Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe na Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania,Mizengo Pinda kwa pamoja wakikata utepe kuasharia kuuzindua mfumo wa kidigitali utakaowezesha ndege kutua salama katika Kiwanja cha Ndege Mpanda, Mkoani Katavi.
Afisa Muongoza Ndege Mwandamizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA Sunday Walinda akimpatia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe maelezo ya kitaalamu kuhusu mfumo wa kidigitali utakaowezesha ndege kutua salama katika Kiwanja cha Ndege Mpanda, Mkoani Katavi.
Rubani wa Shirika la ndege la Tanzania Rubani Hamza akielezea namna mfumo huo ulivyorahisisha hatua za utuaji ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda, Katavi.
Viongozi walioketi meza kuu wakipungia ndege ya Shirika la ndege la Tanzania kama ishara ya kuitakia safari njema ilipokuwa ikipaa kutoka uwanja wa ndege wa Mpanda, Katavi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari akielezea mchakato mzima ukinzia na tafiti na hatimaye kubuniwa kwa mfumo huu wa kidigitali wa kuziwezesha ndege kutua salama katika uwanja wa ndege wa Mpanda, Katavi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe, akielezea kufurahishwa na jitihada zilizofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania kufanikisha mfumo huu kukamilika sambamba na kuipongeza mamlaka hiyo kwa kutumia wataalamu wazawa waliobuni mfumo huu katika Kiwanja cha Ndege Mpanda, Mkoani Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh Juma Zuberi Homera ameipongeza TCAA kwa kubuni mfumo huu na kusisitiza kuwa wananchi wa Mpanda watumie fursa hii ya ujio wa ndege mara tatu kwa wiki kujiimarisha katika kuwekeza kwani milango ya biashara na wageni zaidi kufika mpanda kwa usafiri wa anga sasa imerahisishwa.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda akiwachagiza wanaMpanda kuitumia fursa hii ya ujio wa ndege katika wilaya hiyo kujinufaisha kiuchumi.
Monday, December 30, 2019
Thursday, December 26, 2019
BRELA YAFANYA BONANZA LA MICHEZO KWA ZAIDI YA VIKUNDI 48 JIJINI DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF Anna Makinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika bonanza la Brela akikagua timu ya mpira wa miguu iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF Anna Makinda (katikati) akiwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bi. Loy Watson Mhando ( wa kwanza kushoto) wakifuatilia bonanza la michezo lililoandaliwa na BRELA jijini Dar es Salaam.
Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) wamefanya bonanza la michezo kwa vikundi 48 vya mpira wa miguu likiwa na lengo wa kujenga afya na kuimarisha uhusiano baina ya wafanyabiashara.
Bonanza hilo lilofanyika pia lilikuwa na lengo la kuwaelezea umuhimu wa bima ya afya kwa dereva wa bodaboda na wananchi kwa ujumla.
Akizungumza Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bi. Loy Watson Mhando amesema kuwa wamefurahishwa na jinsi watu walivyojitokeza kushiriki mazoezi na kupima afya zao jambo linalisaidia kupunguza wagonjwa.
Bonanza hilo lilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF Anna Makinda (katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi limefanikiwa kwa asilimi 100 kwa kuweza kufikisha malengo yake.
Sunday, December 22, 2019
WATANZANIA TUSHEREKEE SIKUKUU YA KRISMAS KWA AMANI NA UPENDO MKUBWA - RAIS MAGUFULI
“Niwaombe ndugu zangu wa
Chato na Watanzania kwa ujumla, tusherehekee sikukuu ya Krismasi kwa amani na
upendo mkubwa, lakini pia tuukaribishe Mwaka Mpya kwa amani na upendo mkubwa wa
Kristo, mwaka unaokuja uwe mwaka wa mafanikio, uwe mwaka wa maendeleo, uwe
mwaka wa kujenga umoja wetu kwa Watanzania wote, uwe mwaka wa amani na upendo
na uwe mwaka wa kuendeleza Taifa letu katika maendeleo ya kweli”
amesema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, Mhe. Rais
Magufuli amewapongeza Waumini wa Parokia ya Bikira Maria Chato kwa kazi kubwa
ya upanuzi wa Kanisa wanayoendelea nayo ambayo naye alichangia upanuzi wake
mwaka 2016.
Misa Takatifu hiyo
imeongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Henry Mulinganisa.
Friday, December 20, 2019
TUME YA MADINI YATANGAZA ZABUNI UNUNUZI WA MAENEO YENYE LESENI HODHI ZA MADINI
Tume ya Madini imetangaza zabuni kwa ajili ya ununuzi wa
maeneo 10 yenye leseni hodhi za
madini na yenye ukubwa wa kilomita za mraba
381.89 yaliyopo katika maeneo ya Ngara – Kagera, Kahama- Shinyanga, Chunya-
Mbeya, Bariadi na Busega – Simiyu, Morogoro, Nachingwea – Lindi ambayo awali
leseni hodhi zake zilikuwa zimerudishwa Serikalini.
Uamuzi huo umetangazwa
tarehe 19 Desemba, 2019 na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula
kupitia mkutano wake na waandishi wa habari
uliofanyika jijini Dodoma na
kuhudhuriwa na Kamishna wa Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki, Katibu
Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya pamoja na watendaji wengine
wa Tume ya Madini.
Profesa Kilula alifafanua
kuwa, awali mwaka 2017 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha
marekebisho ya Sheria ya Madini Sura Namba 123 na kanuni zake ambapo pamoja na mambo mengine, zilizokuwa
leseni hodhi za madini ( retention
licence) zilirudishwa Serikalini .
