Matokeo chanyA+ online




Thursday, August 27, 2020

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR, DK. SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA ZANZIBAR

 


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar, kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,leo Augost 27 mwaka 2020, ameongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar. 

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui Zanzibar kuanzia Majira ya Saa 9:00 Asubuhi. 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, mara baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kwa ajili ya Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.
 
Pamoja na mambo mengine Kikao kitapokea na kujadili Taarifa ya mapendekezo ya Wana CCM walioomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, kutoka katika Majimbo na nafasi ya Uwakilishi Viti Maalum vya Wanawake katika Mikoa ya Zanzibar.
 
Kikao hicho ni maalum kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977 Toleo la 2017,Ibara ya 108 na 109  (1), (7). 

Aidha Chama Cha Mapinduzi kinaeleza kuwa Kikao hicho ni miongoni mwa Vikao Vyake vya Uongozi vya Kitaifa vinavyofanyika kwa Mujibu wa Kanuni na Miongozo ya CCM.

AMSHA AMSHA YA UHURU FM KUELEKEA DODOMA, YAKUTANA NA MGOMBEA UBUNGE WA CHALINZE

 


 Mgombea Ubunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete (njano) akizungumza jambo na Kikosi kazi cha Amsha Amsha ya Uhuru FM maeneo ya Chalinze wakati kikielekea jijini Dodoma leo.

Na Pius Ntiga-Chalinze

Mgombea Ubunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete ametaja mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika Jimbo Hilo kwa kuainisha mafanikio hayo ikiwemo kuanzisha kwa viwanda vikubwa vitatu.

Katika mahojiano na Uhuru FM kupitia kampeni yake ya AMSHA AMSHA Dodoma ikiwlekea mikakati mikubwa ya maendeleo, Ridhiwani amesema kuptia viwanda hivyo kumeleta tija ya kupatikana kwa ajira kwa zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wakiwemo vijana wa chalinze ambao nao wamefurahia upatikanaji wa ajira hizo.

Kuhusu matibabu zaidi ya asilimia 40 ya wazee wamepatiwa vitambulisho vya bima ya Afya AMBAYO vinawasaidia katika kupata matibabu kuptia Hospitali ya kisasa iliyopo katika Jimbo la chalinze na maeneo mengine.

Mwaka 2015 amesema kulikuwa na changamoto ya vifo kwa Akina mama vinavyotokana na uzazi ambapo sasa ndani ya miaka mitano chini ya serikali ya awamu ya tano Hali hiyo haipo Tena  kwani Kuna kituo kitubwa Cha afya kipo miono na lugoba ambapo sasa Kuna asilimia 3 tu ndio inayotoka na vifo vya Akina mama wajawazito.

Kutokana na mafanikio hayo AMBAYO pia yamejielekeza katika sekta ya Afya na utalii Ridhiwani amewaomba wananchi wa chalinze kumchagua ili aendeleze mafanikio makubwa yaliyopatikana na.kuhakikisha aliyopatikana maendeleo yanaendelea,Pia amewaomba wananchi wamchague Rais John Magufuli kwa kumpigia Kura za ndio katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

KATIBU MKUU KUSAYA ABAINI KIWANDA CHA MBOLEA KISICHO NA USAJILI WA UBORA

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akiwa ameshika chupa ya mbolea inayozalishwa na kiwanda cha Isacha Feeder cha Moshi leo alipokagua .Katika ziara hiyo alibaini kuwa kiwanda hicho kinazalisha mbolea ya maji aina ya Booster II ambayo haijasajiliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na  ameagiza mmiliki wa kiwanda hicho aende Dodoma ifikiapo 03 Septemba kujieleza kwanini anaendesha kiwanda bila usajili.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya( kulia) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) Dkt.Stephano Ngailo wa kwanza kushoto alipobaini mbolea ya maji isiyo uthibitisho wa ubora toka TBS .Wa kwanza kushoto ni Msimamizi wa kiwanda cha Isacha Feeder -Njoro chaMoshi  Rajab Issa Juma kinachozalisha mbolea hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ( kulia) akikagua mgodi wa chokaa (limestone rock)  leo alipotembelea kiwanda cha mbolea cha ABM Jijini Tanga.Kushoto ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Aubray Maimu.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya (kulia) akiangalia eneo panapochimbwa chokaa kilimo katika kiwanda cha mbolea cha ABM Tanga. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania Bw.Saad Kambona.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akiwa anatazama jiwe la chokaa linalotumika kuzalisha mbolea katika kiwanda cha ABM Tanga leo alipotembelea kukagua utendaji kazi wake na kuhamasisha kuongeza uzalishaji ili wakulima wapate mbolea kwa gharama nafuu.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ( wa tatu toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Bodi ya Mkonge Tanzania na wanahabari mara baada ya kutembelea bodi hiyo leo jijini Tanga kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya  Waziri Mkuu.
(Picha na habari na Wizara ya Kilimo)

