Matokeo chanyA+ online




Friday, April 5, 2019

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA MANGAKA-NAKAPANYA-TUNDURU KM 137 PAMOJA NA BARABARA YA MANGAKA –MTAMBASWALA KM 65.5 NANYUMBU MKOANI MTWARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto watatu kutoka kushoto aliyeshika utepe, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru wasita kutoka kulia aliyeshika utepe pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Mtwara, Wabunge, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Mangaka- Nakapanya-Tunduru km 137 pamoja na Barabara ya Mangaka- Mtambaswala km 65.5 sherehe zilizofanyikka katika Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza wadau wa Maendeleo, Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto pamoja na Mwakilishi Mkazi wa benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kufungua barabara ya Mangaka-Nakapanya-Tunduru km 137 pamoja na Barabara ya Mangaka-Mtambaswala km 65.5 katika Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Nanyumbu mara baada ya kufungua barabara ya Mangaka-Nakapanya- Tunduru km 137 pamoja na Barabara ya Mangaka-Mtambaswala km 65.5 katika Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment