Matokeo chanyA+ online




Monday, February 20, 2023

MAKAMU WA RAIS UFUNGUZI WA MWAKA WA MAHAKAMA YA AFRIKA - ARUSHA

Mpango akizungumza na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Imani Aboud wakati alipowasili Makao Makuu ya Mahakama hiyo mkoani Arusha kuhudhuria ufunguzi wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu   tarehe 20 Februari 2023. (Kulia ni Makamu wa Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Blaise Tchikaya)


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia Majaji, Viongozi na Watumishi mbalimbali wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu wakati wa Ufunguzi wa Mwaka wa Mahakama hiyo uliofanyika Makao Makuu ya Mahakama hiyo mkoani Arusha  tarehe 20 Februari 2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea Vitabu vya Hukumu mbalimbali zilizotolewa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu tangu kuanzishwa kwakwe kutoka kwa Rais wa Mahakama hiyo Jaji Imani Aboud mara baada ya  Ufunguzi wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika Makao Makuu ya Mahakama hiyo mkoani Arusha leo tarehe 20 Februari 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi ya nishani kutoka kwa Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Imani Aboud wakati alipowasili kuhudhuria Ufunguzi wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika Makao Makuu ya Mahakama hiyo mkoani Arusha tarehe 20 Februari 2023



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika Makao Makuu ya Mahakama hiyo mkoani Arusha  tarehe 20 Februari 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Imani Aboud na Makamu wake Jaji Blaise Tchikaya, Majaji wa Mahakama hiyo, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, Majaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki pamoja na Viongozi mbalimbali mara baada ya  Ufunguzi wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika Makao Makuu ya Mahakama hiyo mkoani Arusha leo tarehe 20 Februari 2023.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa wito kwa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuzingatia Mamlaka yake ili kuepukana  na  malalamiko ya nchi wanachama ya kuingilia uhuru wa ndani wa nchi hali inayopelekea baadhi ya Nchi Wanachama kuondoa matamko ya kujiweka chini ya mamlaka ya Mahakama hiyo huku baadhi zikisita kuridhia Mkataba ulioanzisha Mahakama hiyo. 

Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 20 Februari 2023, wakati wa Ufunguzi wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu, uliofanyika Makao Makuu ya Mahakama hiyo Mkoani Arusha. Amesema changamoto zinazopaswa kufanyiwa kazi ni pamoja na zile za kusikiliza na kutolea hukumu mashauri ambayo yako nje ya mamlaka ya mahakama hiyo, Mahakama kutoa  hukumu dhidi ya nchi wanachama bila kuzingatia mazingira na mifumo ya kisheria ya nchi za Afrika na kupelekea hukumu hizo kutotekelezeka. Ameongeza kwamba njia ya mazungumzo kati ya Mahakama na Nchi Wanachama inapaswa kutumika ili malengo yaliyokusudiwa ya Mahakama hiyo yaweze kufikiwa. 

Makamu wa Rais amempongeza  Rais wa Mahakama hiyo Mheshimiwa Jaji Imani Aboud, kwa hatua anazochukua kuimarisha mahusiano kati ya Mahakama hiyo na Nchi Wanachama na kumsihi kuendeleza jitihada hizo.

Makamu wa Rais amesema Tanzania ina dhamira ya dhati kutekeleza malengo ya Umoja wa Afrika na utekelezaji wa Ajenda 2063 pamoja na  kushiriki katika kujenga Taasisi imara za Afrika ikiwa ni pamoja na Mahakama ya Afrika. Amesema kwa kutambua wajibu wa kuhamasisha na kutetea  haki za binadamu, Tanzania imeendelea kuwa chini ya mamlaka ya Mahakama ya Haki  ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu pamoja na  kusaini  na kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa ya haki za 

binadamu.

 

Halikdhalika Makamu wa Rais Dkt. Mpango ametoa wito kwa Mahakama za ndani kuongeza matumizi ya sheria na maamuzi ya mahakama za kimataifa kwa kuongeza matumizi ya TEHAMA ili kuwezesha majaji na wanasheria kupata sheria na maamuzi ya mahakama za kimataifa kwa urahisi. Pia Makamu wa Rais ameiasa Mahakama ya Afrika kuendelea kufanya makongamano ya sheria yatakayokutanisha wadau mbalimbali wa sheria kutoka nchi zenye mifumo tofauti ya sheria ili kuwezesha katika kujifunza na kubadilishana uzoefu. 

Vilevile Makamu wa Rais ametoa wito kwa vyombo vya utoaji haki vya ndani ya nchi kujifunza pamoja na kutumia sheria na maamuzi  ya mahakama za haki za binadamu za kikanda na kimataifa ili kufikia maamuzi katika masuala ya haki za binadamu kwa kuzingatia sheria, hukumu na mazingira ya ndani ya nchi husika katika kufikia uamuzi hayo.

Makamu wa Rais ameipongeza Mahakama hiyo kwa mafanikio makubwa iliyofikia katika kulinda na kutetea haki za binadamu tangu ilipoanzishwa. Ameyataja mafanikio hayo ni pamoja na kusikiliza na kutoa hukumu mbalimbali zinazolinda na kutetea haki za binadamu, kuendeleza mjadala na wadau na nchi wanachama wa umoja wa Afrika kuhusu haki za binadamu na kutoa elimu ya haki za binadamu kwa wadau mbalimbali. 

 

Kwa upande wake Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mheshimiwa Jaji Imani Aboud amesema ni vigumu kwa  malengo ya Umoja wa Afrika ya Ajenda 2063 kufikiwa bila kuwepo msingi imara wa haki za binadamu kwani ustawi, umoja, utangamano, maendeleo, ulinzi na usalama pamoja  na utangamano katika jumuiya za kimataifa unafungamanishwa na  haki za binadamu. 

Amesema Mahakama huru ni chanzo cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi pamoja na kisiasa kwa jamii yeyote ile. Ameongeza kwamba tangu kuanzishwa kwa Mahakama hiyo tayari imetoa hukumu zaidi ya mia mbili ambazo zinagusa nyanja mbalimbali za maisha ya kila siku ya wananchi.

Saturday, February 18, 2023

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano wa 36 wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza kwenye Mkutano wa 36 Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika katika Ukumbi wa Nelson Mandela uliopo Makao Makuu ya Umoja huo Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 18 Februari, 2023.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika wakati wakishiriki Mkutano wa 36 Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika katika Ukumbi wa Nelson Mandela uliopo Makao Makuu ya Umoja huo Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe18 Februari, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 36 Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika katika Ukumbi wa Nelson Mandela uliopo Makao Makuu ya Umoja huo Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 18 Februari, 2023.



 

Friday, February 17, 2023

DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE MWENYEKITI MPYA WA KAMATI YA TUZO YA CHAKULA AFRIKA



 Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Tuzo ya Chakula Afrika, akichukua nafasi ya Rais wa zamani wa Nigeria Jenerali Olusegun Obasanjo ambaye amekuwa Mwenyekiti tangu 2016.

 

Hafla ya kutangazwa kwa uteuzi huo imefanyika katika Hoteli ya Radisson Blu mjini Addis Ababa, Ethiopia, Ijumaa, Februari 17, 2023, kando ya Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Umoja wa Afrika.



 Tuzo ya Chakula Afrika ni tuzo inayotambua wanawake, wanaume, na taasisi ambazo michango yao katika kilimo cha Kiafrika inaanzisha enzi mpya ya usalama endelevu wa chakula na fursa ya kiuchumi ambayo inainua Waafrika wote.


Uteuzi wa Dk. Kikwete unaenda sambamba na wito wa wagombea kwa mwaka 2023  kuwania Tuzo hiyo ya Chakula Afrika yenye kitita cha Zawadi cha Dola za Marekani 100,000. Mwaka huu, kampuni ya NestlĂ© ikishirikiana na Tuzo ya Chakula Afrika, imechangia pesa hizo  ambazo zitatolewa kwa mshindi wa tuzo kuu.



Jenerali Obasanjo alimshukuru Dk. Kikwete kwa kuukubali uteuzi huo, akimtaja kuwa ni mtu mwenye mapenzi na ari ya dhati katika kuleta mageuzi ya kilimo barani Afrika.

 

“Nampongeza Dk Kikwete kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tuzo ya Chakula Afrika. Nina imani kuwa bara hili litaendelea kutafiti na kutekeleza mikakati ya mifumo ya chakula ambayo itawainua watu kutoka katika umaskini kupitia ukuaji jumuishi na maendeleo endelevu,” Obasanjo alisema kwenye hafla hiyo.

 

 Jenerali Obasanjo alisema kuwa Dk. Kikwete ana rekodi ya nzuri  sana ya kuwa mchangiaji mkuu katika mabadiliko ya mifumo ya chakula barani Afrika, na kwamba akiwa rais wa Tanzania, alitekeleza ‘Kilimo Kwanza’ mpango ambao ulifungua tija na faida kwa wakulima wadogo nchini humo.

 

“Dkt Kikwete pia anatajwa kama kiongozi ambaye aliongoza utekelezaji wa Ukanda wa Kukuza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), ubia kati ya sekta ya umma na binafsi unaolenga kufungua uwekezaji zaidi wa sekta binafsi katika sekta ya kilimo nchini Tanzania.

 

“Baada ya kustaafu, Dk Kikwete kupitia Taasisi yake ya JMKF amekuwa akishirikiana na wakulima na watafiti kuandaa mipango na mikakati ya kuongeza mavuno na tija katika kilimo cha wakulima wadogo na biashara ya kilimo”, aliongezea Rais huyo mstaafu wa Nigeria.

 

 

 Mashirika, taasisi, biashara na watu binafsi ambao wameunda fursa kwa wakulima wa Afrika kupata riziki kutokana na biashara yao wanaweza kuwasilisha mapendekezo yao kwenye www.africafoodprize.org/nominate kabla ya Jumatatu, 16 Mei 2023.

YANGA WANASEMA MPIRA NI FURAHA,UPENDO,BURUDANI NA KAZI

WHO NA WAWAKILISHI WIZARA YA AFYA TUSHIRIKIANE KUFANIKISHA AFUA ZA ELIM...

RAIS SAMIA AWASILI ETHIOPIA 16 FEB 2023

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano wa Baraza la Amani na Usalama (PSC) la Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika, Addis Ababa nchini Ethiopia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akishiriki Mkutano wa Baraza la Amani na Usalama (PSC) la Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kujadili hali ya Usalama katika eneo la Mashariki ya Jamhuri ya  Kidemokrasia ya Kongo (DRC).





 Mkutano huo umefanyika katika Jengo la Amani na Usalama la Mwalimu Julius Nyerere lililopo Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa tarehe 17 Februari, 2023.


POPO (FRIUT BATS) KIVUTIO KINGINE KATIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA MAJIMAJI SONGEA

 

Moja ya popo wakubwa dunaini wanaolinga na kunguru ambao wanafika ndani ya Makumbusho hayo  kuanzia mwishoni mwa mwezi Novemba kila mwaka na kuzaliana kisha huondoka mwishoni mwa mwezi Februari.Inaaminika popo hao wabatoka nchini Nigeria




Licha ya kuwepo historia hizo,makumbusho ya Taifa ya Majimaji
imepata aina nyingine ya kivutio cha utalii baada ya kubainika
katika makumbusho hayo kuna aina ya spishi ya popo wakubwa
duniani ambao asili yake ni nchini Nigeria.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo,popo hao wa aina yake kila
mwaka kuanzia Oktoba wanafika katika Makumbusho hayo na
kuweka makazi kwenye eneo la miti mikubwa iliyopo katika
kaburi la pamoja ambalo wamezikwa mashujaa 67.
“Hawa popo wanaokadiriwa kuwa kati ya 6000 hadi 10,000
wakifika hapa wanaishi kuanzia Oktoba hadi Februari kila
mwaka,kutokana na uzito wa popo hawa baadhi ya matawi ya miti
mikavu inaanguka na miti mingine inainama kutokana na
uzito’’,anasisitiza Nyamusya.
Hata hivyo utafiti unaonesha kuwa popo wakubwa kuliko wote
duniani wanapatikana hapa nchini katika visiwa vya Pemba na
Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mtafiti Ng’oko Innocent, popo
wanaopatikana katika visiwa hivyo wanafahamika kwa jina la
flying fox bat au fruit bat ambao wanatajwa kuwa ndiyo popo
wakubwa kuliko wote duniani hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa
watalii.
Ukubwa wa popo hao unakadiliwa kufikia gramu  400 hadi 650 na
kwamba wana mabawa yenye urefu wa  mita 1.6 wakiwa na
sura inayofanana na mnyama aina ya mbweha.

Anasema Popo hao ambao baadhi yao wapo katika msitu wa
bandari ya Wete Pemba wana rangi ya chungwa sehemu ya
tumbo na wana masikio,pua na mabawa meusi ambapo  mara
nyingi ukiwa katika kisiwa hicho popo hao wanapatikana kwenye
misitu mikubwa yenye asili ya matunda.
Kisayansi popo wana faida  kubwa ikiwemo ya kusambaza misitu
kutokana na kula matunda ya aina mbalimbali na kuchavusha
maua na kwamba popo hupendelea misitu yenye mvua.
Popo hujamiana kati ya Januari hadi Juni ambapo jike huzaa
mtoto mmoja kwa mwaka.Inakadiriwa popo wana uwezo wa
kuishi kati ya miaka 15 hadi 30 ingawa  baadhi yao hufikisha
hadi miaka 40.














MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA LONGPING YA CHINA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango akifanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Longping
Agriscience LTD wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Liang
Shi, mazungumzo yaliofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam leo tarehe 17
Februari 2023.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya
Longping Agriscience LTD wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
hiyo Liang Shi pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde mara
baada ya mazungumzo yaliofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam leo tarehe 17
Februari 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Longping
Agriscience LTD Liang Shi mara baada ya mazungumzo yaliofanyika Ikulu Jijini
Dar es salaam leo tarehe 17 Februari 2023.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango leo tarehe 17 Februari 2023 amekutana na kufanya
mazungumzo na viongozi wa Kampuni inayojishughulisha na Kilimo kutoka
nchini China ya Longping Agriscience LTD wakiongozwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo Bwana Liang Shi, Mazungumzo yaliofanyika Ikulu
Jijini Dar es salaam.
Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais ameipongeza kampuni hiyo kwa
nia yake ya dhati ya kuwekeza katika kilimo hapa nchini kwa kutambua
uhusiano wa muda mrefu baina ya Tanzania na China. Amesema Tanzania
inaendelea na jitihada za kuimarisha sekta ya kilimo ikiwemo kuanzisha
programu ya kilimo biashara (Building Better Tomorrow) yenye lengo la
kuwasaidia vijana kushiriki katika sekta hiyo kikamilifu na kuchochochea
ukuaji wake kufikia lengo la asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.
Makamu wa Rais amesema ushirikiano huo utaongeza mafanikio zaidi katika
kuifanya Tanzania kuwa nchi tegemeo kwa chakula Barani Afrika kwa
kuzingatia uwepo wa ardhi nzuri ya kilimo pamoja na jiographia ya kuvutia.
Aidha ameongeza kwamba malengo ya kampuni hiyo katika kuweka mnyororo
wa thamani kuanzia uzalishaji wa mbegu hadi uzalishaji mazao na uongezaji
thamani wa mazao hayo viwandani, utaweza kuongeza tija katika kilimo hapa
nchini.
Halikadhalika amewasisitiza kutumia ubunifu, utafiti, ulinzi wa mimea na
matumizi ya teknolojia rafiki ili kuongeza uzalishaji. Pia kutoa mafunzo na
vitendea kazi kwa wakulima na kutumia vema ardhi watakayopata kwa
maendeleo endelevu.
Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Longping Agriscience LTD
bwana Liang Shi amesema Tanzania ni nchi nzuri yenye ardhi ya rutuba
iliobarikiwa kuwa na idadi ya watu ya kutosha pamoja na jiographia
itakayosaidia uzalishaji wa mazao wa uhakika utakaopelekea Tanzania kuwa
tegemeo la chakula kwa Afrika na Dunia kwa ujumla.
Amesema kampuni hiyo imelenga kuanzisha mashamba ya darasa, kuwasaidia
wakulima wazawa kwa mafunzo ya vitendo, kuanzisha vituo vya mauzo
vitakavyoweka uwazi wa bei za mazao katika maeneo mbalimbali nchini.

 




Waziri Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema ataendelea kushirikiana na watendaji wa Wizara hiyo, watumishi pamoja na wadau ili iendelee kung’ara ndani na nje ya nchi kama ilivyo sasa. Amesema hayo Februari 17, 2023 katika Ofisi za Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.





 

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Addis Ababa, Ethiopia





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika Jengo la Usalama na Amani la Julius Nyerere lililopo katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 17 Februari, 2023.

 


 

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan awasili Jijini Addis Ababa Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) tarehe 16 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) tarehe 16 Februari, 2023.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ngoma za asili za Taifa la Ethiopia mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) tarehe 16 Februari, 2023.