Matokeo chanyA+ online




Thursday, November 19, 2020

MAJITAKA KUPEWA KIPAUMBELE SEKTA YA MAJI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba akifungua Kongamano la 8 la Maji jijini Dodoma.

 Baadhi ya washiriki wa Kongamano la 8 la Maji wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba (hayupo pichani) wakati akihutubia kwenye Kongamano hilo  jijini Dodoma.

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba (kushoto) akimsikiliza Mwanafunzi wa Chuo cha Maji, Daudi Sangi akitoa maelezo kuhusu ufanyaji kazi wa pampu ya kusukuma maji alipotembelea mabanda ya Maonesho ya Wazabuni katika Kongamano la Maji  la 8  jiiini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba akiwa na wajumbe wa meza kuu katika Kongamano la Maji  la 8  jiiini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya ATAWAS, Mhandisi Geofrey Hilly akitoa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo katika Kongamano la Maji la 8 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba (kushoto) akisalimiana na miongoni mwa Wadau wa Maendeleo walioshiriki Kongamano la Maji la 8 jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Nadhifa Kemikimba ameitaka Jumuiya ya Wasambazaji Maji Tanzania (ATAWAS) kutoa kipaumbele kwenye eneo la majitaka baada ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la usambazaji wa majisafi.

Mhandisi Kemikimba ametoa maelekezo hayo katika uzinduzi wa Kongamano la 8 la Maji katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper, jijini Dodoma.

“Kuna mafanikio makubwa kwa upande wa usambazaji maji, lakini kwa upande wa majitaka bado. ATAWAS mnatakiwa kuwekeza kiasi kikubwa kwenye eneo hili, ambapo lengo letu ni kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2025 kwa sababu majisafi ni mengi na itachangia kuwepo kwa majitaka mengi “, amezungumza Naibu Katibu Mkuu.

“Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano ili kufanikisha azma hiyo, lakini pia ni lazima katika majadiliano yenu muweke msisitizo kwenye utafiti na ubunifu kwa kuwatumia Taasisi za Elimu ya Juu ili kuweza kupata suluhisho la kudumu litakalomaliza changamoto zote”, amesisitiza Mhandisi Kemikimba.

Kadhalika, Naibu Katibu Mkuu ametoa wito kwa wadau wote wa Sekta ya Maji nchini kushirikiana na ATAWAS ili kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maji kwa sababu peke yao hawatafanikiwa.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya ATAWAS na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA), Mhandisi Geofrey Hilly amesema ATAWAS imezindua rasmi mpango wa kuwajengea uwezo wanachama wake kwenye eneo la menejimenti ya rasilimali fedha, ukizingatia kuwa miongoni mwa changamoto kubwa ambazo zinazozikabili Mamlaka za Maji na sekta kwa ujumla, ni usimamizi wa fedha za utekelezaji wa miradi mijini na vijijini.

Pia, ameongeza kuwa ATAWAS pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu zimeshasaini mkataba wa ushirikiano kwenye eneo la utafiti kwa lengo la kupata suluhisho la kudumu changamoto za kisekta.

Lengo la Kongamano hilo ni kujadiliana, kutathimini na kuzipatia ufumbuzi  changamoto za kisekta na kubaini fursa zilizopo ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kufikia  dira ya Taifa ya mwaka 2025, pamoja na lengo la sita (6) la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2030.

TFCG na MJUMITA WACHOCHEA KUWEPO USAWA WA KIJINSIA KATIKA JAMII KWENYE UHIFADHI SHIRIKISHI WA MISITU


Rasi wa Ndaki ya Misitu Wanyamapori na Utalii  SUA, Prof. Suzan Augustino akiwasilisha matokeo ya utafiti huo wa masuala ya kijinsia kwa wadau wa uhifadhi shirikishi wa misitu  nchini.
Prof. John Jackoniah ambaye ni mmoja wa watafiti kutoka Ndaki ya sayansi za jamii na Insia ya Chuo kikuu cha sokoine cha kilimo SUA  akiwasilisha sehemu ya utafiti huo wa mbele wa wadau hao wa misitu mjini Morogoro.
Mkurugenzi msaidizi wa Shirika la TFCG bwana Emmanuel Lyimo akieleza malengo ya utafiti huo uliofanywa na watafiti kutoka SUA kabla ya kuanza rasmi kusikiliza matokeo hayo ya utafiti.
Baadhi ya wadau kutoka TFCG,MJUMITA, Wizara ya Maliasili na utalii,Waandishi wa habari na maafisa Misitu kutoka halmashauri za wilaya wakifuatilia uwasilishwaji wa matokeo hayo.
Baadhi ya wadau kutoka TFCG,MJUMITA, Wizara ya Maliasili na utalii,Waandishi wa habari na maafisa Misitu kutoka halmashauri za wilaya wakifuatilia uwasilishwaji wa matokeo hayo.
Baadhi ya wadau kutoka TFCG,MJUMITA, Wizara ya Maliasili na utalii,Waandishi wa habari na maafisa Misitu kutoka halmashauri za wilaya wakifuatilia uwasilishwaji wa matokeo hayo.
Baadhi ya wadau kutoka TFCG,MJUMITA, Wizara ya Maliasili na utalii,Waandishi wa habari na maafisa Misitu kutoka halmashauri za wilaya wakifuatilia uwasilishwaji wa matokeo hayo.


Na Calvin Edward Gwabara, Morogoro


Utafiti uliyofanywa na Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) umebainisha kuwa usawa wa kijinsia unaimarika na kuzingatiwa sana kwenye vijiji vinavyoshiriki miradi ya uhifadhi shirikishi wa Misitu kupitia Shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania -TFCG.

Hayo yamebainika na Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyama pori na utalii Profesa. Suzan Augustino  wakati wa  uwasilishwaji wa matokeo ya utafiti mbele ya wadau wa misitu mjini Morogoro na kusema kuwa jitihada kubwa zimefanywa na TFCG na Mtandao wa Jamii wa usimaizi wa Misitu Tanzania MJUMITA kwa kuhakikisha jamii yote inashirikishwa na inanufaika na rasilimali zitokanazo na misitu hiyo.

“ Kuna mabadiliko makubwa chanya kwenye vijiji ambavyo TFCG na MJUMITA wanatekeleza miradi yao hasa wa mkaa endelevu ikilinganishwa na vijiji vilivyo nje ya mradi ingawa wanaume wanaongoza kwenye kazi zinazohitaji nguvu” alibainisha Prof. Suzan.

Prof. Suzan alisema kuwa kwenye Mradi wa Mkaa Endelevu wanawake wanakuja juu katika kushiriki kwenye biashara hiyo ijapokuwa wao wanatumia fedha kulipa watu kufanya kazi zao kama vile kukata magogo, kuyakusanya na kupanga tanuri la mkaa kazi ambazo zinaonekana kuhitaji nguvu zaidi.

Aidha Suzan alisema kuwa baadhi ya vijiji vina ushiriki mdogo wa wanawake na hiyo kwa mujibu wa utafiti wao wamesema inasababishwa mila na  destuli Zao kwamba kazi za maporini hufanywa na wanaume tu na sio wanawake ingawa mitazamo hiyo imeanza kufutika taratibu baada ya jitihada za TFCG na MJUMITA za kutoa elimu.

Prof. Suzan alisema watu wengi wanajua usawa wa kijinsia kwenye ngazi za maamuzi ni kuwa na idadi sawa ya wanawake, wanaume na Makundi mengine lakini ukweli ni kwamba kinachotakiwa kuangaliwa ni nani kawakikisha kundi gani na sauti ya like na mchango wake kwenye kufanya maamuzi maana wanaweza kuwa idadi sawa lakini wote hawana sauti.

Kwa upande wake Prof. John Jackoniah Mtafiti kutoka Ndaki ya Sayansi za jamii na Insia - SUA alisema pamoja na mafanikio hayo ya kuongeza uwiano wa kijinsia kwenye jitihada za usimamizi shirikishi wa Misitu na matumizi ya mapato ya rasilimali hizo lakini wanaume ndio wameonekana kunufaika zaidi.

Alisema kupitia utafiti huo walioufanya kwenye vijiji 10 katika Wilaya za Kilosa, Mvonero na Morogoro wanaume ndio wameonekana kuwa na sauti zaidi kwenye maamuzi na hata kwenye kugawana rasilimali za misitu kwenye maeneo hayo.

“ Lakini utaona wanawake walioolewa ndio wasio na sauti zaidi lakini wale ambao hawajaolewa au waliopewa talaka wananufaika Kama wanaume na Pia wana sauti kwenye kutoa maamuzi na kwenye kugawana mapato ya rasilimali za Misitu” alifafanua Prof. Jackoniah.