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amesikitishwa na kitendo cha kiwanda cha mbolea za maji cha Isacha Feeders Intertrade cha Moshi mkoani Kilimanjaro kuzalisha bidhaa za mbolea ambazo hazisajiliwa na kuthibitishwa ubora wake kwa wakulima.  
 
Akiwa katika ziara ya kukagua viwanda vya mbolea nchini leo  Katibu Mkuu huyo alijionea bidhaa za mbolea ya maji iitwayo “Booster II” ikiwa katika ghala la kiwanda cha Isacha Feeder –Njoro Manispaa ya Moshi na kubaini kuwa haijasajiliwa na mamlaka za uthibiti ubora nchini.  
 
“Sijafurahishwa na utendaji kazi wa kiwanda hiki cha mbolea cha Isacha Feeders kuona mbolea inayozalishwa haijasajiliwa na Shirika la Viwango (TBS ) pia haina Barcode hali inayohatarisha mazao ya wakulima na afya za walaji” alisema Kusaya. 
 
Taarifa ya kiwanda hicho cha mbolea ya maji imeonyesha kilianzishwa mwaka 2016 kikizalisha mbolea ya maji ambazo zinauzwa kwenye maduka mbalimbali nchini bila kuwa na usajili wa ubora toka TBS. 
 
 Kufuatia hali hiyo, Katibu Mkuu Kusaya ameagiza wamiliki wa kiwanda hicho kwenda ofisini kwake Dodoma ifikapo tarehe 03 Septemba 2020 ili kujieleza kwanini serikali isichukue hatua za kukifunga kiwanda hicho hadi wakamilishe taratibu za usajili ili kulinda wakulima na uharibifu unaoweza kujitokeza endapo mbolea hiyo ikikosa ubora. 
 
“Ninyi mnazalisha mbolea na kuipeleka kwa wakulima wangu sasa ikitokea mazao ya wakulima yameharibika na mbolea hii isiyo na uthibitisho wa ubora nani atalipia gharama hizo?” alihoji Katibu Mkuu Kusaya Kufuatia hali hiyo Kusaya alitoa maagizo matano kwanza, mmiliki wa kiwanda hicho cha Isacha kuwasilisha taarifa inayoonyesha tangu mwaka 2016 wamezalisha kiasi gani cha mbolea na wameuza wapi, pili wawasilishe uthibitisho wa cheti cha kuendesha kiwanda toka BRELA na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). 
 
Agizo la tatu mmiliki wa kiwanda mbolea cha Isacha aeleze kwanini kiwanda hakina bango la utambulisho na hakijulikani na uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro mahala kilipo na nne kiwanda hicho kiwasilishe taarifa ya ulipaji kodi serikalini tangu kilipoanza kazi mwaka 2016 hadi sasa. 
 
“Mkija Dodoma nataka mje na taarifa kamili kuhusu uhalali wa kiwanda hiki kuwa na sifa za kuzalisha mbolea inayokwenda kutumika na wakulima ili kuishawishi serikali kuwa mnastahili kuendelea ka kazi ” alisisitiza Kusaya. 
 
 Kusaya alisema akirejea Dodoma atawaalika Wizara ya Viwanda na Biashara, Mamlaka ya Mapato (TRA) Shirika la Viwango (TBS), BRELA na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) wajadili hatua za kuchukua dhidi ya viwanda ambavyo vinakiuka taratibu za uzalishaji mbolea nchini.
 
  Naye Msimamizi wa kiwanda hicho cha Isacha Feeder -Njoro, Rajab Issa Juma alisema kiwanda hicho kinazalisha lita 17,000 za mbolea ya maji (Booster II: Foliar Fertilizer for Use in all Crops) kwa mwaka ambapo lita moja huuzwa kwa bei ya shilingi 2,000 kwa wakulima.  
 
