Thursday, April 14, 2022
KINANA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI, JIJINI DAR ES SALAAM
BALOZI KATANGA AKUTANA NA WAZIRI WA NCHI WA U.A.E

Waziri wa nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan, akieleza jambo wakati wa mazungumzo baina yake na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga, Ikulu Jijini Dar es Salaam
*************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Katanga amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa nchi Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Balozi Katanga amekutana na ugeni huo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Sulluhu Hassan. Viongozi hao pamoja na mambo mengine, wamejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) katika nyanja za biashara na uwekezaji pamoja na Ulinzi na Usalama.
Balozi Katanga amemhakikishia Waziri huyo kuwa Tanzania inayo mazingira mazuri ya biashara na salama kuwekeza.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiutoka kwa Umoja huo wakati wote.
Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan amewasili nchini leo kuja kushiriki Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu.
RAIS SAMIA AWASILI WASHINGTON MAREKANI
KITETO WANUFAIKA NA MILIONI 80 ZA MAJOSHO
MRADI WA MAJI WA BILIONI 69 UNATEKELEZWA MWANZA
ANWANI ZA MAKAZI KUTUNZA HISTORIA YA NCHI, WATAKAOHARIBU MIUNDOMBINU KUSHUGHULIKIWA
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akiwa na Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakati wa ziara yake katika mkoa huo kukagua utekelezaji wa operesheni ya Anwani za Makazi.
BALOZI MBEGA AWATAKA WAFANYABIASHARA WA INDIA KUWEKEZA TANZANIA
Balozi wa Tanzania nchini India, Anisa Mbega ametoa wito kwa wafanyabiashara wa nchi hiyo kuja kuwekeza Tanzania kwenye sekta mbalimbali za uwekezaji.
Alitoa wito huo katika kongamano kubwa la biashara
na uwekezaji (Tanzania India Trade Conference) lililofanyika katika jiji la Chennai, India tarehe 11 na 12 Aprili
2022.
Kongamano hilo lililoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ubalozi wa Tanzania nchini India na Taasisi ya Uchumi na Biashara ya India (Indian Economic Trade Organization) lilitoa fursa kwa taasisi mbalimbali
zinazohusika na masuala ya uwekezaji na biashara ikiwepo Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE),
na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwasilisha mada
kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini.
Balozi Mbega alisema licha
ya India kuwekeza nchini mtaji wa kiasi cha Dola za Marekani Bilioni 3.7 na
kuifanya nchi hiyo kuwa ya tano kwa uwekezaji, lakini bado nchi hiyo ina fursa kubwa
ya kuongeza uwekezaji wake nchini.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na wafanyabiashara na wawekezaji takribani 110 ambapo
waliweza kufahamishwa fursa za biashara kwa bidhaa za mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi na fursa za uwekezaji katika
sekta za Miundombinu, Madini, Ujenzi wa majumba, viwanda vya madawa, mitambo ya
viwandani, nguo, Elimu na Afya.
Kutokana na kongamano hilo,
tayari wawekezaji mbalimbali wa India wameonesha nia ya kuwekeza nchini
Tanzania ambapo kundi la kwanza la wawekezaji kwenye sekta ya ujenzi wa viwanda
vya madawa ya binadamu na vifaa tiba kutoka India, linatarajiwa kutembelea
Tanzania kuanzia tarehe 19 Aprili 2022 ili kukutana na wadau na kuanza taratibu
za kuwekeza Tanzania.
Wafanyabiashara wengine
walioshiriki Kongamano hilo wameonesha nia ya kushiriki maonesho ya 46 ya biashara
ya kimataifa ya Dar es Salaam ambayo yataanza
tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022. Ushiriki huo utawawezesha kukutana na wafanyabiashara
na kuona bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania.
Kupitia kongamano hilo, wazalishaji
wa bidhaa za Ngozi na korosho wa Tanzania wameunganishwa na wafanyabiashara wa
India ambapo watapata fursa ya kuuza bidhaa hizo katika soko la India.
Sambamba na kongamano hilo, Ubalozi pia ulishiriki
katika hafla ya uzinduzi wa ofisi ya uhamasishaji na uratibu wa biashara na uwekezaji inayojulikana kwa jina la INDIA TANZANIA TRADE COMMISSION (ITTC) iliyopo katika jengo laJJ Diamonds Mart No. 85,
Barabara ya Gopathi Narayanas wani Chetty Chennai katika eneo la Thyagaraya Nagar ambalo ni kitovu cha biashara jijini Chennai. Ofisi hiyo itaongozwa na kusimamiwa na Dkt. J. Shrenik Naharkama Kamishna wabiashara wa
ITTC.
Uwepo wa ITTC utasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa
haraka wa taarifa sahihi za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania, kwa kuwa ITTC itakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na taasisi
zinazosimamia masuala ya biashara na uwekezaji za nchini Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe Anisa Mbega akifungua Kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na India Jijini Chennai, India. |
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la biashara na uwekezaji kati ya