Alisema kuwa ushiriki wa wanawake kwenye shughuli za kibiashara za rasilimali za Misitu umeongeza mzigo kwa wanawake kwakuwa kazi za nyumbani nazo zinawaangalia kwakuwa mgawanyo wa majukumu ya nyumbani haujabadilika umebaki palepale.

Akieleza lengo la Utafiti huo Mkurugenzi Msaidizi wa TFCG, Emmanuel Lyimo alisema masuala ya kijinsia yametengenezewa mkakati mahususi wa kuhakikisha yanazingatiwa kikamilifu kwakuwa ni swala mtambuka kwenye maendeleo.

Alisema baada ya kutekeleza Mradi kwa muda sasa wameona wafanye Utafiti huo ili kuona namna maswala hayo yanavyozingatiwa na kutafuta njia za kuboresha zaidi kama kuna vitu Vinakosekana kupitia mapendekezo ya watafiti hao kutoka SUA.

Wednesday, November 18, 2020

RAIS WA ZANZIBAR DK. HUSSEIN MWINYI AMETOA MUDA WA MIEZI MITATU KWA UONGOZI WA WIZARA YA AFYA KUREKEBISHA KASORO ZA KIUTENDAJI

 



Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa muda wa miezi mitatu kwa uongozi wa Wizara ya Afya kurekebisha kasoro za kiutendaji zinazosababisha kutokuwepo  ufanisi katika utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa.

Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo  wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja, alipofika kuangalia utoaji wa huduma kwa wagonjwa katika maeneo na vitengo  tofauti  vya Hospitali hiyo.

Alisema kwa kiwango kikubwa mambo mengi yanahitaji kufanyiwa marekebisho, akibainisha kuwepo changamoto mbali mbali za kiutendaji na hivyo kuzorotesha uapatikanaji wa huduma bora kwa wagonjwa.

Alisema analenga kuchukua hatua za kiutawala dhidi ya watendaji wasiowajibika kazini na kusababisha wananchi kulalamika kutokana na ukosefu wa huduma, pamoja na kupewa lugha zisizordhisha kutoka kwa wauguzi na watendaji wengine  wa Hospitali hiyo.

Aidha, Dk. Mwinyi alisema pamoja na Serikali kuipatia fedha za kutosha Hospitali hiyo kila mwezi, kumekuwepo changamoto za ukosefu wa vifaa muhimu kwa wagonjwa ikiwemo magodoro, dawa na vifaa vya maabara, hivyo akautaka Uongozi wa Hospitali hiyo kubadilika na kuondokana na utendaji wa mazowea.

Alisema pale Serikali inapotoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa na hatimae wagonjwa wakakosa dawa hizo, ni dhahiri kuwa kuna tatizo mahala hapo.

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AKANUSHA KUUZA KIWANJA ALICHOPEWA SINGIDA

Rais mstaafu wa Nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Mzee Andrew (wa pili kulia) ambaye ni mmiliki wa nyumba aliyokuwa akiishi wakati akifanyakazi mkoani Singida. Katikati ni mke wa Mzee Andrew. Wengine ni watoto wa Mheshimiwa Kikwete.

Rais mstaafu wa Nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na wajumbe wa kamati ya siasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida na wananchi waliojitokeza kumpokea alipowasili kwa ajili ya ziara ya siku moja ya kutembelea nyumba alizokuwa akiishi mkoani humo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida, Dk. Denis Nyiraha.
Rais mstaafu wa Nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipata maelezo katika ziara hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida, Dk. Denis Nyiraha.


Hii ni moja ya nyumba aliyowahi kuishi Mhe. Kikwete mkoani Singida.
Rais mstaafu wa Nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Mulagiri. Kutoka kulia ni  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida, Dk. Denis Nyiraha na Katibu wa Itikadi na Uenezi  na Itikadi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida Ahmed Kaburu.


Rais mstaafu wa Nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana Mzee Andrew ambaye ni mmiliki wa nyumba aliyokuwa akiishi wakati akifanyakazi mkoani Singida.


 Na Mwandishi Wetu, Singida


Rais mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekanusha taarifa zilizopo Mkoani Singida kwamba kiwanja alichopewa kwa ajili ya makazi amekiuza kwa moja ya waumini wa makanisa yaliyopo mjini Singida.

Dkt. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM Taifa, alitoa kauli hiyo mjini Singida alipokuwa katika ziara yake ya siku moja ya kutembelea na kukagua nyumba alizowahi kuishi zaidi ya miaka 40 iliyopita wakati akiwa mtumishi wa chama cha TANU.

