Matokeo chanyA+ online




Tuesday, July 20, 2021

WAZIRI MKUU MGENI RASMI MAONESHO YA MADINI SHINYANGA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo.

Na Marco Maduhu, Shinyanga

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, ana tarajiwa kuwa mgeni Rasmi kwenye maonesho ya biashara ya Teknolojia na Madini mkoani Shinyanga.

Maonesho hayo yatafanyika kuanzia Julai 23 mwaka huu hadi Agost Mosi, katika viwanja vya Butulwa, Kata ya Old Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, amebainisha  hayo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari ,kuwa maonesho hayo ni ya awamu ya pili, ambayo yamelenga kukuza Sekta ya Madini na biashara mkoani humo.

Alisema Mkoa wa Shinyanga una migodi mingi ya madini , hivyo kupitia maonesho hayo, yatatoa fursa kwa wawekezaji kuja kuwekeza mkoani humo, pamoja na kuunganisha mtandao wa wafanyabiashara.

"Maonesho haya ya Biashara na Teknolojia ya madini mkoani Shinyanga, yatatusaidia kukuza uchumi wa Mkoa wetu, na  pato la mtu mmoja mmoja, na Taifa kwa ujumla, na tuta yafungua Julai 23, na Mgeni Rasmi atakua Waziri Mkuu Kassim Majaliwa," amesema Dk. Sengati.

"Tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye maonesho haya, kuja kuona madini live, pamoja na wafanya biashara wajumuike ili wapate mtadao na kukuza biashara zao," ameongeza.

Naye Mwenyekiti wa Maonesho hayo Kulwa Meshack, ambaye ni Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA)mkoani Shinyanga, alisema maonesho hayo ni fursa kwa wachimbaji na wafanyabiashara, ambapo watabadilisha uzoefu namna ya kufanya kazi zao.

MAVUNDE AWASHUKURU WANANCHI DODOMA,ASIKILIZA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA WANANCHI NA KUZITAFUTIA UFUMBUZI

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akiwa ameongozana na Kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Dodoma Mjini, jana amefanya mkutano wa kuwashukuru wananchi kwa kuichagua CCM 2020 sambamba na kusikiliza kero,changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Baada ya kusikiliza Changamoto za wananchi wa eneo husika,Mbunge Mavunde alieleza haya yafuatayo;

-Katika kutatua changamoto ya maji mtaa wa Chididimo,tumeshapata fedha za uchimbaji wa kisima kipya cha maji, kazi ambayo itaanza mapema mwezi Agosti.
Kusambaza umeme maeneo yote ya mitaa iliyosalia katika kata ya Zuzu hasa mitaa ya Chididimo na Sokoine.


Kufuatilia malipo ya fidia ya barabara ya mzunguko(Outer Ring Road) kwa wananchi ambao bado hawajahakikiwa na kuingizwa kwenye malipo.


Kufuatilia kwa ukaribu malipo ya fidia kwa wananchi wanaopisha maeneo yao kwa ajili ya uwekezaji,mashamba darasa na hifadhi ya wanyama(Zoo).


Kusimamia uwasilishwaji mapema  wa fedha Tsh 20,000,000 za ujenzi wa miundombinu ya vyoo Shule ya Msingi Chididimo
 

Ujenzi wa Sekondari Mpya kata ya Zuzu kwa nguvu za Mbunge na wananchi kuwapunguzia mwendo watoto wa shule kutembea umbali mrefu.
Kurasimisha vikundi vya wavuvi na kuviwezesha mikopo vikundi vya wakina Mama,Vijana na watu wenye ulemavu.


Kutoa magodoro 30 kwa ajili ya  Hostel ya Wanafunzi wa Sekondari wanaotoka maeneo ya mbali.




 

RAIS SAMIA ATOA MILIONI 100 UJENZI WA PAA SOKO LA MACHINGA COMPLEX.


RC Makalla aelekeza Suma JKT kuanza Ujenzi Mara moja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi Cha Shilingi Milioni 100 kwaajili ya Ujenzi wa Paa la Kisasa la kuzuia Jua na Mvua kwa Wahanga 1,800 wa Soko la Kariakoo waliohamishiwa Machinga Complex ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amethibitisha kupokea fedha hizo.


Akizungumza na Wafanyabiashara hao, RC Makalla amesema baada ya Jana kuwatembelea na kuwasikiliza, Rais Samia aliona changamoto hiyo na alipomuuliza RC Makalla kiasi Cha fedha kinachohitajika alisema ni Milioni 62 za Ujenzi wa Paa la Turubai lakini kwa kutambua umuhimu wa Wafanyabiashara Rais  Samia alitoa Milioni 100 ili lijengwe Paa la Kudumu kwa Bati la Kisasa.


Kutoka na fedha kupatikana, RC Makalla amewaelekeza Suma JKT ambao ndio wajenzi kuanza Ujenzi Mara moja ili Wafanyabiashara hao wafanye biashara bila kero.


Kuhusu suala la Meza, RC Makalla amesema tayari amepatikana Mkandarasi atakaejenga Meza za kisasa za kuhamishika kuendana na hadhi ya Soko.


Aidha RC Makalla ameelekeza Viongozi wa Jiji la Ilala kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya Taka, Mifumo ya Maji, Mifumo ya umeme na wafunge Vizima Moto ili kukabiliana na majanga ya Moto.




Thursday, July 8, 2021

RAIS SAMIA AKISALIMIANA NA WANANCHI WA DUMILA WILAYANI KILOSA NA GAIRO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi  Dumila Wilayani Kilosa alipokuwa njiani akirejea Jijini Dodoma  Julai 08,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Gairo wakati akimalizia ziara yake ya siku mbili mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi pamoja na Wasanii mara baada ya kuhutubia wananchi wa Dumila mkoani Morogoro.
Wasanii mbalimbali kutoka Dar es Salaam wakimpungia mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Dumila mkoani Morogoro
Wananchi wa Dumila wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mara baada ya kusimama katika eneo hilo. PICHA NA IKULU

Wednesday, July 7, 2021

WAZIRI MKENDA ATUA SIMIYU//AZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA KUONGEZA UZALISHAJI NA TIJA KATIKA ZAO LA PAMBA


Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati Akizindua kampeni ya Kuongeza Tija katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu tarehe 4 Julai 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akikata utepe kuashiria kuzindua kampeni ya Kuongeza Tija katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu tarehe 4 Julai 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati alipotembelea na kukagua shamba darasa la Pamba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kuongeza Tija katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu tarehe 4 Julai 2021.
Balozi wa Pamba Tanzania Ndg Agrey Mwanri akitoa elimu kwa wakulima wa Pamba kuhusu namna bora ya kulima, kupanda kwa kufuata mistari kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda kuzindua kampeni ya Kuongeza Tija katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu tarehe 4 Julai 2021.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Ndg Marco Mtunga akitoa ufafanuzi juu ya dhamira ya Bodi kuhakikisha Tija inaongezeka kwenye zao la Pamba mbele ya mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda kabla ya kuzindua kampeni ya Kuongeza Tija katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu tarehe 4 Julai 2021.
Sehem ya wananchi wa Wilaya ya Busega wakifuatilia maelezo ya wataalamu kuhusu namna bora ya kulima zao la Pamba kabla ya rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkend kuzindua kampeni ya Kuongeza Tija katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu tarehe 4 Julai 2021.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu

“Tija ya zao la pamba kwa sasa ni kilo 200 hadi 300 kwa ekari. Taarifa nilizonazo, tunaowakulima wanozingatia kanuni 10 za kilimo bora cha pamba na tija yao ni kati ya kilo 1,000 na 1,200 kwa ekari. Tanzania ina fursa kubwa ya kuongeza uzalishaji wa pamba kutoka wastani wa tani 300,000 hadi tani 1,000,000”      

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo tarehe 5 Julai 2021 wakati Akizindua kampeni ya Kuongeza Tija katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

“Kwa lengo la kufikia lengo la kuzalisha tani 1,000,000 ifikapo mwaka 2025 kama ilivyoainishwa kwenye ilani, leo ni siku muhimu sana. Nimezindua kampeni ya kuongeza tija katika zao la pamba. Wizara iliona ni muhimu kuendesha kampeni kabambe ya kuwahamasisha wakulima wa pamba kuzingatia kanuni 10 za kilimo bora cha pamba” Amekaririwa Waziri Mkenda

Amesema Kwa kuwa pamba inazalishwa katika Mikoa 17 nchini, hivyo Wakuu wa Mikoa na viongozi wote katika ngazi mbalimbali, wanapaswa kuunga mkono juhudi hizo ikiwemo Wabunge kusaidia kuelimisha wananchi katika maeneo yao ili kilimo cha pamba kiwe mkombozi wa maisha wakulima na watanzania kwa ujumla wake.