Tanzania na India wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa kongamano hilo. |
Balozi
wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega akikata utepe na kuwasha mshumaa kuashiria
uzinduzi rasmi wa ofisi ya uratibu wabiashara na uwekezaji ITTC.
|
| Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe Anisa Mbega akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa masuala ya biashara na uwekezaji kutoka Tanzania na India katika hafla ya uzinduzi rasmi wa ofisi ya uratibu wabiashara na uwekezaji ITTC |
Wednesday, April 13, 2022
KAMATI YA PAMOJA WATAALAM WA MIPAKA TANZANIA NA KENYA YAKAGUA MPAKA
Timu ya Wataalamu wa Mipaka kati ya Tanzania na Kenya imetembelea na kujionea kazi ya uimarishaji mipaka wa Kimataifa wa nchi hizo iliyofanywa kwa lengo la kukagua na kushauri namna bora ya kuendelea na kazi zinazofuta.
Ukaguzi wa mipaka hiyo ulifanyika tarehe 12 April 2022 na ni sehemu ya kikao cha pamoja cha Wataalam wa Mipaka wa nchi hizo kilichoanza juzi kwa ajili ya kupokea mawasilisho ya kazi iliyofanyika sambamba na kutoa muongozo wa namna bora ya kutekeleza kazi iliyobaki.
Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Hamdouny Mansoor akionesha muelekeo wa mpaka kati ya Tanzania na Kenya eneo la Serengeti wakati timu ya wataalam wa mipaka kutoka Kenya na Tanzania ilipotembelea mpaka huo tarehe 12 April 2022. Wa pili kulia ni Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya Balozi Joseph Vungo na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Mipaka ya Kimataifa nchini Kenya (KIBO) Juster Nkoroi.
Wataalam hao wakioongozwa na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Hamdouny Mansoor pamoja na Juster Nkoroi Mtendaji Mkuu Ofisi ya Mipaka ya Kimataifa nchini Kenya (KIBO) walitembelea mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Kirongwe wilayani Rorya kwa upande wa Tanzania na Muhuru Bay katika Kaunti ya Migori nchini Kenya pamoja na ule mpaka wa nchi hizo eneo la Serengeti/Masai Mara ili kukagua kazi ya uwandani.
Timu ya wataalamu wa mipaka kutoka nchi za Tanzania na Kenya tayari imekamilisha uimarishaji mpaka wa kimataifa wa nchi hizo kipande cha Kilomita 83 kutoka hifadhi ya Serengeti/ Masai Mara hadi Ziwa Natron na awamu ya pili ya kipande cha kilomita 110 uimarishaji wake utaendelea baada ya kukamilika kuandaliwa mpango kazi.
Wakati wa ufunguzi wa kikao cha pamoja cha Wataalam wa Mipaka wan chi hizo mbili, Mkuu wa wilaya ya Tarime Kanali Michael Mangwela kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara aliwaambia washiriki kuwa, uimarishaji mipaka ulenge kuimarisha mahusiano pia pamoja na kujadili changamoto za maeneo ya mipakani.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya Balozi Joseph Vungo alishauri wataalamu wanaoshiriki kikao hicho kuhakikisha wanajadili na kuzitolea maamuzi changamoto kwa amani hasa wakizingatia nchi ya Tanzania na Kenya zimekuwa na mahusiano mazuri.
Mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la nchi kavu una ukubwa wa Kilomita 758 na uimarishaji wake utasaidia kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwa zikijotokeza kutoka kwa wananchi wanaofanya shughuli maeneo ya mipakani katika nchi hizo.
KINANA ATETA NA BALOZI WA ZIMBABWE NCHINI TANZANIA
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania Mheshimiwa Lt. Jen. (Mst) Anselem Sanyatwe, (kushoto) leo Aprili 13 ,2022 katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar Es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimsindikiza Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania Mheshimiwa Lt. Jen. (Mst) Anselem Sanyatwe, (katikati) (wa kwanza kushoto) Ndg Ngemela Lubinga Katibu wa Idara ya Siasa Na Uhusiano wa Kimataifa CCM leo katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar Es Salaam.
Monday, April 11, 2022
KINANA AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM-Bara), Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amekutana na Balozi wa Marekani nchini, Donald Wright, jijini Dar es Salaam ambapo wamezungumza mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na nchi ya Marekani.
Akizungumza muda mfupi baada ya balozi huyo kuondoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Aprili 11 2022, Kanali Mstaafu Kinana alisema mazungumzo hayo yalikuwa ya kawaida katika kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na nchi hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Donald J. Wright (kushoto) leo katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar Es Salaam. (Picha na Fahad Siraji)
“Mazungumzo yetu yalikuwa ya kawaida, tumezungumzia namna ya kuimarisha uhusiano pamoja na ustawi wa wananchi,” alisema Kanali Kinana.
Alisema miongoni mwa maeneo waliyoyagusia katika mazungumzo yao ni pamoja na kuimarisha huduma za kijamii ikiwamo afya na utoaji haki kupitia mifumo mbalimbali.
Viongozi hao wamekutana zikiwa siku chache tangu balozi huyo alipokutana na Rais Samia Suluhu Hassan.




.jpg)






.jpeg)
