Alifafanua kiongozi huyo mstaafu kwamba mwaka 1975 akiwa Katibu Msaidizi wa Chama Cha TANU aliishi katika nyumba tano tofauti tofauti kabla na baada ya kwenda jeshini kwa hali hiyo anazifahamu kikamilifu mali za chama mkoani Singida zilipo.

“Kiwanja changu sijampa mtu yeyote yule kama wamechukua kanisa waulizeni,kama ni kiwanja changu waulize,kama ni kiwanja changu tulipatana wapi mimi na wao? alihoji raisi huyo mstaafu.

Akizungumzia moja ya nyumba alizowahi kuishi wakati akiwa mtumishi wa chama katika kipindi hicho,Dkt. Kikwete alisisitiza kwamba nyumba ile alikuwa akiishi baada ya kurejea kutoka jeshini. 

Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu alisema baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa rais na mwenyekiti mstaafu wa CCM, Dkt Jakaya Kikwete watayafuatilia ili waweze kujua ukweli kuhusu kiwanja alichokuwa amepewa kiongozi huyo mkuu ya nchi.

“Tumepokea maelekezo na tutayafuatilia na kwa bahati nzuri na kamisaa wetu DC alikuwepo anasikia kwamba kuna kiwanja cha Mheshimiwa rais mstaafu Jakaya Kikwete eneo la Somoku tutafuatilie vile vile hapo alipokuwa akikaa zamani ambako amesema ilikuwa nyumba ya TANU tutaifuatilia na tutatoia matokeo yake.”alisisitiza Kaburu.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida, Dk. Denis Nyiraha amemuhakikishia Mwenyekiti huyo mstaafu wa chama hicho Dkt.Jakaya Kikwete kuwa kwa kushirikiana na viongozi wa CCM wa mkoa huo watahakikisha moja ya nyumba mali ya TANU aliyokuwa akiishi wakati akifanyakazi mkoani hapa umiliki wake unarudishwa kwenye CCM kwani hivi sasa anaishi mfanyabiashara mmoja.

"Sisi kama vijana wa CCM kwa kushirikiana na viongozi wetu tutafanya uchunguzi ili kujua mfanyabiashara huyo alipateje nyumba hiyo iliyokuwa mali ya TANU na sasa CCM" alisema Nyiraha.

Tuesday, November 10, 2020

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WABUNGE WATEULE WA CCM JIJINI DODOMA


 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Wabunge Wateule wa CCM mara baada ya kuzungumza nao katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma tarehe 09 Novemba 2020



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wabunge Wateule wa CCM katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma tarehe 09 Novemba 2020.

WAZIRI MKUU MSTAAFU MAJALIWA AKIWASILI BUNGENI MJINI DODOMA


Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi akiingia ndani ya ukumbi wa Bunge.
Utatu wa Kazi! Wabunge wa CCM kutoka kulia ni Nape Nnauye wa Jimbo la Mtama, Dotto Biteko wa Jimbo la Bukombe (katikati) na Hussein Bashe wa Nzega Vijijini.
Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Manyara, Asia Kilangi akiingia kwenye viwanja vya Bunge asubuhi ya leo.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (kulia), Patrobas Katambi na Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigonga wakiingia kwenye viwanja vya Bunge mapema asubuhi ya leo.

Mbunge Mteule wa Jimbo la Mlimba Mkoani Morogoro CCM akiingia katika viwanja vya Bunge tayari kuanza shughuli zake za kibunge.

Mbunge Mteule wa Jimbo la Chamwino, Deo Ndejembi (kulia) akiwa na Mbunge Mteule wa Ubungo, Prof Kitila Mkumbo nje ya viwanja vya bungeni mapema leo asubuhi.

 Charles James, Michuzi TV
Ni mwendo wa sauti! Hii ndio kauli unayoweza kusema baada ya leo wabunge waliochaguliwa na wananchi kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuripoti bungeni leo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kibunge.

Michuzi Blog imeshuhudia kundi kubwa la wabunge wakiingia katika viwanja vya Bunge wakiwa wamevalia Suti zao nadhifu za aina mbalimbali.

Akizungumza na Michuzi Blog Mbunge wa Mlimba mkoani Morogoro (CCM), Godwin Kunambi amesema licha ya kuwa ni mara yake ya kwanza kuingia bungeni lakini amejipanga kuhakikisha anafanya kazi yake ya kuisimamia serikali na kuwatetea wananchi wake wa Mlimba waliomchagua kwa kufuata Katiba, Sheria, Kanuni na Miongozo ya Bunge.

Nae Patrobas Katambi mbunge wa Shinyanga Mjini amesema anaamini wingi wa wabunge wa CCM utasaidia kuisimamia serikali katika kuwatumikia wananchi wake.

Shughuli kubwa katika siku ya leo ni kumchagua Spika wa Bunge na kuwaapisha Wabunge tayari kwa kuanza kuwatumikia wananchi.

Tuesday, November 3, 2020

DK.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM ZANBZIBAR


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais mstaafu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ameongoza Kikao Maalum cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.
Kikao hicho kimefanyika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar  iliyopo Kisiwandui.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili mapendekezo ya WanaCCM wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Spika wa Baraza la Wawakilishi mwaka 2020.
Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984,ibara ya 73 Spika wa Baraza la wawakilishi anaweza kuchaguliwa kutoka miongoni mwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi au mtu mwenye sifa za kuchaguliwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  Zanzibar  na Rais Mstaaf wa Awamu ya Saba Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein  na (kulia kwake ) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe Balozi Seif Ali Iddi na (kushoto ) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi wakiwa wamesimama walipowasili katika ukumbi wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM
Kisiwandui Jijini Zanzibar jana 2/11/2020.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi akizungumza wakati wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini

Pamoja na hayo kwa mujibu wa kanuni ya 5 ya kanuni za Baraza la Wawakilishi toleo la mwaka 2020 zinaeleza kwamba kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kinaweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika kwa kuwasilisha jina la mgombea wake Time ya Uchaguzi,hivyo basi CCM inawajibika kufanya mchakato wa ndani ili kupata jiba la mwanachama mmoja atakayegombea Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Katika Kikao hicho kimepokea na kujadili majina ya Wanachama waliojitokeza  kuoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Spika wa Baraza la Wawakilishi mwaka 2020.

Aidha,Kikao hicho kitatoa mapendekezo yake juu ya wanachama wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Spika wa Baraza la wawakilishi Zanzibar  kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambapo Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuteua jina la mwanachama mmoja atakayegombea nafasi ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Akizungumza Dk.Shein, alisema matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 yamevunja rekodi toka enzi za ASP hadi hivi sasa wakati wa mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Alisema wagombea wote wa CCM walikuwa imara na wana sera zinazouzika kwa wananchi.

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Rais Mstaaf wa Awamu ya Saba Mhe.Dk. Ali Mohameed Shein akifungua Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCK Kisiwandui Jijini Zanzibar 2/11/2020.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  Zanzibar na Rais Mstaaf wa Awamu ya Saba Mhe Dk. Ali Mohameed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijinin Zanzibar kuhudhuria Kikao cha Kamati Maalum ya Halmaashauri Kuu ya CCM Zanzibar 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar , kuhudhuria Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar 2/11/2020.

Wajumbe Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakipitia makamrasha yao kabla ya kuaza kwa Kikao hicho kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais Mstaaf wa Awamu ya Saba Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.

 

Picha na Ikulu


NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

Pamoja na hayo aliwasihi wajumbe hao kutobweteka na ushindi uliopatikana badala yake waanze mapema kujiandaa na uchaguzi ujao baada ya miaka mitano.
Aliwashukru Wana CCM wote na wananchi kwa ujumla waliofanya maamuzi sahihi ya kuichagua CCM ili iwaletee maendeleo endelevu kisiasa,kiuchumi na kijamii.
Alieleza kuwa amefika ukomo wa utumishi wake wa kiti cha Urais kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984,na kumkabidhi mrithi wake ambaye ni Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi nchi ikiwa katika mikono salama ya CCM hivyo anatakiwa kuendelea kulinda tunu za Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Akizungumza Makamu mstaafu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, aliwashukru na kuwaaga wajumbe wa Kamati Maalum na kuwasihi waendelee kushirikiana na kushikamana ili CCM iendelee kuwa imara zaidi.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, alisema CCM ina deni kwa wananchi la kutekeleza ahadi zake pamoja na Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025.
Kikao hicho kimeudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.

