alieleza mnunuzi huyo alitapeliwa kwa kuwa kiwanja kilikuwa kimefutwa.

Lukuvi alitoa onyo kwa wanasheria kuacha tabia ya kuchelewesha kesi kwa kutowaeleza ukweli wateja wao iwapo kesi wanayoishughulikia hawezi kushinda na kufafanua kuwa ni bora wanasheria wakawaeleza ukweli kuhusiana na mwenendo wa kesi wanazoziendesha kuhusina na masuala ya ardhi.

Aidha, amewataka wananchi wanaotaka kununua viwanja kufanya utafiti katika ofisi ya Msajili wa Hati Wizarani kwa lengo la kujiridhisha umiliki wa muuzaji wa eneo husika.

Kwa upande wake Brigedia Jenerali Mstaafu Mbena amefurahishwa na uamuzi uliofanywa na Lukuvi wa kumpatia hati yake aliyoihangaikia kwa miaka 20 na kueleza kuwa eneo hilo limekuwa likimtesa sana kwa kuendesha kesi kwa muda mrefu na kutumia fedha yake ya pensheni kuendeshea kesi.

Mbena alisema eneo hilo alilipata mwaka 1988 Oktoba 3 na kuingia katika mgogoro baina yake na watu wanaodai kulimiki kuanzia mwaka 1999ambapo kesi ilianzia Baraza la Ardhi na Nyumba na kufikia Mahakama Kuu amapo iliisha mwaka jana Julai na Mbena kushinda.

Naye Idan Mongi aliyetapeliwa kiwanja hicho alieleza kuwa kiwanja alichotapeliwa kina historia ndefu ambapo kabla yeye kukinunua kilipitia kwa wamiliki wengine watatu na kubainisha kuwa yeye alikinunua kwa John Rwechungura mwaka 2009.

Alisema kuwa, anamkabidhi eneo lake Brigedia Mstaafu Mbena kwa moyo mmoja na hatabomoa nyumba na ukuta aliojenga na ameomba kuhamisha vitu vyake ndani ya miezi mitatu.

Lukuvi alisema, kutokana na uungwana aliounesha Idan Mongi Wizara itamzawadia kiwanja katika eneo la Pemba na Mnazi Kigamboni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya kuishi tu.

Friday, August 2, 2019

RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI SHAREHE ZA MBIO ZA MWENGE WA UHURU

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mke wake Mhe. Mama Salma Kikwete walipata fursa ya kushiriki sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru kijijini Msoga.

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mke wake Mhe. Mama Salma Kikwete walipata fursa ya kushiriki sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru kijijini Msoga.

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mke wake Mhe. Mama Salma Kikwete walipata fursa ya kushiriki sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru kijijini Msoga.

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mke wake Mhe. Mama Salma Kikwete walipata fursa ya kushiriki sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru kijijini Msoga.

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mke wake Mhe. Mama Salma Kikwete walipata fursa ya kushiriki sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru kijijini Msoga.

Thursday, August 1, 2019

RAIS MAGUFULI: SISI WATANZANIA TUMEAMUA NA TUNAO UWEZO WA KUTEKELEZA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika uzinduzi huo.


Rais Dkt. John Magufuli amesema Tanzania imeamua na ina uwezo mkubwa wa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo nchini pasipo kutegemea fedha zenye masharti zinazotolewa kutoka kwa wafadhili na wadau wa kimataifa wa maendeleo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la 3 la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi (Agosti 1, 2019), Rais Magufuli alisema uzinduzi wa Jengo la Uwanja huo ni ushahidi wa wazi wa usimamizi na nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali zinazotokana na kodi ya wananchi.

Aliongeza Jengo la Uwanja huo limejengwa kwa asilimia 100 kutokana na kodi za Watanzania, na hivyo kuiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD) kusimamia vyema miundombinu ya Uwanja huo kwa kuhakikisha kuwa inatunzwa ili kuakisi vyema taswira ya Jiji la Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema jengo hilo litakalokuwa na uwezo wa kuhudumia jumla ya abiria Milioni 6 kwa mwaka limeigharimu Serikali kiasi cha Tsh Bilioni 722 ambazo ni fedha zilizotolewa na Serikali, limeweza kuifanya Serikali kuaminika na kuwa na udhubutu wa kutekeleza miradi ya Maendeleo kupitia fedha za ndani.

