Matokeo chanyA+ online




Thursday, July 25, 2019

SHULE YA WATU WENYE ULEMAVU NA MAHITAJI MAALUMU YAJENGWA WILAYANI ARUMERU


Zaidi ya shilingi bilion 2.8 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya secondary ya elimu maalumu katika eneo la chuo cha Patandi kilichopo Tengeru wilaya ya Arumeru mkoani Arusha

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya miundombinu wilayani Arumeru Mkuu wa wilaya hiyo Mh, Jery Muro amesema kuwa fursa hiyo ni ya kwanza hapa nchini ambapo italeta manufaa kwa watu wenye mahitaji maalumu

Amesema kuwa licha ya kusaidia kitaleta kielelezo cha kuhakikisha watoto wenye ulemavu watapewa mtazamo mpya wa elimu kwa kuokoa watoto wenye changamoto na mahitaji maalumu kutoka sehemu mbalimbali 

Aidha ameseama kila mwezi serikali inatoa bilioni 23 kwa wastani kwa ajili ya ujenzi wa elimu na kugharamia sera ya elimu bure hapa nchini 

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya mahitaji maalumu Patandi Mwl. Janeth Molel ameipongeza serikali kwa juhudi kubwa za kuwajali watu wenye mahitaji maalumu hasa kupitia elimu kwani hii itasaidia kupunguza ongezeko la watoto wa mtaani na hatiamye kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda

Amsesema kuwa,kwa sasa yamekamilika madarasa manane 8 na itachukua wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo tayari wameshapata waalimu 5 kwa ajili ya kuanza kutoa elimu hiyo ambayo itakuwa shule ya mfano hapa Tanzania.

Amewataka wazazi kutowaficha watoto wao wenye ulemavu bali watumie fursa iliyojitokeza katika kuhakikisha wanawapatia elimu ambayo itawasaidia katika kujenga msingi mzuri wa maisha

Kwa upande wake mbunge wa Arumereru Mashariki John, Danielson Palanjo amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha elimu inapewa kipaombele hasa kwa watu wenye mahitaji maalumu kwa kuwa nao wana uwezo wa kulitumikia taifa

Amesema huduma ya elimu katika ambayo imeletwa wilayani hapo, italeta manuafaa kwa jamii na kuwa mfano kwa huiduma ambazo kila mtu atazifaidi kwa kuwa itakuwa tegemezi kwa kila mwananchi

Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru Bw. Emanuel Mkongo amesema wao kama halmashauri bwanasubiri kukabidhiwa madarasa na pia watahakikisha kila kitu kimekamilika ili kuweza kuruhusu wanafunzi kuingia madarasani ambapo nao wana mchango mkun=bwa katika kuhakikisha wanaungana na serikali kuendeleza watu wenye mahitaji maalumu 

Hata hivyo shule hiyo itakuwa na uwezo wa kuwa na wanafunzi 120 wenye mahitaji maalumu bila ubaguzi na watapata huduma mabalimbali kulingana na uwezo wao 
Muonekano wa Bwalo la Wanafunzi wenye mahitaji maalumu linalojengwa katika Shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Chuo cha Ualimu Patandi, Arumeru mkoani Arusha
Muonekano wa Jengo la Utawala la Shule ya Wanafunzi wenye mahitaji maalumu inayojengwa katika Chuo cha Ualimu Patandi.
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Wednesday, July 24, 2019

MLOGANZILA WAPATIWA MAFUNZO DHIDI YA MAJANGA YA MOTO

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Peter Mwambene (kushoto) akiwapatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto watumishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, kulia ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Elinimo Shang’a.
Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wamepatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwa lengo la kujikinga na majanga ya moto na kuhakikisha Tanzania inakua salama dhidi ya majanga ya moto.

Watumishi wa Hospitali ya Mloganzila wakifuatilia mafunzo hayo 
Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo ni yanadharia na vitendo yametolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Elinimo Shang’a akielezea majanga ya moto yanavyotokea na namna ya kukabili.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Peter Mwambene amesema moja ya vitu vinavyomfanya mtu ashindwe kupambana na moto ni uoga na kutokua na vifaa sahihi vya kupambana na moto unapokua katika hatua za awali. 

Kamanda Shang’a akifundisha kwa vitendo namna ya kuzima moto kwa kutumia blanket maalum ya kuzimia moto (fire blanket).
Hivyo mafunzo hayo yatawajengea uelewa wa matumizi sahihi ya vifaa vya kuzimia moto, kujua aina mbalimbali za moto na namna ya kukabili, kujua mbinu za kuzima moto pamoja na namna ya kujiokoa pindi moto unapotokea.