Awali Katibu Mkuu huyo alitembelea kiwanda cha mbolea ABM cha Tanga kuona hali ya uzalishaji na kukuta kiwanda hicho kikizalisha chokaa kilimo chini ya uwezo wake kutokana na changamoto ya mtaji.  
 
Akizungumza na waandishi wa habari kiwandani hapo Mkurugenzi wa kiwanda hicho Aubray Maimu alisema wanazalisha tani 5,000 za chokaa kilimo (limestone) kati ya lengo la tani 10,005 kufikia mwaka 2021. “Mgodi wetu wa Zange Mkulumuzi hapa Kange Tanga una mawe ya chokaa zaidi ya tani milioni 25 inayotesheleza uzalishaji wa mbolea ya chokaa kwa wakulima” alisema Maimu. 
 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt. Stephano Ngailo amesema mahitaji ya mbolea nchini ni tani 664,000 wakati uzalishaji katika viwanda vyote 12 umefikia tani 38,000 pekee kwa mwaka. Katibu Mkuu Kusaya yuko katika ziara ya kukagua na kujionea hali ilivyo kwenye viwanda vya mbolea nchini ambapo tayari ametembelea kiwanda cha Mbolea za Asili cha Guavay cha Dar es Salaam ambapo anatarajia kutembelea pia mikoa ya Arusha na Manyara Lengo la ziara hii ni kuhamasisha wawekezaji wa ndani ya nchi na nje kuanzisha viwanda vya mbolea ili wakulima wapate kwa gharama nafuu na karibu na mashamba yao badala ya kutegemea mbolea toka nje.

TANROADS YAPEWA SIKU TATU KUKAMILISHA BARABARA


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga (WaKwanza kulia), akikagua barabara ya Rusumo- Lusahunga (KM 92), mkoani Kagera, alipofika mkoani humo kuangalia maendeleo yake. 
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Masiliano, anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga, ametoa siku Tatu kwa Uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Kagera kuhakikisha wanakamilisha ukarabati wa barabara ya Rusumo - Lusahunga (KM 92) ambayo imekuwa kero kubwa kwa wasafirishaji wa mizigo ya ndani na nje ya nchi.


Akizungumza wakati wa ukagauzi wa barabara hiyo, mkoani Kagera, Mwakalinga, amemtaka Kaimu Meneja wa Mkoa huyo na wasaidizi wake kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana kuanzia leo ili kuruhusu magari ambayo yameshindwa kupita kuendelea na safari zake kutokana na ubovu wa barabara hiyo.
 

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Kagera, Mhandisi Jackson Lwerengera, alipofika mkoani humo kukagua barabara ya Rusumo- Lusahunga (KM 92) ili kujionea maendeleo yake.
 
“Nadhani Meneja umenielewa, nataka ndani ya siku Tatu kama ulivyoahidi barabara hii iwe inapitika, na hakikisheni mnafanya kazi usiku na mchana kuanzia leo ili mkamilishe kazi hii”, amesema Mwakalinga.
 
 
Aidha, Mwakalinga ameongeza kuwa barabara hiyo inatakiwa kuwa yenye viwango bora kutokana na umuhimu wake katika uchumi wa nchi, na hivyo kumuelekeza Mkurugenzi wa barabara wa Sekta hiyo Mhandisi Hussein Mativila, kuhakikisha wanatazama kwa jicho la pekee na kuzipa kipaumbele barabara zote ambazo zinaunganisha nchi yetu na nchi jirani.
 
 Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Kagera, Mhandisi Jackson Lwerengera, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga (Kulia), alipofika mkoani humo kukagua barabara ya Rusumo- Lusahunga (KM 92) ili kujionea maendeleo yake.
 
Mwakalinga, amefafanua kuwa barabara hiyo imetengewa kiasi cha shilingi Bilioni 12.5 ambazo ni kwa ajili ya kuwekewa lami ambapo kwa kuanza ameelekeza utekelezaji wa fedha hizo uanze kwa kurekebisha vipande vilivyoharibika sana.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa (TANROADS) Mkoa wa Kagera, Mhandisi Jackson Lwerengera, amemhakikishia Katibu Mkuu huyo kukamilisha ukarabati wa barabara hiyo ndani ya siku alizowaagiza.