“Ipo miradi mingi ya Maendeleo tunayoisimamia kwa fedha zetu za ndani ikiwemo Ujenzi wa reli ya kisasa, mradi wa kufua umeme Mto Rufiji, Barabara za Juu Ubungo, Daraja la Kigongo-Busisi, Daraja la Salender, Ujenzi na ukarabati wa Viwanja vya ndege 15, kujenga rada 4 katika Viwanja vya Ndege vya Dar Salaam, Mwanza, Mbeya na Kilimanjaro, huu ni ushahidi wa usimamizi imara wa fedha zetu za ndani” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya sekta ya anga nchini, kwa kuwa sekta hiyo imekuwa kiungo muhimu katika maendeleo ya sekta ya Utalii, kwani kila siku takribani watu Milioni 12 duniani hutumia usafiri wa anga kutokana na kuwa njia ya haraka na ya uhakika kwa ajili ya usafirishaji wa abiria na mizigo.

Akifafanua zaidi Rais Magufuli aliitaka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutoa kipaumbele kwa makampuni ya kitanzania yanapewa nafasi katika maduka yatakayofunguliwa ndani ya Uwanja huo ili kuwawezesha kufaidi matunda ya kodi yao sambamba na kuweza kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale alisema tangu mwaka 2004-2011 Serikali imechukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya majengo ya Uwanja wa ndege vyaJulius Nyerere ikiwemo ujenzi wa Jengo jipya la tatu la abiria katika uwanja huo, kutokana na majengo ya sasa ya jengo la I na II kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uwezo mdogo wa kuhudumia abiria.

Anaongeza kuwa ujenzi wa Jengo hilo la tatu la abiria lilisimama ujenzi wake mwaka 2016 kutokana na mkandarasi kudai Tsh Bilioni 29, ambapo awali alishapokea kiasi cha Tsh Bilioni 380 kati ya Tsh Bilioni 560 zilizohitajika kwa ajili ya ukamlishaji wa jengo hilo hapo awali, lakini mwaka 2017 Serikali ilitoa zabuni ya ujenzi wa mradi huo kwa mkandarasi mwingine kutokana mkandarasi aliyepita kuwa na kasi ndogo ya utekelezaji wa mradi.

Kwa mujibu wa Mhandisi Mfugale alisema kutokana na kasoro zilizojitokeza, shughuli za ujenzi wa jengo hilo zilipelekwa kwa kampuni ya TECU na mshauri mwelekezi kampuni ya Arab Contractor ambapo hadi kufikia Mei 29 mwaka huu zilikamilisha ujenzi wa jengo hilo na kusubiri kukabidhiwa kwa Serikali kwa ajili ya kuanza kutumika kwake.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama alisema hadi kufikia sasa jumla ya makampuni 18 kati ya 23 ya kimataifa tayari yamehamishia shughuli zao katika Uwanja huo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma za usafiri kwa abiria wanaosafiri kwenda nje ya nchi.

Aliongeza kuwa katika kuimarisha usimamizi bora wa Jengo la Uwanja huo, Mamlaka hiyo pia imewapatia mafunzo watumishi wake kwa ajili ya kupata uelewa wa pamoja wa namna bora ya kulinda miundombinu ya Uwanja huo na hadi sasa imepokea Tsh Milioni 500 kutoka Serikalini ilizozilipa kwa mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo.