Kamanda Shang’a akielekeza namna ya kuzima moto kwa kutumia kizimia moto aina ya poda kavu (dry powder fire extinguisher).
“Moto unapotokea mtu hushindwa kuukabili kutokana na uoga, unatakiwa ufanye yafuatayo pindi unapogundua moto, piga king’ora, kengele au mayowe,ita Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia namba 114, watu wasiojiweza wapewe kipaumbele kutoka eneo hatarishi, jaribu kuzima moto bila kuhatarisha usalama wako na watu wengine’’ amesema Mwambene.

Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mloganzila wakifanya zoezi la kuzima moto mara baada ya kupatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto.
Ametaja vyanzo vikuu vinavyoweza kusababisha majanga ya moto kuwa ni matumizi ya vifaa vya umeme visivyokua na ubora, ajali, nguvu asilia (radi, upepo,mkali, tetemeko la ardhi , milipuko ya Volkano).

Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mloganzila wakifanya zoezi la kuzima moto mara baada ya kupatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto.

Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mloganzila wakifanya zoezi la kuzima moto mara baada ya kupatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto.







Tuesday, July 23, 2019

WAZIRI MKUU AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 35 WA JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA (ALAT)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasikiliza watumishi wa Benki ya CRDB, wakati akikagua mabanda, katika mkutano mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), uliyofanyika katika ukumbi wa Malaika, jijini Mwanza, alipomwakimwakilisha Rais Magufuli katika mkutano huo, Julai 23.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Meneja wa Mahusiano ya Serikali Benki ya NBC, William Kallaghe, wakati akikagua mabanda, katika mkutano mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), uliyofanyika katika ukumbi wa Malaika, jijini Mwanza, alipomwakimwakilisha Rais Magufuli katika mkutano huo, Julai 23.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo, Wakati na Kilimo wa Benki ya NMB, wakati akikagua mabanda, katika mkutano mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), uliyofanyika katika ukumbi wa Malaika, jijini Mwanza, alipomwakimwakilisha Rais Magufuli katika mkutano huo, Julai 23.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na watumishi wa Benki ya NMB, wakati akikagua mabanda, katika mkutano mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), uliyofanyika katika ukumbi wa Malaika, jijini Mwanza, alipomwakimwakilisha Rais Magufuli katika mkutano huo, Julai 23.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), katika mkutano mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), uliyofanyika katika ukumbi wa Malaika, jijini Mwanza, Waziri Mkuu amemwakimwakilisha Rais Magufuli katika mkutano huo, Julai 23.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Monday, July 22, 2019

SERIKALI KUWAJENGEA UWEZO MAKANDARASI WADOGO

Serikali imesema itawajengea uwezo makandarasi wadogo wanaotumia teknolojia ya nguvukazi (Labor Based Technology) katika ujenzi na ukarabati  wa matengenezo ya barabara, madaraja na majengo ili kuhakikisha kuwa wanapata fursa zaidi za kushiriki na kushindana katika kazi zilizotengwa mahsusi kwa ajili makandarasi hao.

Hayo yalibainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, kwenye kongamano la uhamasishaji na uanzishwaji wa umoja  wa makandarasi na vikundi vinavyotumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi katika ujenzi, ukarabati wa matengenezo ya barabara uliofanyika mkoani Mbeya katika Chuo cha Teknolojia Stahiki ya Nguvu Kazi (ATTI) na kuhudhuriwa na wakandarasi wadogo wadogo zaidi ya 150.

Arch. Mwakalinga, alisema kuwa Wizara kupitia taasisi zake zinazotekeleza miradi ya ujenzi itaendelea kutumia sheria na kanuni zilizowekwa ili kuhakikisha kazi zilizoainishwa kwenye miradi ya ujenzi ikiwemo ukarabati  na matengenezo ya barabara, madaraja na majengo zinafanywa na makandarasi  hao.

"Wizara imeteua timu ya wataalam kupitia nyaraka mbalimbali za miradi ya ujenzi ili kuhakikisha asilimia 30 ya fedha zinazolipwa kwenye mikataba mbalimbali ya ujenzi zinaelekezwa kwa makandarasi wanaotumia teknolojia ya nguvu kazi", alisema Mwakalinga. 

Aliongeza kuwa upitiaji utafanyika kwa haraka chini ya wataalam hao ambapo anaamini watafanya kazi hiyo vizuri ili kubainisha vigezo ambavyo makandarasi hao wamekuwa wakivilalamikia kila siku katika utekelezaji wa kazi zao ili vifanyiwe kazi.

Aidha Arch. Mwakalinga, alibainisha kuwa Serikali inatambua makandarasi hao ni chachu kubwa katika kutatua tatizo la ajira kwa wananchi hususani maeneo ya vijijini kwani mara nyingi wakandarasi hao hutumia vifaa na vibarua wanaopatikana katika eneo la mradi. 

"Mbali na kuongeza ajira na kuimarisha usafiri hususani maeneo ya vijijini, serikali inaelewa fika mnachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi kwa kodi mnayolipa kupitia kazi mnazozifanya" alisisitiza Mwakalinga.

Alisema ni jukumu la wakandarasi hao kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na kuwa na sauti moja katika kufuatilia fursa mbalimbali na maslahi yao na kupata ufumbuzi wa pamoja wa changamoto zinazowakabili. 

Awali akimkaribisha Katibu Mkuu huyo Mkurugenzi wa Barabara, Mhandisi Rogatius Mativila, alisema madhumuni ya kikao kazi hicho ni kujadili kwa pamoja masuala muhimu katika Sekta ya Ujenzi ili kuendeleza na kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Nguvukazi katika kutekeleza matengenezo ya barabara, madaraja na majengo bila kusahau sekta nyingine nchini. 

Akiongea kwa niaba ya makandarasi hao, Bi Aurelia Mtui, alitoa shukrani za dhati kwa Serikali kwani amekuwa kwenye taaluma hiyo kwa miaka 18 na kwa mara ya kwanza wamekutana na Katibu Mkuu  wa Sekta ya Ujenzi kuzungumzia changamoto zao na kuomba maazimio waliyokubaliana katika kikao hicho yafanyiwe kazi. 

Serikali ilianzisha mpango wa kuendeleza matumizi ya teknolojia ya Nguvukazi tangu mwaka 2004 na kulingana na takwimu zilizopo hadi kufikia mwezi Juni 2019 jumla ya Makandarasi 267 walikuwa wamesajiliwa na bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) katika madaraja ya kutumia teknolojia ya nguvukazi.
1
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akifungua kongamano la uhamasishaji na uanzishwaji wa umoja  wa makandarasi na vikundi vinavyotumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi katika ujenzi, ukarabati wa matengenezo ya barabara lililofanyika katika Chuo cha Teknolojia Stahiki ya Nguvu Kazi (ATTI) mkoani Mbeya.
2
 Mshiriki wa kikao kazi cha Makandarasi wanaotumia teknolojia stahiki ya nguvukazi katika ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara, Bw. Ambakisye Mwakipesile, akiwasilisha hoja zake kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch.Elius Mwakalinga (hayupo pichani) katika kongamano lililofanyika katika Chuo cha ATTI Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya na kushirikisha wakandarasi hao kutoka nchi nzima.
3
 Mkandarasi Boniface Mambya, akitoa maoni yake kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch.Elius Mwakalinga (hayupo pichani) wakati wa kongamano la umoja kwa makandarasi na vikundi vinavyotumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi katika Ujenzi ukarabati wa Matengezo ya barabara lililofanyika katika chuo ATTI, Mkoani Mbeya.
4a
4b
Washiriki wa kongamano la uhamasishwaji wa uanzishwaji wa umoja wa makandarasi na Vikundi vinavyotumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi katika ujenzi, ukarabati wa matengezo ya barabara wakipitia baadhi ya makabrasha na kumsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch.Elius Mwakalinga (hayupo pichani) lililofanyika katika Chuo cha ATTI, Mkoani Mbeya.

WAZIRI MKUU: TUMIENI FURSA ZA UTALII KUBORESHA MAISHA YENU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Bashay, wilayani Karatu watumie fursa zinazojitokeza kwenye sekta ya utalii kuboresha maisha yao.

“Tumieni fursa ya uwepo wa eneo hili. Halmashauri wakishajenga vizimba vya biashara, leteni bidhaa zenu kama vile picha za tingatinga, mapambo, vinyago na vyakula vya asili ili watalii wakija hapa wapate huduma kutoka kwenu,” alisema.

PMO_3490
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo, wakati alipofungua kituo cha huduma za utalii, katika Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha, Julai 21, 2019.
 
Ametoa wito huo jana jioni (Jumapili, Julai 21, 2019) wakati akizindua mradi wa ujenzi wa vituo vya polisi vya kupunguza changamoto kwa magari ya utalii barabarani na kukabidhi gari la polisi kwa ajili ya patrol ya watalii katika eneo la Bashay, wilayani Karatu, mkoani Arusha.