Alisema baada ya marekebisho
hayo maeneo yote 10 yenye ukubwa wa
kilomita za mraba 381.89 yalirudishwa Serikalini na kuongeza kuwa, wachimbaji
wa madini wengi wamekuwa wakiulizia maeneo hayo mara kwa mara lengo likiwa ni
kuomba leseni za uchimbaji madini.
Aliendelea kusema kuwa,
baada ya uchambuzi wa kina kufanyika, Serikali kupitia Tume ya Madini, maeneo yote 10 yaliyokuwa na
leseni hodhi yatatolewa kwa zabuni na kukaribisha kampuni za uchimbaji wa
madini na watu binafsi wenye uwezo wa
fedha na utaalam katika miradi ya uchimbaji wa madini na wenye nia ya kuendeleza miradi ya madini
ya nickel, dhahabu na rare earth elements kuomba zabuni hizo.
Aliongeza kuwa, mwekezaji
atakayeonesha nia ya kuwekeza katika maeneo hayo atakuwa na jukumu la kufanya kazi na kuwaendeleza wachimbaji
wadogo wa madini.
Katibu Mtendaji wa Tume ya
Madini, Profesa Shukrani Manya (kushoto)
akifafanua jambo katika mkutano huo.
|
Wakati huo huo, Katibu
Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akielezea hatua
zinazochukuliwa kwa wamiliki wa leseni
wasioendeleza maeneo yao, aliwataka wamiliki na waombaji wote wa leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini wenye mapungufu kurekebisha mapungufu hayo ndani ya
siku 30 kuanzia sasa.
Alifafanua mapungufu hayo
kuwa ni pamoja na leseni ambazo hazifanyiwi kazi, leseni ambazo hazijalipiwa
ada ya pango la mwaka, maombi ambayo hayajalipiwa ada ya maombi na maombi
yaliyokosa viambatisho muhimu kwa mujibu wa sheria.
Profesa Manya alitaja
mapungufu mengine kuwa ni pamoja na waombaji waliokidhi vigezo vya kupewa leseni
lakini hawajalipa ada ya maandalizi na wamiliki ambao leseni zao zimeshatolewa
lakini hazijachukuliwa.
Alifafanua kuwa mpaka sasa
leseni zaidi ya 134 za utafutaji na uchimbaji wa kati wa madini hazijachukuliwa
na zaidi ya maombi 450 ya leseni za utafutaji yana mapungufu.
Akielezea hatua
zitakazochukuliwa kwa kampuni au watu binafsi walioaminiwa na Serikali na
kupewa leseni lakini wameshindwa kutekeleza masharti ya leseni kwa mujibu wa
Sheria ya Madini, alisema leseni ambazo
hazijalipiwa ada ya pango kwa mwaka, leseni ambazo hazifanyiwi kazi na leseni
ambazo zimekwishatolewa lakini hazijachukuliwa zitaandikiwa hati ya makosa na
yasiporekebishwa zitafutwa kwa mujibu wa sheria.
Aidha alisema kuwa, maombi
yote ya leseni za utafutaji na uchimbaji wa kati yenye mapungufu yataondolewa
kwenye mfumo wa utoaji wa leseni ili waombaji wengine wenye sifa pamoja na
wachimbaji wadogo waweze kuomba maeneo hayo.
Aliendelea kusema kuwa,
maombi ambayo yamekidhi vigezo vya kupewa leseni lakini hayajalipiwa ada ya kuandalia
leseni yataondolewa kwenye mfumo ili waombaji wengine wenye sifa waweze kuomba
maeneo hayo.
Alisisitiza kuwa tangazo la
zabuni husika linapatikana katika tovuti ya Wizara ya Madini ambayo ni (www.madini.go.tz) Tume ya Madini (www.tumemadini.go.tz) magazeti ya Habari
Leo na Daily News ya tarehe 20 Desemba, 2019 pamoja na blogs na mitandao ya
kijamii.
KONGAMANO LA TATU LA SIKU MBILI LA KIMATAIFA LA KISWAHILI LAFUNGULIWA ZANZIBAR
Balozi Seif akiangalia baadhi ya Vitabu vya Kiswahili na kuridhika na kazi kubwa ilivyofanywa na Magwiji wa Lugha ya Kiswahili kutoka pembe mbali mbali za Dunia. |
Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais wa ZanzibarMabaraza, Taasisi pamoja na
Wataalamu wanaoshughulikia Kiswahili wana wajibu wa kusimama kidete
kuhakikisha kuwa Lugha ya Kiswahili inaendelezwa na kutumiwa katika
usahihi wake kulingana na Utamaduni wa Waswahili kwa vile Lugha ni
kipengele muhimu cha Utamaduni wa Jamii.
Washirika
hao lazima waone fahari ya mafanikio ya Lugha ya Kiswahili kwamba sasa
imekuwa sio Lugha ya Waswahili wazawa wachache peke yao bali imeshaenea
kuwa Lugha ya Kimataifa yenye utambulisho wa kujivunia kama nembo ya
Afrika.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein
alitanabahisha hayo wakati akilifungua Kongamano la Tatu la Siku Mbili
la Kimataifa la Kiswahili katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika
Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni.
Alisema
hiyo ni hatua muhimu ya kupanda hadhi kwa Lugha ya Kiswahili jambo
ambalo halitotokea kwa sadfa, bali litatokana na dhamira ya dhati ya
Watu wenye mapenzi na Lugha hii adhimu na wanaoishughulikia.
Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ali Aman Karume akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kulifungua Kongamano hilo la Siku mbili la Kiswahili. |
Subscribe to:
Posts (Atom)