MAKAMU WA RAIS AONYA MATUSI NA VITENDO VYA UDAHALILISHAJI MASOKONI



F87A0909-1024x683

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Funguo ya Pikipiki Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith S. Mahenge Baada ya kuzindua rasmi Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko kwa ajili ya kuongeza Chachu ya kurahisisha Usafiri katika kufanikisha zoezi hilo, Jumla ya Pikipiki 14 zilitolewa kwa Mkoa wa Dodoma . Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
F87A0699-1024x683 F87A0703-1-1024x683 F87A0709-1-1024x683
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Wajasiriamali Wanawake katika Mkoa wa Dodoma alipotembelea Mabanda ya Maonesho kwenye Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
F87A0887-1-1024x683
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Bango Juu kama ishara ya Uzindua rasmi Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko pamoja na ugawaji wa Pikipiki 14 kwa Maafisa wa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino Dodoma kwa ajili ya kuongeza kurahisisha Usafiri katika kufanikisha kutokomeza Ukatili na Unyanyasaji kwa Wanawake na watoto . Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Katikati Mwenyekiti wa ALAT Taifa na Meya wa Manispa ya Shinyanga Mhe. Gulamhafeez Z. Mukadam na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
F87A0719-1024x683 F87A0725-1024x683
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Masokoni Wanawake na Wanancho wa Dodoma, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akihutubia kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
F87A0940-1024x683
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mratibu wa Umoja wa Mataifa Tanzania Alvaro Rodriquez walipokutana kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
F87A0946-1024x683
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake (UN WOMEN) Bibi. Hadon Addou walipokutana kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
index-119-1024x683
Mwenyekiti wa ALAT Mhe Gulamhafeez Mukadam,akizungumza na Wafanyabishara Wanawake wa Masokoni na Wananchi wa Dodoma kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
F87A0868-1024x683
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Wafanyabishara Wanawake wa Masokoni na Wananchi wa Dodoma kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 

index-120-1024x683
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Wafanyabishara Wanawake wa Masokoni na Wananchi wa Dodoma kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
F87A0896-1024x683
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata Utepe kuzindua rasmi Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko pamoja na ugawaji wa Pikipiki 14 kwa Maafisa wa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino Dodoma kwa ajili ya kuongeza kurahisisha Usafiri katika kufanikisha kutokomeza Ukatili na Unyanyasaji kwa Wanawake na watoto . 
 
 Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema watu wanatumia matusi ni watu waliokosa malezi kwa namna tofauti tangu wakiwa wadogo hivyo kuitaka Jamii ya Watanzania kutumia nguvu nyingi katika malezi ya watoto ili kuepukana na athari za ukosefu wa malezi ukubwani. 

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hayo leo jijini Dodoma katika hotuba yake ya uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo ya masoko na zoezi la ugawaji wa pikipiki kwa waataalam wa maendeleo ya Jamii leo Jijini Dodoma. 

Aidha Makamu wa Rais amekemea wanaume wanaotumia lugha ya matumisi katika maeneo ya masoko kuwa yanasabababisha wakina mama wafanya biashara Sokoni kukosa uhuru na hata kushindwa kuleta watoto wao sokoni kwa ajili ya kuwasaidia kwa kutopenda vijana wao kusikia lugha isiyokuwa na maadili. 

“Mnawazalilisha wanawake kwa kuwatukana matusi kwa kutumia viungo vyao, kuwashika au kuwapapasa bila idhini yao kwanini nyie wanaume msishikane wenyewe vitendo vya kuwazalilisha wanawake havikubaliki kabisa’’. Alisisitiza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan. 

Katika hotuba yake hiyo Makamu wa Rais wa Tanzania amesema vitendo hivyo vya ukatili havikubaliki na ndio maana ya ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ibala ya 168 c inasema wanawake wanayo haki ya kulindwa dhidi ya unyanyasaji wa aina yoyote ile hivyo hatua za kukomesha vitendo vya ukatili dhidi yao ni utekelezaji wa ilani hiyo. 

Pamoja na kukemea vitendo hivyo Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wanaume wanaonyanyaswa Kijinsia wasione aibu bali watoe taarifa kwenye dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi ili Serikali iweze kupata takwimu sahihi ili iweze kufanyia kazi chanagamoto hiyo. 

Aidha Makamu wa Rais amehoji wanawake walio katika Kamati ya Soko kwanini wanafumbia macho vitendo vya ukatili ili hali wao ni viongozi watoa maamuzi sokoni hapo na kuonya kuwa uenda na wao wanachangia kuendelea kuwepo kwa ukatili katika maeneo ya sokoni. 