Waziri Mkuu alizindua kituo cha kutolea huduma za usalama kwa watalii wilayani Karatu ikiwa ni ishara ya kuwakilisha vituo vingine vitatu vinavyoendelea kujengwa mkoani Arusha katika maeneo ya Kikatiti (Arumeru), Makuyuni (Monduli) na Engikaret (Longido). 

PMO_3498
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua kituo cha huduma za utalii, kilichopo katika Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha kabla ya kukifungua rasmi, Julai 21.2019.
 
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasihi wakazi hao wawalinde watalii ili waitangaze vema nchi ya Tanzania pindi wakirudi makwao. “Ili kukuza na kutangaza utalii, tunapaswa tuwe na mapenzi mema kwa watalii lakini kikubwa zaidi ni usalama wao.” 

Aliwataka wakazi hao waendelee kuiamini Serikali ya awamu ya tano na waendelee kumuombea Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili apate nguvu ya kuleta maendeleo zaidi. 

PMO_3502
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia kituo kidogo cha Polisi kilichopo katika kituo cha huduma za utalii, wilayani Karatu, kabla ya kukifungua rasmi, Julai 21.2019.
 
Pia aliwashukuru viongozi wa Tanzania Association of Tour Operators (TATO) kwa kuchangia ujenzi wa vituo hivyo na kutoa gari jipya la polisi kwa ajili kituo hicho cha Karatu. Gari hilo aina ya Toyota Landcruiser lililogharimu dola za Marekani 45,000, limepewa namba za usajili za PT 4190. 

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wakazi wa Bashay waliohudhuria hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo alisema ujenzi wa vituo hivyo umetokana na malalamiko aliyopokea kwamba watalii wakitoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) hadi kufika Karatu wanakuwa wamesimamishwa njiani zaidi ya mara 20. 
 
PMO_3512
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipewa maelezo na Mrakibu wa Polisi Joseph Bukombe, ndani ya kituo kidogo cha Polisi, kilichopo katika kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019. Tokea kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
 
“Tulijiuliza hawa watalii wamekuja kutalii, wanataka kupumzika, sasa ni kwa nini wasumbuliwe kiasi hicho? Tuliamua kuanzisha vituo vya aina hii, ili watalii wafanyiwe ukaguzi kwenye check-points maalum,” alisema. 

Aliomba Jeshi la Polisi liwapange barabarani askari ambao ni weledi na wana uelewa wa masuala ya utalii na kutolea mfano wa wiki iliyopita ambapo alikuwa akitokea mjini kwenda Karatu na kukuta magari ya watalii zaidi ya 10 yamesimamishwa njiani. 

PMO_3527
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua gari jipya la Polisi, lililokabidhiwa kwa ajili ya kuwahudumia watalii, kwenye kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019.
 
“Niliona baadhi yao wakiwa wamelala kwenye magari kwa uchovu, nilipowauliza wamekalishwa kwa muda gani, walisema ni kwa zaidi ya dakika 45. Nilipomuuliza askari aliyewasimamisha ni kwa nini anafanya hivyo, akanijibu kwamba dereva amemjibu vibaya. Hivi ni kwa nini watalii wateseke juani wakati mwenye makosa ni dreva?” 
 
PMO_3556
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikabidhi gari jipya la Polisi, litakalotumika kwa ajili ya kuhudumia watalii, kwa Kaimu RPC Mkoa wa Arusha James Manyara, kwenye kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019.
 
Naye, Makamu Mwenyekiti wa TATO, Bw. Henry Kimaro aliishukuru Serikali kwa jitihada inazofanya za kupambana na ujangili na kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini. “Tumeona hivi karibuni watalii wengine kutoka Israel, China na sasa ndege yetu imeanza kwenda India kuwafuata hukohuko,” alisema. 
 
PMO_3563
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
 
Alisema wameanza na vituo hivyo vinne mkoani Arusha lakini tatizo hilo liko maeneo mengi nchini na wao hawawezi kufika nchi nzima kutoa huduma kama hiyo. Hivyo, alimuomba Waziri Mkuu awahimize Wakuu wa Wilaya ambao wilaya zao zinajihusisha na sekta ya utalii, waige mfano wa wilaya ya Karatu ili kuhakikisha usalama wa watalii wawapo nchini. 
 
PMO_3568
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe kuzindua rasmi  kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019.
PMO_3580
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kuzindua rasmi  kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019.
PMO_3591
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Mke wa Bwana Joseph Erro, Bibi Evalina Madawe, ambaye amejitolea kiwanja kilichotumika kujengea kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. Kulia ni mtoto wa bwana Francis Theodosia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
PMO_3619

SHUBILA STATON ANYAKUA TAJI LA MISS MOROGORO 2019

 Miss Morogoro 2019 Shubila Staton akipungia mkono wageni waalikwa walifika katika shindano la kumsaka mlimbwende wa mjini kasoro bahari Morogoro mara baada ya kutangazwa.
  Miss Morogoro 2019 Shubila Staton atoa machozi ya furaha baada ya kutangazwa kubeba taji hilo. Pembeni yake kulia ni Meya wa Manispaa ya Morogoro Paschal Kihanga, Miss Morogoro namba mbili Moureen Kaaya na kulia ni muandaaji wa mashindano hayo Farida Fujo.
Wadhamini wa shindano hili, DSTV wakitoa zawadi kwa washindi wa tatu wa Miss Morogoro 2019.
Muandaaji wa Miss Morogoro 2019 Farida Fujo akitoa neno la nasaha kwa washiriki na shukrani kwa wageni waliofika katika shindano hilo lililofanyika mjini Morogoro July 20, 2019.
Mbunifu wa Mavazi Martin Kadinda (picha ya juu kulia) akitangaza mshindi. Picha ya chini ni warembo Moureen Kaaya aliyenyakuwa nafasi ya pili akiwa ameshikana mikono na Shubila wakati wakingoja kutangazwa kwa mshindi.
Muandaaji wa Miss Morogoro 2019 Farida Fujo akiwa na msemaji wa timu ya Simba Haji Manara ambaye nae aliungana katika hafla hiyo.
 
Muandaaji wa Miss Morogoro 2019 Farida Fujo (katikati) akiwa na Msimamizi wa Mshindano hayo Martini Kadinda (kulia) na kushoto ni Msanii wa bongo movie Irene Uwoya.
Wasimamizi wa shindano la Miss Morogoro 2019 wakiwa katika picha ya pamoja.
Msanii Christian Bella akitoa burudani. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro. 

Mbio za kumtafuta Miss Morogoro 2019 zimefikia tamati alfajili ya leo ambapo mrembo Shubila Staton ameibuka kidedea kwa kuwaangusha warembo wenzake 12 na kupata nafasi ya kuwakilisha mkoa wa Morogoro katika mashindano ya Miss Tanzania. Akimtangaza mshindi huyo msimamizi wa mashindano hayo Mbunifu wa Mavazi Martin Kadinda alianza kwa kutangaza walioingia sita bora na baade tatu kumalizia mshindi. 

 Katika shindano hilo warembo hao walipanda jukwaani na kuonyesha mavazi ya aina mbalimbali ikiwemo vazi la Ubunifu, vazi la jioni, navazi la ufukweni ambapo mlimbende Shubila Staton kushika nafasi ya kwanza huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Moureen Kaaya na nafasi ya tatu ameshinda Veronica Royal. 

Akitoa neno mgeni rasmi Meya wa Manispaa ya Morogoro Paschal Kihanga amewashukuru waandaaji wa shindano hilo kwa kulifanya la wazi na haki na linaloletea heshima katika mkoa. "Binafsi nimefurahishwa na waandaaji kwa kuendelea kuuletea heshima mkoa wetu kwa mwaka wa pili mfululizo," amesema. 

Kwa upande wake muandaaji wa Miss Morogoro 2019 Farida Fujo amewashukuru wakazi wa Morogoro kwa kuendelea kuwaamini kwa miaka miwili mfululizo jambo linalowapa heshima ya pekee. Mashindano yaliyoandaliwa na Nyumbani Park ambao ni wamiliki wa kiwanja cha burudani cha Samaki Spot kilichopo mjini Morogoro yalikuwa na ushindani mkubwa kwa vile yalikuwa na warembo wenye viwango. 

Ni usiku ulipambwa na burudani za aina yake kutoka kwa wasanii Barnaba, Christian Bella na watu mashughuli nchini akiwemo Irene Uwoya, mama Dangote, Ndama mtoto wa ng'ombe, msanii Steve Nyerere huku shauku kubwa ya mashabiki wa sekta ya urembo mkoani Morogoro ni kushudia nani anatwaa taji la miss Morogoro mwaka 2019 kati ya walimbwende 12 walioshiriki shindano hilo.