RAIS WA ZANZIBAR DKT. HUSSEIN MWINYI AANZA KAZI SIKU YA KWANZA TU, AFANYA ZIARA BANDARI YA MALINDI JIJINI ZANZIBAR


Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia Wafanyakazi wa Bandari ya Malindi Jijini Zanzibar alipofanya ziara ya kustukiza katika Bandari ya Zanzibar mchana.

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika ziara yake kutembelea Bandari Kuu ya Malindi leo akiwa katika ziara yale 3/11/2020 na (kulia kwa Rais)
Mdhiniti wa Bandari ya Malindi Jijini Zanzibar Ndg Majaliwa Abdalla Rashid.


Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wac Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi  akimsikiliza Mdhibiti wa Bandari ya Malindi Jijini Zanzibar Ndg. Majaliwa Abdalla Rashid alipofanya ziara kutembelea Bandari hiyo leo 3/11/2020, kujionea utendaji kazi wa Shirika la Bandari Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziMhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji Ndg. Juma Sururu akitowa maelezo wakati wa ziara ya Mhe. Rais alipotembeleaBandari ya Zanzibar 3/11/2020

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziMhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji Ndg.Juma Sururu akitowa maelezo wakati wa ziara ya Mhe. Rais alipotembelea Bandari ya Zanzibar 3/11/2020.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Shirika la Bandari Zanzibar alipofanya ziara yake 3/11/2020, kutembelea bandari hiyo kujionea utendaji kazi wa Bandari ,aloshika kipaza sauti Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Ndg. Ali Haji Haji.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziMhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Shirika la BandariZanzibar alipofanya ziara kutembelea eneo la ujenzi wa Bandari ya Kisasa
Mpigaduri Maruhubi Jijini Zanzibar 3/11/2020.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Shirika la Bandari Zanzibar alipofanya ziara kutembelea eneo la ujenzi wa Bandari ya Kisasa Mpigaduri Maruhubi Jijini Zanzibar 3/11/2020, (Picha na Ikulu)

JUMUIYA YA MARIDHIANO YAMSHUKURU MUNGU UCHAGUZI KUFANYIKA KWA AMANI NA UTULIVU


Mwenyekiti wa Jumuia  ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma, kumshukuru Mungu kwa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika kwa amani na utulivu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo, Askofu Oswald Mlay na  Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma, Askofu Evance Chande. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA




 

Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma.

Mwenyekiti wa Tume ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salumu amewasihi watanzania kuendelea kumshukuru Mungu kwa wema aliowatendea baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika kwa salama na amani.

Ameyazungumza hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, akiwa pamoja na wajumbe wa tume ya kitaifa ya maridhiano na wa mkoa wa Dodoma.

 Aidha, Sheikh Alhad Mussa amesema kuwa inatakiwa sasa baada ya uchaguzi kumalizika salama ni kuungana kuendelea kuiombea kwa Mungu serikali iliyoshinda iongoze vema.

"Tunashukuru Mungu Uchaguzi umeisha kwa amani na salama, kilicho mbele yetu ni kuungana kuendelea  kuiombea Mungu Serikali iliyopo madarakani ituongoze salama.

Katika chaguzi zote kuna kushinda na kushindwa, huwezi kukubalika na kila mmoja  haiwezekani, manabii wa Mwenyezi Mungu na hata Wacha Mungu hawakukubalika nao walipingwa, hii ni desturi ni jambo la kawaida,"amesema Sheikh Alhad. 

Ameshauri upande ambao haujaridhika usisababishe vurugu, bali ufuate taratibu zilizopo ikiwemo ya kisheria na hata jumuia hiyo inaweza kuweka mambo sawa.

"Kubwa tunawaomba Watanzania Nchi yetu iendelee kuwa salama na utulivu, tunahitaji nchi yenye amani ili tuweze kufanya shughuli zetu kwa ukamilifu bila bughudha yoyote, tusijaribu kuchezea amani iliyopo, tutajuta, tuna mifano mingi ya nchi mbalimbali zilizochezea amani, kuirejesha ni ngumu sana."

Amesema viongozi wa Dini walimlilia sana Mungu ili Uchaguzi uvuke kwa salama na amani, hivyo inabidi kumshukuru Mungu  kwa wema wake  aliotutendea. na kwamba wakifanya hivyo Mungu atatuzidishia. 

Alimalizia kwa kutoa shukrani kwa viongozi wote walioiombea kwa Mungu  nchi wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa corona na Uchaguzi Mkuu  na sasa iko salama hivyo tuendelee kumshukuru Mungu naye ataendelea kutusikiliza.