Makamu wa Rais amewataka viongozi wa masoko nchini kuhakikisha wanafanyia kazi tabia ya watoto wadogo kufanya biashara sokoni kwa lengo la kusaidia familia na kuutaka uongozi wa soko kuwahoji na kuwarudisha shuleni ili kusaidia kukata mnyororo wa umasikini wa familia kwani mtoto akipata elimu inamsaidia kutumia elimu yake kupambana na umasikini. 

Kwa upande wake Waziri wa Afya, MAendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemwomba Makamu wa Rais kuagiza Halmashauri zote nchini kuacha kutoa kiwango kidogo cha mikopo kwa akina na mama na waongeze kiwango cha fedha ili wakinamama wapate miradi ya maana ya biashara kupitia makato ya 4% ya mapato ya kwa Halmashauri. 

“Unakuta kikundi cha akina mama watano wapewa mkopo wa laki tano nakugawana fedha kidogo hii ni pesa gani ndio maana wakina mama wanaishia kuila na kushindwa kufanya marejesho kwa kuwa fedha hii inakuwa haitoshi kufanya chochote’’ Aliongeza Waziri Mwalimu. 

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema Wizara kwa kushirikiana na wadau wataendelea kutafuta na kugawa Pikipiki kwa Mikoa mingine baada ya Mkoa wa Dodoma ili kuwawezesha Maafisa Maendeleo nchini kutoa elimu kwa jamii kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto. 

Dkt. Jingu amesema kuwa Wizara imetoa pikipiki 25 kwa mkoa wa Dodoma na mapema mwezi ujao itatoa pikipiki kumi na tano kama hizo kwa Mkoa wa Rukwa ili kuwawezesha Maafisa Maendeleo Mkoani humo kutumia usafiri huo kuelimisha wananchi kuhusu ukatili na unyanyasaji dhidi ya Wanawake na Watoto. 

Naye Beatrice Siame ambaye ni Mwakilishi wanawake Soko la Majengo ameiomba Serikali kusimamia usawa wa kijinsia katika maeneo ya kazi ili wanawake waweze kunufaika na kuwezeshwa kiuchumi lakini pia akibainisha kuwa changamoto ya soko ya bidhaa zao ni kikwazo katika kumwendeleza mwanamke kiuchumi. 

Uzinduzi wa Mradi wa kupinga unyanyasaji na udhalilishaji wanawake kijinsia katika Masoko ni hatua muhimu ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto unaolenga kutokomeza vitendo vya ukatili Nchini kwa 50% ifikapo 2022.

LIVE:RAIS MAGUFULI KATIKA UZINDUZI WA JENGO LA TATU LA ABIRIA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE


MAADHIMISHO NA MAONESHO YA NNE YA WIKI YA VIWANDA YA JUMUIYA YA MAENDELEO YA KUSINI MWA AFRIKA (SADC)

Mabanda yatakayotumika katika maonyesho ya viwanda ya SADC ambayo yanatarajia kuanza rasmi tarehe 5-9 Agosti 2019 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwl.Nyerere jijini Dar es Salaam
KAULIMBIU:  MAZINGIRA BORA KWA MAENDELEO ENDELEVU NA JUMUISHI YA VIWANDA, KUKUZA BIASHARA KIKANDA NA AJIRA

#39SADCSummit

#SIW2019


Mabanda yatakayotumika katika maonyesho ya viwanda ya SADC ambayo yanatarajia kuanza rasmi tarehe 5-9 Agosti 2019 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwl.Nyerere jijini Dar es Salaam

Mabanda yatakayotumika katika maonyesho ya viwanda ya SADC ambayo yanatarajia kuanza rasmi tarehe 5-9 Agosti 2019 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwl.Nyerere jijini Dar es Salaam

Mabanda yatakayotumika katika maonyesho ya viwanda ya SADC ambayo yanatarajia kuanza rasmi tarehe 5-9 Agosti 2019 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwl.Nyerere jijini Dar es Salaam

LIVE CATCH UP: RAIS MAGUFULI KATIKA UZINDUZI WA KIWANDA CHA KUSAGA NAFAKA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM