Matokeo chanyA+ online




Friday, September 4, 2020

MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO YAPIMWE BAADA YA MIAKA 10 - DKT. JOHN MAGUFULI

Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Bariadi katika mkutano wa Kampeni za Urais kwa upande wa CCM zilizofanyika katika uwanja wa Bariadi mkoani Simiyu


 

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.John Magufuli amesema kwa maendeleo ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imefanya katika miaka mitano haoni sababu ya wananchi kutomchagua ili aendelee kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo, hivyo ni vema akapewa miaka mingine mitano.

 Amesema hayo katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

"Ninawaomba ndugu zangu mnipe miaka mingine mitano ili nimalizie miradi ya maendeleo tuliyoianza na ndio mnipe utendaji wangu kwa miaka kumi" Amesema Magufuli

 


Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Chama
Cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipowahutubia katika Mkutano wake wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi mkoa wa Simiyu  leo Ijumaa Septemba 4, 2020

 


Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa jukwaa kuu na vijana wenye ulkemavu wa ngozi waliohudhuria Mkutano wake wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi mkoa wa Simiyu  leo Ijumaa Septemba 4, 2020

 


Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa jukwaa kuu na vijana wenye ulkemavu wa ngozi waliohudhuria Mkutano wake wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi mkoa wa Simiyu  leo Ijumaa Septemba 4, 2020

Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais Dkt. John Pombe Magufuli akicheza jukwaani na vijana wenye ulkemavu wa ngozi wakati wa Mkutano wake wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi Mkoa wa Simiyu leo Ijumaa Septemba 4, 2020





Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Bariadi katika mkutano wa Kampeni za Urais kwa upande wa CCM zilizofanyika katika uwanja wa Bariadi mkoani Simiyu




  Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Watoto wenye Ulemavu wa Ngozi mara baada ya kuwasili Bariadi mkoani Simyu.

MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MAGANZO, MWIGUMBI NA MASWA AKIWA NJIANI KUELEKEA BARIADI MKOANI SIMIYU

Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Maswa mkoani Simiyu katika mikutano ya Kampeni wakati akiwa njiani kuelekea Bariadi.

Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mwigumbi wakati akielekea Maswa mkoani Simiyu.




Sehemu ya Wananchi wa Maswa wakishangilia mara baada ya Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili wakati akitokea mkoani Shinyanga.

 

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Rais John Magufuli leo ametangaza ajira elfu -13 za walimu nchini.

Amemwelekeza Waziri wa Tamisemi Seleman Jafo kutangaza ajira hizo kuanzia leo ili walimu waliokosa ajira waajiriwe na wasikae nyumbani.

Aidha, Dkt. Magufuli amesema kuanzia jana wakulima wa Pamba wameanza kulipwa madeni yao, ambapo serikali imetoa zaidi ya shilingi Bilioni Moja  ili kulipa madeni yao.

Ametangaza neema hiyo leo katika Mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika Mjini Bariadi akiwa njiani kuelekea Bunda Mkoani Mara kuendelea na Kampeni.

WAZIRI HASUNGA AWASHUSHIA NEEMA WAKULIMA WA KAHAWA KARAGWE NA KYERWA

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akikagua kahawa ya wakulima katika kiwanda cha Kamahungu kinachomilikiwa na Chama Kikuu cha Ushirika Karagwe (KDCU)  wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Kagera Leo tarehe 3 Septemba 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga tarehe 3 Septemba 2020 amewasili Wilayani Karagwe katika mkoa wa Kagera kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, ambapo amekagua shughuli mbalimbali za kilimo.

Katika ziara hiyo Waziri Hasunga amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa vyama vya Ushirika (AMCOS) wa Wilaya ya Kyerwa na Karagwe ambapo amejionea hali ya malipo ya wakulima wa kahawa wanaodai.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Karagwe wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Kagera tarehe 3 Septemba 2020. 

Waziri Hasunga amekiagiza Chama Kikuu cha Ushirika Karagwe (KDCU) kuwalipa wakulima malipo yao ambapo ametoa siku tatu kuanzia tarehe 4 Septemba 2020 mpaka Septemba 6, 2020 Jumla ya Bilioni 7.8 ziwe zimelipwa haraka.

“Ninyi KDCU ndio mmechukua kahawa za wakulimaa mmechukua kwa malikauli wananchi wakawaamini na kuwapa kahawa lakini mkawapa maneno mazuri kwamba mtawalipa kwa wakati lakini mmeshindwa kuwalipa mpaka sasa” Amesisitiza Waziri Hasunga

Viongozi wa Vyama vya Ushirika wa Wilaya ya Karagwe na Kyerwa wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga wakati akizungumza kwenye mkutano uliofanyika Mjini Karagwe wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Kagera Leo tarehe 3 Septemba 2020. 

Ametoa maagizo hayo mbele ya Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wataalamu wa Wilaya ya Karagwe huku akikitaka Shirika la ukaguzi wa hesabu za vyama vya Ushirika (COASCO) kukamilisha ukaguzi wa vyama vya Ushirika ndani ya wiki mbili ili wakulima waweze kulipwa fedha zao za malipo ya nyongeza, Kadhalika ameitaka COASCO kupitia hesabu zao ili waweze kutoa taarifa.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Ushirika wa Wilaya ya Karagwe na Kyerwa wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Kagera Leo tarehe 3 Septemba 2020. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Kagera

Hasunga amesema kuwa ni Marufuku kuchelewesha malipo ya wakulima badala yake Bodi ya Kahawa kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania inapaswa kubainisha njia bora ili kurahisisha malipo ya wakulima.

