Tuesday, January 14, 2020
WAZIRI DKT. KALEMANI AKAGUA TENA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA MAJI WA JULIUS NYERERE MW 2115, AAGIZA WAKANDARASI KUHAKIKISHA WAFANYAKAZI WAO WOTE WANAHAMIA ENEO LA MRADI
NA
MWANDISHI WETU, RUFIJI
Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, amefanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere Mw 2115 (JNHPP) uliotimiza mwaka mmoja
tangu kuanza kwa utekelezaji wake. Dkt. Kalemani ameridhishwa na hatua
mbalimbali ambazo mradi huo unaotekelezwa kwenye mto Rufiji kwenye mpaka wa
mikoa ya Pwani na Morogoro umefikia tangu kuanza kwa ujenzi wa mradi.
Aidha, alitoa maagizo kwa Wakandarasi kuhakikisha Wafanyakazi wao wote wanahamia eneo la mradi, huku akitoa mwezi mmoja kwa wafanyakazi wengine wa mradi wawe wamehamia.
"Wafanyakazi wote wakae eneo la mradi, hii itaharakisha mradi kukamilika mapema na haraka", alisema Dkt. Kalemani. Pia, alisisitiza kazi zote zinazohusu utoaji huduma zifanywe na Makampuni ya kitanzania ikiwemo Wakandarasi wasaidizi.
Mkataba wa ujenzi mradi wa Julius Nyerere ulisainiwa Desemba 12, 2018 Ikulu Jijini Dar ea Salaam ambapo Mkandarasi alikabidhiwa eneo la mradi Februari 14, 2019 na kuanza kazi za maandalizi ya ujenzi kwa kipindi cha miezi sita, ambapo mwezi Juni 2019 alianza rasmi kazi za ujenzi. Mradi wa Julius Nyerere unatarajiwa kukamilika 14 Juni 2022
Aidha, alitoa maagizo kwa Wakandarasi kuhakikisha Wafanyakazi wao wote wanahamia eneo la mradi, huku akitoa mwezi mmoja kwa wafanyakazi wengine wa mradi wawe wamehamia.
"Wafanyakazi wote wakae eneo la mradi, hii itaharakisha mradi kukamilika mapema na haraka", alisema Dkt. Kalemani. Pia, alisisitiza kazi zote zinazohusu utoaji huduma zifanywe na Makampuni ya kitanzania ikiwemo Wakandarasi wasaidizi.
Mkataba wa ujenzi mradi wa Julius Nyerere ulisainiwa Desemba 12, 2018 Ikulu Jijini Dar ea Salaam ambapo Mkandarasi alikabidhiwa eneo la mradi Februari 14, 2019 na kuanza kazi za maandalizi ya ujenzi kwa kipindi cha miezi sita, ambapo mwezi Juni 2019 alianza rasmi kazi za ujenzi. Mradi wa Julius Nyerere unatarajiwa kukamilika 14 Juni 2022
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, (kushoto), akimsikiliza Mratibu wa ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius NyerereMw 2115 (JNHPP) wa mto Rufiji mkoani Pwani, Mhandisi Steven Manda wakati alipofanya ziara ya kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.
Dkt. Kalemani (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kushoto kwa waziri), wakati wa ziara hiyo leo Januari 12, 2019.
RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri
Ikulu jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020 |
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri
Ikulu jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020 |
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri
Ikulu jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020 |
RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI WA AFRIKA KUSINI, ZIMBABWE, NAMIBIA NA NIGERIA
Rais Dkt. John Magufuli tarehe 14 Januari, 2020 amewaapisha Mabalozi 4 aliowateua hivi karibuni kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Afrika Kusini, Namibia, Zimbabwe na Nigeria.
Walioapishwa
ni Mej. Jen (Mstaafu)
Gaudence Salim Milanzi anayekuwa Balozi wa Tanzania Pretoria - Afrika Kusini,
Dkt. Modestus Francis Kipilimba anayekuwa Balozi wa Tanzania Windhoek –
Namibia, Prof. Emmanuel David Mwaluko Mbennah anayekuwa Balozi wa Tanzania
Harare – Zimbabwe na Dkt. Benson Alfred Bana anayekuwa Balozi wa Tanzania Abuja
– Nigeria.
![]() |
| Mabalozi wakila kiapo |
Baada
ya kuwaapisha, Mhe. Rais Magufuli amewataka kuripoti katika vituo walivyopangiwa
ndani ya wiki 2 kuanzia sasa na amewasisitiza kwenda kutekeleza majukumu yao
kwa mujibu wa sheria, kwa kuzingatia maslahi ya Taifa hasa kiuchumi na
kuwawezesha Watanzania kupata ajira katika fursa zilizopo katika nchi hizo.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi
amewataka Mabalozi hao kufuatilia maeneo yote ambayo Mhe. Rais Magufuli
alikubaliana na Waheshimiwa Marais wenzake alipotembelea nchi hizo hivi
karibuni, na pia kuitangaza vyema Tanzania ambayo kwa sasa inapiga hatua kubwa
katika maeneo mengi.
Hafla
ya kuapishwa kwa Mabalozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu
Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
![]() |
| Add caption |
WAGENI KUTOKA KCMC NA NCHINI MAREKANI WATEMBELEA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA AJILI YA KUONA HUDUMA ZA MATIBABU YA MOYO
MKEMIA MKUU KUANZISHA KANZI DATA YA VINASABA
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali [GCLA] ipo katika
mkakati wa kuanzisha Kanzi Data ya taifa ya Vinasaba vya Binadamu
[DNA] ambayo itakuwa ikitambua asili ya kila Mtanzania na kuweza
kusaidia chunguzi mbalimbali ikiwemo majanga na kupata majibu kwa kina.
Hayo
yameelezwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko wakati
wa ziara ya kampeni ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano
inayojulikana kama ‘Tunaboresha Sekta ya Afya’ ambapo amesema kuwa;
Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha wanafikia malengo ya kusaidia jamii katika upande huo wa vinasaba.
"Kwa
sasa tupo katika mpango wa kuanzisha Kanzi Data ya Taifa ya Vinasaba
ambapo eneo hilo kwa sasa tutaliwekea kipaumbele katika bajeti ya fedha
ya mwaka huu na tayari tumeshaanza kutengeneza mpango kazi wazo dhana
ya utengenezaji wake na itajumlisha wadau mbalimbali na Serikali
kupitia Wizara ya Afya na wadau wengine". Alisema Mkemia Mkuu wa
Serikali Dkt. Mafumiko.
![]() |
| Mkurugenzi anayesimamia Idara ya Huduma ya usimamizi wa vinasaba, David Eliasi akizungumza katika tukio hilo. |
Dkt. Mafumiko
amebainisha kuwa, kutokana na mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano kwa
kuboresha rasilimali watu, miundombinu ya utendeajji kazi na vifaa vya
kisasa ndio maana wamepewa jukumu hilo la kuanzishwa kwa Kanzi data
hiyo sambamba na kujumuisha wadau mbalimbali.
Nae
Mkurugenzi anayesimamia Idara ya Huduma ya usimamizi wa vinasaba,
David Eliasi akizungumzia suala hilo la Kanzi data, amesema kuwa, Mkemia
wa Serikali ndio atakuwa msimamizi na inajengwa na watanznia wenyewe
huku akiwataka watanzania wajivunie juu ya hilo.
"Serikali
ya awamu ya Tano imeweza kuongeza chachu na sasa tunajenga kanzi data
ya Kitaifa ya Vinasaba na inajengwa na Watanzania wenyewe.
Ni
kitu cha kujivunia na timu ya Kitaifa inasimamia huu ujenzi wakiwemo
Wizara ya Afya ambayo ni mlezi wetu, pia wapo EGav- Serikali mtandao,
NIDA, RITA, NEC na taasisi nyingi tu na wote hao wamekaa pamoja na
wamekuja na dhana ya uanzishwaji wa Kanzi data hii ya Kitaifa" alisema
David Eliasi.
Ameongeza kuwa kuanzishwa kwa
kanzi data hiyo, itarahisisha upatikanaji wa haraka wa majibu ya
vinasaba kwani tayari sampuli zitakuwa zinapatikana kwenye data.
"Tutachukua
muda mfupi na wa haraka zaidi. Mfano lile janga la Morogoro la moto,
ndugu wa marehemu wangepatikana kupitia kanzi data hii na tungelipata
majibu kwa haraka na kwa wingi zaidi" alisema Davidi Eliasi.
Aidha,
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imenunua mitambo tisa
kwa gharama ya shilingi bilioni 9.5 kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa
kemikali, sumu, madawa ya kulevya na viambata.
Ambapo pia imeweza kusajili wadau 2426 mwaka 2019 kutoka wadau 4340 mwaka 2015/2016.
Mpaka
sasa Mamlaka hiyo ya Mkemia Mkuu imeendelea kuboresha huduma zake
ikiwemo katika Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Nyanda za Juu Kusini na maeneo
mengine ya Kanda.
NEMC, MGODI WA NORTH MARA WASAINI MAKUBALIANO YA UZINGATIAJI SHERIA YA MAZINGIRA
Subscribe to:
Posts (Atom)


