Amesema kuwa TANROADS Mkoa huo ulitekeleza kazi za dharura chini ya matengenezo ya muda maalumu katika barabara hiyo ambapo kilometa 6.7 kwa sehemu ya Kwanza na Kilometa 7.1 za sehemu ya pili zimekamilika.
 
 Ukarabati wa barabara ya Rusumo- Lusahunga (KM 92) ukiendelea ambapo unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Magari ya mizigo yakipita katika moja ya vipande vinavyokarabatiwa katika  barabara ya Rusumo- Lusahunga (KM 92) ambapo ukarabati wake unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
PICHA NA WUUM
Mhandisi Lwerengera, ameeleza baadhi ya changamoto kuwa barabara hiyo kuchelewa kufanyiwa matengenezo makubwa kutokana na ongezeko kubwa la magari ambalo linahitaji tabaka la zege ya lami badala ya lami nyepesi ambayo ndiyo iliyopo na inayotumika kwa marekebisho ya sasa.

Barabara hiyo ambayo ina historia ya miaka 35 tangu ilipojengwa imekuwa ni kiungo kikubwa katika masuala ya kiuchumi kati ya nchi yetu na nchi jirani za Rwanda, Burundi na Congo (DRC) kutokana na wafanya biashara wengi kutumia barabara hiyo kusafirisha mizigo yao.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

TUJIKUMBUSHE KAMPENI ZA MAGUFULI 2015: DK MAGUFULI ATANGAZA KIAMA CHA MAJAMBAZI, WEZI NA MAFISADI KATIKA KAMPENI SUMBAWANGA,TUNDUMA, ILEJE NA MBOZI

ALIYOAHIDI AMETEKELEZA on 

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni alipokuwa akijinadi kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma, wilayani Momba, Mkoa wa Songwe. Magufuli alisema kuwa endapo akishinda urais atahakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Kidato cha Nne wanasoma bila kulipa ada yaani bure. Pia alisema barabara inayoingia mpakani kutoka Mbozi itajengwa njia nne tena kwa kiwango cha lami ili kupunguza msongamano wa magari yanayovuka kwenda Zambia.


 

Dk. Magufuli amesema kuwa akiingia madarakani atahakikisha wezi, majambazi na mafisadi wanaswekwa gerezani. Pia anataka Jeshi la Polisi lenye nidhamu na lenye uwezo wa kupambana na wahalifu wakiwemo majambazi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

 Dk. Magufuli akihutubia huku akishangiliwa na mwanachama wa CCM aliyeshika kadi ya uanachama katika Kijiji cha Ndalambo wilayani Momba ambapo alisimama kwa muda akitokea Sumbawanga mkoani Rukwa akienda Tunduma wilayani Momba kuhutubia mkutano wa hadhara
 Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ta Taifa ya CCM, William Lukuvi akielezea wasifu wa Mgombea urais wa Tanzania Dk. John Magufuli katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Lahela, Sumbawanga Vijijini
Dk. Magufuli akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya LAHELA, Sumbawanga Vijijini
Wananchi wa Kata ya Lahela wakishangilia alipokuwa akihutubia Dk. Magufuli ambapo aliahidi mambo mbalimbali likwemo kutatua tatizo sugu la upatikanaji wa dawa za hospitalini.
Dk. Magufuli akisalimiana na wagombea udiwani kupitia CCM katika Kata mbalimbali za Jimbo la Sumbawanga Vijijini.
Msafara wa Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli ukiingia katika Kijiji cha Nzoka wilayani Momba, ukitokea Sumbawanga Vijijini, Mkoa wa Rukwa.
Dk. Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Ni furaha iliyoje kumuona Dk Magufuli
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Nzoka wakisikiliza  kwa makini hotuba ya Dk. Magufuli

Dk. Magufuli akimtambulisha mgombea ubunge, Dk. Lucas Siame

Wananchi wa Kijiji cha Lwasha wakimshangilia Dk. Magufuli alipozungumza nao aliposimamishwa na wananchi akitokea Sumbawanga mkoani Rukwa.
Wazee wa Kijiji cha Ndalambo wakienda kwenye mkutano wa kampeni uliokuwa ukihutubiwa na mgombea na mgombea urais kupitia CCM, Dk. Magufuli.
Ni furaha iliyoje kwa wakazi wa Kijiji cha Ndalambo kumuona Dk. Magufuli.
Wafuasi wa Chadema wakimshangilia mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli alipowasili katika Kijiji cha Ndalambo.
Wananchi wakimshangilia na kuahidi kumpigia kura za ndio, Dk Magufuli
Waendesha Bodaboda wakimlaki Dk Magufuli