Vilevile, Waziri Hasunga ameitaka Bodi ya kahawa kujenga maeneo maalumu kwa ajili ya kuhamasisha unywaji wa kahawa wa ndani kwani kufanya hivyo kutaongeza soko la ndani la kahawa.

Thursday, September 3, 2020

MGOMBEA URAIS WA CCM RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA SHINYANGA MJINI



Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Shinyanga mjini katika Mkutano wa Kampeni za Urais kwa upande wa CCM uliofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga leo tarehe 03 Septemba 2020.

 


Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza huku akiwa ameishika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa mwaka 2020-2025 katika mkutano wa Kampeni za Urais kwa upande wa CCM uliofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga leo tarehe 03 Septemba 2020.

 



Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anafurahia wakati akiangalia msanii wa Singeli Sholo Mwamba alipokuwa akitumbuiza katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.  


Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho tawala Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimu wananchi wa Shinyanga waliofurika katika Uwanja wa Kambarage mjijini Shinganya alipohutubia mkutano wa hadhara wa kampeni leo Alhamisi Septemba 3, 2020

 

Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni za Urais leo tarehe 03 Septemba 2020.

 

Wagombea Ubunge na Udiwani wakiamsha amsha mbele ya Mgombea Urais na Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Magufuli na wananchi wa Shinyanga waliofurika katika Uwanja wa Kambarage mjijini Shinganya wakati wa mkutano kampeni leo

 

Nukuu ya leo kuhusu Mkoa wa Shinyanga

"Hapa Shinyanga tumejenga Vituo vya afya 11 kwa thamani ya Bilioni 4.2, tumejenga zahanati 28 zenye thamani ya bilioni 2.08, dawa tumeleta zenye thamani ya bilioni 16.1 kutoka bilioni 4.9 zamani, tumeajiri watumishi wa afya 347 na kujenga nyumba za watumishi 20 zenye thamani ya bilioni 1.3." - Rais Magufuli

MGOMBEA MWENZA KWA TIKETI YA CCM AZUNGUMZA NA WANANCHI KATIKA KIJIJI CHA MIKESE NA BWAWANI



 

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi katika Kijiji cha Mikese na Bwawani Mkoani Morogoro alikuwa akielekea Mkoani Pwani kuendelea na Ziara yake ya Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM  leo Septemba 03,2020.

 


 

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana umati wa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wa kijiji cha Kiwangwa Wilayani Bagamoyo alipokuwa njiani kuelekea Bagamoyo Mjini  Wilaya ya Morogoro Mjini kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa Kampeni wa Chama cha Mapinduzi  leo Septemba 03,2020.


Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia  Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani kwenye mkutano wa Kampeni wa Chama cha Mapinduzi CCM leo Septemba 03,2020.                                       

Wednesday, September 2, 2020

SPIKA JOB NDUGAI AZINDUA JENGO LA TAKUKURU WILAYA YA MANYONI

Spika wa Bunge, Job Ndugai (watatu kulia) akikata utepe wakati akizindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida. Watatu kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Rahabu Mwagisa (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Ndg. Sabina Seja (wapili kulia) na Mbunge wa Manyoni Magharibi, Mhe. Yahaya Masare.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na viongozi wa wilaya, watumishi wa TAKUKURU na wageni mbalimbali kabla ya kuzindua jengo la Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika akizungumza na watumishi wa TAKUKURU na wageni mbalimbali (hawapo kwenye picha) kabla ya uzinduzi wa jengo la Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Mkurugenzi wa uzuiaji Rushwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Ndg. Sabina Seja akizungumza na viongozi wa wilaya, watumishi wa TAKUKURU na wageni mbalimbali (hawapo kwenye picha) kabla ya uzinduzi wa jengo la Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.Spika wa Bunge, Job Ndugai akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili kwa ajili ya kuzindua jengo la Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa baada ya kuzindua jengo la Taasisi hiyo Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida. Wapili kushoto waliokaa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa  Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Rahabu Mwagisa (kushoto waliokaa) na Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Ndg. Sabina Seja (wapili kulia waliokaa)

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AFANYA MAZUNGUMZO NA MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Generali Wilbert A. Ibuge akizungumza na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,
Bw. Zlatan Milišić
 alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 2 Septemba 2020.

Katika mazungumzo yao walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa ambapo Balozi Ibuge alitoa shukrani kwa Shirika hilo kwa ushirikiano uliopo kati yake na Serikali hususan kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kwa upande wake, Bw. 
Milišić aliipongeza Tanzania kwa kudumisha amani na utulivu ambao ni chanzo cha uchumi wa nchi kustawi. Pia aliipongeza kwa kuendelea kuchangia vikosi vya ulinzi wa amani kwenye mataifa mbalimbali  yenye  migogoro duniani na kuitakia Tanzania uchaguzi wa amani na utulivu hapo mwezi Oktoba 2020.
Ujumbe wa Wizara ukimjumuisha Bw. Hangi Mgaka, Katibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bi. Prisca Mwanjesa, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Ibuge na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Milišić (hawapo pichani)


Mazungumzo yakiendelea
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ibuge akiwa katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Milišić mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ibuge akiagana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini, Bw. Milišić mara baada ya mazungumzo kati yao.