Serikali imesema iko katika hatua za mwisho kukamilisha sera ya sayansi,
teknolojia na ubunifu ambayo itatotoa mwongozo wa namna ya utekelezaji
wa masuala ya ubunifu na kuwatambua wabunifu kwa ajili ya maendeleo ya
nchi. Pia
iko tayari kufadhili bunifu mbalimbali zitakazoondoa changamoto za hali
ngumu ya maisha nchini na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Viwanda.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, ameyasema
hayo leo Machi 25, 2019 wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Ubunifu
iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa
kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na wadau
wengine iliyofanyika leo katika ukumbi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia
jijini Dar es Salaam.
Amesema,
katika awamu hii ya Tano, serikali imeweka kipaumbele teknolojia ili
kuongeza chachu ya maendeleo na kufikia uchumi wa viwanda ifikapo 2025.
Amesema
ili kufikia viwango vya ubunifu vinavyohitajika, serikali imeongeza
fedha za ubunifu kwa Costech na kufungua dirisha la kushughulikia
masuala ya ubunifu kwani, ubunifu ni kichocheo cha kufikia uchumi wa
kati kwa kuhakikisha kunakuwa na mazingira wezeshi kwenye sekta za afya,
elimu na viwanda.
Amesema,
mapema katika maonesho ya ubunifu yaliyofanyika jijini Dodoma,
washindi 3O walipatikana na kazi zao zitaplekwa atamizi kwa ajili ya
kuzifanyia kazi na kutumika katika masuala mbalimbali ya kusaidia nchi
Amesema,
amewaasa wadau wawafikie wabunifu wengi zaidi wa kawaida ambao
hawatambuliki ambao hawatambuliki ili waweze kutumia ubunifu zao
zinazoendana na maisha halisi ya wananchi.
"Wabunifu
wengi ni wale wanaokumbana na changamoto za kila siku na kujaribu
kuangalia namna ya kuzitatua hivyo wakati mwingine mtakapoandaa wiki ya
ubunifu muhakikishe kwamba mnaweka katika maeneo ya wazi kwa ajili ya
kuwakutanisha wabunifu wengi na wananchi ili waweze kujua
kinachofanyika," ameeleza.
Aidha
Ole Nasha amewaasa wabunifu kufanya ubunifu zitakazoendana na
changamoto za maisha zilizopo nchini na siyo kufanya bunifu za
kujifurahisha sababu wanaweza kukosa soko.
Naye,
Kiongozi Mkuu wa mfuko (HDIF), David McGinty amesema wadau wa maendeleo
nchini, wamekuwa wakichangia Tanzania kupanda viwango vya kimataifa vya
ubunifu kwani mpaka wanafunzi wa vyuo na sekondari wanahamasishwa
kutumia teknolojia kwa ajili ya kujifunzia.
McGinty
alisema wanaangalia ubunifu katika sekta za maji, afya, elimu na usafi
wa mazingira kwa sababu ni miongoni kwa changamoto zinazoikabili jamii
ya kitanzania.
Kwa
upande wake, Makamu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya
Serikali ya Uingereza, Jane Miller alisema wanaendelea kuhamasisha
wananchi kujitokeza katika Wiki hiyo ili kuona kazi zinazofanywa pamoja
na kuwaunganisha wabunifu kwa lengo la kuleta mabadiliko ya ubunifu
nchini.
Miller
amesema ni lazima watumie ubunifu kutatua changamoto mbalimbali
zinazoikabili Tanzania katika sekta hizo ili kufikia malengo ya uchumi
wa viwanda na kwamba kwa kushirikiana na HDIF wataendelea kufadhiki
bunifu nchibi ili kutekeleza na kuinua masuala ya ubunifu nchini.
Wiki
ya Ubunifu inatekelezwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu
(HDIF) kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
pamoja na wadau wengine.
Naibu
waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Olle Nasha akizungumza
na wabunifu pamoja na wadau wa kazi za bunifu nchini, wakati akizindua
wiki ya Ubunifu leo Machi 25, 2019 katika ukumbi wa Costech jijini Dar
es Salaam waliokaa kulia kwake ni Katibu mkuu wizara hiyo, Dk. Leornad
Akwilapo, akifuatiwa na Kiongozi Mkuu wa HDIF David McGinty na kushoto
ni Mkurugenzi Mkuu wa Costech Dk. Amos Nungu.
Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Sayansi na Technolojia (COSTECH), Dk Amos Nungu
akizingumza na wabunifu na wadau mbalimbali wa kazi za ubunifu wakati wa
uzinduzi wa wiki ya ubunifu iliyoanza leo Machi 25, 2019 ambapo
wabunifu zaidi ya 3000 wa mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Iringa na
watakutana na kubadilishana uwezo kwa lengo la kukuza ubunifu nchini.
Kulia kwake aliyevaa miwani ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia William Olle Nasha akifuatiwa na Katibu mkuu wizara ya Elimu
Sayansi na Teknolojia Dk. Leornad Akwilapo, Na kushoto kwake no Makamu
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Jane
Miller na kushoto Makamu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya
Serikali ya Uingereza, Jane Miller.
Kiongozi
Mkuu wa mfuko wa ubunifu wa maendeleo(HDIF), David McGinty akizungumza
mara baada ya ufunguzi wa wiki hiyo ya ubunifu ambayo imezinduliwa leo
Machi 25, 2019 jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wabunifu pamoja na
wadau mbalimbali wa kazi za bunifu kutoka ndani na nje ya nchi.
Makamu
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Jane
Miller akizungumza mafanikio ya Tanzania yatokanayo na bunifu
zinazofanywa na watanzania wakati wa uzinduzi wa wiki ya bunifu, leo
jijini Dar es Salaam.
Jopo
la wazungumzaji katika wiki ya Ubunifu wakiwa katika meza ya duara
wakiendesha mjadala kuhusiana na maonesho ya ubunifu ambapo wamejadili
na kueleza mambo ambayo wangependa Serikali iyachukue na kuyafanyia
kazi.
No comments:
Post a Comment