Mambo yalivyokuwa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma, mkoani Songwe

Wananchi wakiahidi kumpigia kura za ndiyo mjini Tunduma

Waendesha Bodaboda wakimlaki Dk. Magufuli
Wananchi wakiwa na hamu ya kumuona Dk. Magufuli
Wananchi wakimkubali Dk Magufuli
Dk Magufuli akimnadi Mbunge mtarajiwa Janeth Mbene
Dk Magufuli akizungumza na mgombea ubunge Jimbo la Ileje pamoja na madiwani
Dk. Magufuli akipiga picha na Lukuvi pamoja Waziri wa Adhi wa zamani, Gideon Cheyo.
Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akiwasili Vwawa kuhutubia

Tuesday, August 25, 2020

RPC MKOA WA SINGIDA AFANYA MKUTANO NA VIONGOZI WA DINI KUZUNGUMZIA UCHAGUZI MKUU


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida,  Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Sweetbert Njewike, akizungumza na viongozi wa dini na wadau wengine (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa  Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Veta mkoani hapa jana.
Baadhi ya viongozi wa dini waliokuwepo kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.


Mkuu wa Polisi Wilaya ya Singida, Florence Mwenda akiwa kwenye kikao hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida,  Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Sweetbert Njewike, akisisitiza jambo kwa waandishi wahabari.
Viongozi wa dini wakichukua taarifa hiyo.



 Kikao kikiendelea.

 Boniphace Jilili na Dotto Mwaibale, Singida.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida,  Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Sweetbet Njewike ametoa rai kwa wananchi wa mkoa huo kujiepusha na makundi yanayolenga kuleta uvunjifu wa amani katika kipindi cha uchaguzi.

Kamanda Njewike alitoa rai hiyo jana alipokutana na viongozi wa dini mkoani hapa na wadau wengine katika makundi mbalimbali kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi wa  Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Veta.

Aliyataka makundi mbalimbali yakiwemo ya Vijana kutojiingiza kwenye makundi yanayolenga kuleta uvunjifu wa amani katika kipindi cha kampeni,wakati wa zoezi la kupiga kura na matokeo kwani jeshi la polisi limejipanga sawasawa.

"Askari watakuwepo kwenye maeneo yote kunakofanyika kampeni na kila kituo cha kupigia kura na sio kwamba watakuwepo kutisha wananchi hapana ni kuhakikisha wanalinda amani na usalama wa wananchi." alisema kamanda.

Njewike alisema maendeleo ambayo yapo mkoani hapa yanatokana na amani iliopo, hivyo amewaomba Viongozi wa dini kuwahimiza waumini wao kuzingatia sheria na taratibu wasije wakajikuta wako mikononi mwa vyombo vya sheria.

"Mkiwahimiza na kuwafundisha waumini wenu kuacha dhambi wakiacha watakuwa wametii sheria za nchi." alisema Njewike.

Aidha aliwasisitiza viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na ambayo yamekwisha tolewa na tume ya uchaguzi ikiwemo muda wa kuanza na kumaliza kampeni.

Nao wadau na Viongozi wa dini walipongeza hatua hiyo huku wengine wakiomba maelekezo hayo yatolewe na maaskari kwenye makanisa na misikitini licha ya kuwepo wawakilishi ambao ni viongozi hao.

Kwa upande wake Sheikh Issa Nassoro alisema anaamini kiongozi wa dini akimfundisha kwa unyenyekevu mtu akiwemo mwanasiasa ukiukwaji wa sheria hautakuwepo.

"Wapo wanasiasa ambao dhamira zao ni kuwasaidia wananchi lakini pia tufahamu wapo ambao wanatumiwa na watu/nchi kuleta machafuko,ni wajibu wetu sisi viongozi kuwakemea watu wa namna hiyo." alisema sheikh Nassoro.

Wengine waliwataka wanasiasa na wananchi kufahamu kuwa kuna maisha baada ya kupita uchaguzi, hivyo wasije wakakatisha maisha yao kwa jambo ambalo ni la mda mfupi,huku wakiwaomba wanasiasa kuwa wastaarabu wanaponadi sera za vyama vyao ili kuepuka uvunjifu wa amani.