Waziri Mkenda amesema kuwa kilimo kinakabiliwa na tatizo kubwa la tija kuwa ndogo sana karibu katika kila zao. Hali hiyo inasababisha pato la mkulima kuwa chini.

”Wizara yangu imelitambua tatizo hili la msingi na kwamba tuna jukumu kwanza la kuuelimisha umma na wakulima kwa ujumla juu ya umuhimu wa kuangalia pato la mkulima kama kigezo cha ufanisi katika shughuli zote za kilimo. Pili tuna wajibu wa kuweka mazingira sahihi ili kila mkulima nchini wa zao lolote abadili maisha yake kutokana na shughuli yake. Hivyo, kwa nafasi ya pekee niwapongeze Wadau wa Pamba kuwa wa kwanza kutekeleza maono ya Wizara ya Kilimo katika kuongeza tija” Amesema Waziri Mkenda

Waziri wa Kilimo amesem akuwa Kipato cha mkulima kinategemea kiasi mkulima anachozalisha kwa ekari, ubora wa zao na bei ambayo soko liko tayari kulipa. Mkulima yoyote ana uwezo wa kupata tija kubwa na kuzalisha zao bora. “Muda umefika wa viongozi na wakulima kuelewa kwamba tija ikiwa kubwa kwa bei yoyote itakayokuwepo sokoni, pato litakuwa kubwa” Amesisitiza

Waziri Mkenda amesema kuwa ili kilimo kiweze kutoka kwenye tija ndogo, suala la kuboresha utoaji wa huduma za ugani ni la lazima. Katika mwaka huu wa fedha jumla ya Pikipiki 1,500 zitanunuliwa na kusambazwa katika mikoa mbalimbali baada ya kutosheleza Mikoa ya Dodoma, Singida na Dodoma.

Amesema kuwa kuwa Lengo ni kufanya vizuri katika Mikoa 3 ili mwaka ujao kujipima kiasi cha mafanikio na kuongeza nguvu kuifikia mikoa mingine; ikiwa ni pamoja na Maafisa Ugani kupatiwa mafuta  ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao; na Ili kuimarisha usimamizi vyombo vya usafiri vitafungiwa GPS.

Kwa upande wake Balozi wa Pamba Tanzania Ndg Geofrey Mwanri akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema kuwa ili tija iweze kuongezeka kwenye zao la Pamba ni lazima wakulima Kubadili vipimo vya kupandia kutoka 90x40cm na kuwa 60x30cm ambapo idadi ya mimea kwa ekari itaongezeka kutoka 22,222 hadi 44,400. Mabadiliko yanafanyika baada ya kukamilika kwa utafiti uliofanywa na TARI Ukiriguru na kuonesha ongezeko kubwa la tija kufikia kilo 1,000 kwa ekari.

Mwanri amesema kuwa wakulima wanapaswa Kusomba samadi na kusambazwa mashambani ili kurutubisha udongo ambapo wakulima wa pamba wanapaswa kuondokana na matumizi ya jembe la palizi la kukokotwa na wanyamakazi. Hatua hii itarahisisha palizi kufanyika kwa saa 2 kwa ekari badala ya siku 7 kwa jembe la mkono;

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba  Ndg Marco Mtunga amesema kuwa Bodi ya Pamba imejipanga Kuimarisha huduma za ugani, Kusambaza kamba za kupandia katika wilaya zote ili kuwezesha wakulima wa pamba kuzingatia vipimo vipya vya upandaji; na Pembejeo zote ikiwemo mbegu, viuadudu, vinyunyizi kusambazwa kwa wakati.

Ameongeza kuwa katika maeneo yote ya usukumani na mikoa inayolima Pamba wakulima hawana tatizo la nguvu kinachokosekana ni maarifa machache yanayopatikana kwenye kilimo cha Pamba.

Hata hivyo amewapongeza wakulima wa Pamba kote nchini kwa kuitikia mwito wa serikali wa kuhakikisha uzalishaji unaongezeka katika msimu wa mwaka 2020/2021 hivyo amewaomba wananchi kuitikia tena mwito wa serikali kuhakikisha kuwa uzalishaji na tija unazidi kuongezeka.


Monday, July 5, 2021

WAZIRI PROF MKENDA: USHIRIKA USIINGILIWE KIMAJUKUMU


Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda amewaonya baadhi ya viongozi wenye tabia ya kuingialia Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) huku akiwataka kuacha tabia hiyo mara moja.

Aidha, amesema ushirika sio idara ya serikali hivyo hauwezi kuongozwa kama idara kwakuwa mamlaka yake ina mipaka na hakuna kiongozi anayetakiwa kuingilia matumizi ya fedha wala kuzipangoa matumizi.

Waziri Mkenda ametoa agizo hilo (Jumamosi, Julai 3, 2021) kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya lipuli, Tabora, ambapo alisema kwa kiasi kikubwa serikali imepambana kurejesha mali mbalimbali za ushirika zilizokuwa zimeibiwa kupitia ushirika.

”Tumepambana sana na wabadhilifu kwenye ushirika na kurejesha mali mbalimbali zilizoibiwa kupitia ushirika hivyo kurudisha imani ya wanaushirika, na mali zao haziwezi kufanyiwa ubadhirifu wa aina yoyote.

Tutaendelea kusimamia ushirika kuhakikisha kwamba unaendelezwa kwa weledi, uwajibikaji na uwazi ili watu wengi wakubali kujiunga na ushirika kwa sababu unasaidia sana kunyanyua hali zao za kimaisha kwa kuwa  ni hiari kujiunga hakuna kulazimishwa,”alisema.

Alieleza kuwa ushirika ni hiari na msingi wa kwanza duniani na kwamba ni kweli ushirika sio idara ya serikali hivyo hauwezi kuongozwa kama IDARA YA SERIKALI KWAKUWA mamlaka yake kwenye ushirika yana mipaka yake.

”Na hili ni muhimu kwa sababu kuna mahali ametokea kiongozi mmoja kaingia kwenye AMCOS anatoa amri toa shilingi milioni ishirini na tano hapa peleka kule, hatuna mamlaka hayo, ushirika ni hiyari ya wanaushirika

”Na hapaswi kupelekesha wana ushirika wanapaswa kujisikia kwamba ushirika ni mali yao, wasimame kidete, wasimamie shughuli zao bila kuingiliwa kinyume na taratibu zinazokubalika,”alisema.

Alisisitiza anasema hilo kwa sababu kuanzia Waziri wa kilimo (yeye), Mrajisi wa ushirika, wote lazima wajue mpaka upi wa kwao au si wao

”Mpaka sasa tunakwenda vizuri ukiacha hilo tukio mtu kwenda kutoa amri chukua hela za ushirika kutoka eneo moja kupeleka eneo ambalo ushirika huo hauhusiki nalo kwenda kujenga shule,

”shule ni jambo zuri lakini hakuna mamlaka ya kiongozi yoyote kwenda kuingia kwenye ushirika kuingilia fedha zao kuzipangia matumizi hayo yatafanywa na wanaushirika wenyewe ,”alisema.

Wednesday, June 23, 2021

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MKUTANO WA SADC, MAPUTO NCHINI MSUMBIJI

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Joaquim Chissano uliopo Maputo nchini Msumbiji leo tarehe 23 Juni, 2021.

 


Monday, June 21, 2021

MAANDALIZI YA MKUTANO WA 14 WA MAWAZIRI WA EAC WA SEKTA YA KILIMO NA USALAMA WA CHAKULA YAANZA JIJINI ARUSHA

Mkutano wa 14 Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Ngazi ya Wataalam umeanza hivi karibuni jijini Arusha ukiwashirikisha Wataalam wa Kilimo kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.

Mkutano wa Wataalam utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 24 Juni 2021 na kuhitimishwa na Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 25 Juni 2021.

Lengo la Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo  na Usalama wa Chakula pamoja na mambo mengine ni kupitia na kujadili utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya pamoja na kupitia na kujadili masuala mbalimbali  muhimu ya kisera, kikmkakati, miradi na program zinazotekelezwa katika sekta ya kilimo.

Kadhalika agenda muhimu zitajadiliwa wakati wa mkutano huo ambazo ni pamoja na Taarifa ya Usalama wa Chakula ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu Mradi wa Afrika wa Kilimo cha Ushindani cha Mpunga kwa Kanda ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu Maendeleo ya Mifugo; Taarifa kuhusu Mradi wa Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu; Taarifa kuhusu Maendeleo ya Uvuvi; na Taarifa kuhusu Uhamasishaji wa Uchangiaji Rasilimali.

Awali akifungua Mkutano huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Peter Muthuki, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo anayeshughilikia Sekta za Uzalishaji na Jamii, Mhe. Christophe Bazivamo amezitaka Nchi Wanachama kujikita kwenye kilimo cha ushindani na kuboresha viwango vya mazao yanayozalishwa na nchi zote wanachama ili kupata soko la ndani na nje ya jumuiya la mazao hayo kwa manufaa ya wananchi wa jumuiya.

Pia amesisitiza umuhimu wa nchi wanachama kuendelea kuwajengea uwezo wakulima katika maeneo yao kwa kutoa elimu ya kilimo bora na chenye manufaa ili kupata mazao bora yenye viwango vinavyokubalika ndani na nje ya mipaka ya nchi wanachama.

“Napenda kuzihimiza nchi wanachama kutoa elimu ya kilimo bora kwa wakulima wao pamoja na kuwajengea uwezo ili kuwawezesha kuzalisha mazao bora na yenye viwango vinavyokubalika ndani ya jumuiya na nje ili hatimaye wunufaike na soko la ndani na nje ya jumuiya” alisisitiza Dkt. Muthuki kwenye hotuba yake.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mkutano huo wa Ngazi ya Wataalam, Bw. Julius Mwabu kutoka Jamhuri ya Kenya aliwataka wajumbe wa mkutano huo kujadili na kutoa mapendekezo yenye tija kuhusu Sekta ya Kilimo na Usalama wa Chakula kwani ni miongoni mwa sekta muhimu zinazotegemewa na wananchi wote wa nchi wanachama wa Jumuiaya ya Afrika Mashariki.

Aliongeza kuwa, mbali na changamoto ya ugonjwa wa corona uliozikumba nchi mbalimbali duniani zikiwemo zile za Jumuiya ya Afrika Mashariki, yapo mafanikio kadhaa yaliyopatikana katika sekta ya kilimo na usalama wa chakula na kuwaomba wajumbe kujadili na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto hiyo ili kuziwezesha nchi wanachama kutotetereka katika kipindi hiki ambacho ugonjwa huo bado haujatokomezwa.

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Ngazi ya Wataalam umeongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Kilimo, Bw. Gungu Mibavu na kuhudhuriwa pia na Maafisa Waandamizi kutoka Sekta mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya kilimo na usalama wa chakula hapa nchini. 

Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Kilimo, Bw. Gungu Mibavu akizungumza kama kiongozi wa ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wataalam uliofanyika jijini Arusha hivi karibuni ikiwa ni maandalizi ya awali ya Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini hapa tarehe 25 Juni 2021. Mkutano wa ngazi ya wataalam utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu tarehe 24 Juni 2021.
Mwenyekiti wa Mkutano wa Ngazi ya Wataalam, Bw. Julius Mwabu kutoka Kenya akiwa na Mkurugenzi wa Sekta ya Uzalishaji katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw.Jean Havugimana (kulia) pamoja na Katibu wa Mkutano huo kutoka Burundi

Mwenyekiti wa Mkutano wa Ngazi ya Wataalam, Bw. Mwabu akizungumza wakati wa mkutano huo
Mkurugenzi wa Sekta ya Uzalishaji kutoka Sekrtarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Havugimana naye akizungumza wakati wa mkutano wa wataalam

Ujumbe wa Kenya ulioshiriki mkutano wa wataalam
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Kenya ukifuatilia mkutano
Mjumbe wa Burundi naye akishiriki mkutano wa wataalam
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Benjamin Mwesiga akishiriki mkutano wa wataalam
Ujumbe wa Tanzania ukiwa kwenye mkutano wa wataalam
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania kutoka sekta mbalimbali zinazojishughulisha na kilimo wakifuatilia mkutano wa wataalam
Mkutano ukiendelea
Wajumbe kutoka Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishiriki mkutano wa wataalam
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania katika mkutano
Mkutano ukiendelea
Mshiriki mwingine wa mkutano kutoka Tanzania

Saturday, June 19, 2021

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 19 Juni, 2021 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya katika Mikoa ya Tanzania Bara kama ifuatazo:-

Mkoa wa Arusha (1).

1.    Sophia Edward Mjema kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

2.    Eng. Richard Henry Ruyango kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

3.    Raymond Stephen Mangwala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro.

4.    Nurdin Hassan Babu kuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido.

5.    Frank James Mwaisumbe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli.

6.    Abbas Juma Kayanda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu.

Mkoa wa Dar es Salaam (2).

7.Godwin Crydon Gondwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

8.    Ng’wilabuza Ndatwa Ludigija kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala.

9.    Jokate Urban Mwegelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

10.Fatma Almas Nyangasa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni.

11.Kherry Denis James kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.

Mkoa wa Dodoma (3).

12.Gift Isaya Msuya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chamwino.

13.Jabir Mussa Shekimweri kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.

14.Simon Kemori Chacha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba.

15.Khamis Athumani Mkanachi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kondoa.

16.Mwanahamisi A. Munkunda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi.

17.Josephat Paul Maganga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa.

18.Remedius Mwema Emmanuel kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa.

Mkoa wa Geita (4).

19. Said Juma Nkumba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe.

20. Eng. Charles Francis Kabeho kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe.

21.Jamuhuri David William kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale.

22. Wilson Samwel Shimo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita.

23.Martha John Mkupasi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato.

Mkoa wa Iringa (5).

24.Saada Ahmed Mtambule kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi.

25. Peres Boniphace Magiri kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo.

26. Mohamed Hassan Moyo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa.

Mkoa wa Kagera (6).

27.Kemirembe R. Lwota kuwa Mkuu wa Wilaya ya Biharamuro.

28.Juliet Banyula Nkebanyi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe.

29.Toba Alnason Nguvila kuwa Mkuu wa Wilaya ya Muleba.

30. Rashid Mwaimu Mohamed kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa.

31.Moses Joseph Machali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba.

32.Col. Mathias Julius Kahabi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara.

33.Col. W.C. Sakullo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi.

Mkoa wa Katavi (7).

34.Filberto Hassan Sanga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mlele.

35. Jamila Yusuph Kimaro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda.

36. Onesmo Mpuya Buswelu kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika.

Mkoa wa Kigoma (8).

37.Ester Alexander Mahawe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma.

38.P 8608 Col. I. A. Mwakisu kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu.

39.Col. E. M. Malasa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko.

40. Hanafi Hassan Msabaha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza.

41.Col. Michael Masala Nyayalina kuwa Mkuu wa Wilaya ya Buhingwe.

42. P 8310 Col. A. J. Magwaza kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo.

Mkoa wa Kilimanjaro (9).

43.Thomas Cornel Apson kuwa Mkuu wa Wilaya ya Siha.

44. Said Mtanda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi.

45. Abdallah Mussa Mwaipaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga.

46.Col. H. M. Maiga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo.

47. Juma Said Irando kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.

48.Edward Jonas Mpogolo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Same.

Mkoa wa Lindi (10).

49.Hashim Abdallah Komba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea.

50. Hassan Nassor Ngoma kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa.

51. Judith Martin Nguli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Liwale.

52. Shaibu Issa Ndemanga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi.

53.Zainab Rashid Mfaume Kawawa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa.

 

 

Mkoa wa Manyara (11).

54.Lazaro Jacob Twange kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati.

55. Sezaria Venneranda Makota kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu.

56. Janeth Peter Mayanja kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang

57.Mbaraka Alhaji Batenga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto.

58.Dkt. Suleiman Hassan Serera kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Mkoa wa Mara (12).

59.Juma Issa Chikoka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya.

60. Dkt. Vicent Mashinji kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti.

61. Joshua Samwel Nassari kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda.

62. Mwl. Moses Rudovick Kaegele kuwa Mkuu wa Wilaya ya Butiama.

63. Lt. Col. Michael Mangwela Mtenjele kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime.

64. Dkt. Halfan Haule kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma.

Mkoa wa Mbeya (13).

65.Mayeka Simon Mayeka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya.

66. SACP. Ismail Twahir Mlawa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela.

67. Dkt. Rashid Chuachua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya.

68. Dkt. Vicent Naano Anney kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rungwe.

69.Reuben Ndiza Mfune kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali.

Mkoa wa Morogoro (14).

70. Jabir Omary Makame kuwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo.

71. Hanji Yusuph Godigodi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero.

72. Halima Habib Okash kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero.

73.Albert Msando kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.

74. Ngollo Ng’waniduhu Malenya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga.

75. Majid Hemed Mwanga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa.

76. Mathayo Francis Masele kuwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi.

Mkoa wa Mtwara (15).

77.Mwangi  Rajab Kundya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Newala.

78. Mariam Khatib Chaurembo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu.

79. Dunstan Dominick Kyobya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara.

80. Claudia Undalusyega Kitta kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi.

81. Col. Patrick K. Sawala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba.

Mkoa wa Mwanza (16).

82. Hassan Elias Massalla kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela.

83. Johari Mussa Samizi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba.

84. Senyi Simon Ngaga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema.

85. Amina Makilagi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana.

86. Salum Hamis Kalli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu.

87. Col. Denis Filangali Mwila kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe.

88. Veronika Arbogast Kessy kuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi.

Mkoa wa Njombe (17).

89. Kisa  Gwakisa Kasongwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe.

90. Andrea Axwesso Tsere kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa.

91. Lauter John Kanoni kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe.

92. Juma Samwel Sweda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Makete.

Mkoa wa Pwani (18).

93.Zainab Abdallah Issah kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo.

94. Khadija Nassir Ali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga.

95. P 10699 Capt. Gowelle kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji.

96. Martin Stephen Ntemo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mafia.

97. Sara Ally Msafiri kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.

98. Nickson Simon John kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

99.P 8189 Col. Ahmed A. A kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti.

Mkoa wa Rukwa (19).

100.Sebastian Muungano Waryuba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga.

101. Peter Ambrose Lijuakali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi.

102. Tano Seif Mwera kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo.

 

Mkoa wa Ruvuma (20).

103. Julius Keneth Ningu kuwa Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo.

104. Aziza Ally Mangosango kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga.

105. P 8819 Col. L. E Thomas kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa.

106. Julius Sunday Mtatiro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru.

107. Polotet Kamando Mgema kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea.

 

Mkoa wa Shinyanga (21).

108. Joseph Modest Mkude kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu.

109. Jasinta Venant Mboneko kuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga.

110. Festo Kiswaga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama.

 

 

 

 

 

Mkoa wa Simiyu (22).

111. Gabriel Zakaria Olemegili kuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega.

112. Aswege Enock Kaminyoge kuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa.

113. Dkt. Charles Mhina kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi

114. Fauzia Hamidu Ngatumbura kuwa Mkuu wa Wilaya ya Meatu.

115. Faiza Suleiman Salim kuwa Mkuu wa Wilaya ya Itilima.

Mkoa wa Singida (23).

116. Sophia Mfaume Kizigo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama.

117. Rahabu Jackson Mwagisa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.

118. Paskasi Damian Murangili kuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida.

119. Jerry Cornel Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi.

120. Kenan Laban Kihongozi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba.

Mkoa wa Songwe (24).

121. Simon Peter Simalenga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe.

122. Anna Jerome Gidarya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje.

123. Cosmas Isuna Nshenye kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi.

124. Fack Raphael Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba.

Mkoa wa Tabora (25).

125. ACP. Advera John Bulimba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nzega.

126. Matiko Paul Chacha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua.

127. Sauda Salum Mtondoo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga.

128. John Ernest Pallingo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sikonge.

129. Dkt. Yahya Ismail Nawanda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora.

130. Louis Peter Bura kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo.

131. Kisare Matiku Makori kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui.

Mkoa wa Tanga (26).

132. Hashim Shaibu Mgandilwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga.

133. Halima Abdallah Bulembo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza.

134. P 8576 Col. M. H Surumbu kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

135. Ghaibu Buller Lingo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani.

136. Siriel Mchembe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.

137. Basilla Kalubha Mwanukuzi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe.

138. Abel Yeji Busalama kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi.

139. Kalist Lazaro Bukhay kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto.

Wakuu wa Wilaya wateule wataapishwa  kuanzia tarehe 21 Juni, 2021 saa nne (4) asubuhi na Wakuu wa Mikoa yao.

 

Jaffar Haniu

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.