Serikali kupitia Waziri
wa Madini Doto Biteko amesema, serikali ipo katika hatua za mwisho za
majadiliano kuhusu miradi ya mchuchuma na Liganga ili iweze kuanza. Ameongeza
kuwa mradi wa mchuchuma na Liganga ni miradi ya miaka mingi lakini haina tija
na ndio maana serikali ya awamu ya tano iliamua kufuatilia kuhusu mikataba ya
miradi hiyo ili kuona kama ina tija kwa taifa wakiwemo watu wa Ludewa.
Akizungumza jana tarehe
15 Machi, 2020 wakati wa mkutano na wananchi wa kijiji cha Mundindi wilayani
Ludewa,Waziri wa Madini Doto Biteko amesema, pamoja na kuchelewa kuanza kwa miradi
ya Mchuchuma na Liganga, kuna manufa makubwa kwa wananchi na taifa kuliko miradi
hiyo ingeanza kabla kufanyika kwa majadiliano yanayoendelea.
Waziri wa Madini Doto Biteko wa pili kushoto akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christophher Ole Sendeka wakati wa ziara yake mkoa humo wakiwa wilayani Ludewa. |
“Ndugu zangu niseme
stori za Mchuchuma na Liganga imetosha. Nafahamu mnamahitaji makubwa kuona hii
miradi ianze, hata mimi nikiwa mdogo nimeshasikia sana kuhusu miradi ya
Mchuchuma na Liganga, serikali tunayo sabau ya kuangalia maslai yenu na taifa.
naomba niwaambie, serikali yenu ipo kwa ajili yenu, naomba kuweni na subira” alisema Biteko.
Biteko ameongeza kuwa
serikali iligundua mambo mengi yasiyo na tija kuhusu mikataba ya miradi hii
ndio maana tuliamua kufanya majadiliano ilikuona namna gani serikali
itakavyonufaika. Mmekuwa wapole, watulivu na wasikivu ni jambo zuri sana, niwaombe
endeleni kuwa wavumilivu viongozi wenu
wa mkoa na wilaya, mbunge na diwani wenu wamekuwa na kilio kama chenu ndio
maana niliamua nije niweze kuzungumza na ninyi.
Biteko amesema, hakuna
mwananchi yeyote atakae punjwa kuhusu fidia yake, serikali italisimamia suala
hilo kwa uzito mkubwa.
Sehemu ya Wananchi kijiji cha Mundindi wilayani Ludewa wakimsikiliza Waziri wa Madini Doto Biteko hayupo pichani wakati wa kikao cha hadhara. |
“Nawaomba. kuweni na
imani na serikali yenu, nitasimamia kama nilivyosimamia fidia za wananchi wa Nyamongo wilayani Tarime dhidi ya Mgodi wa
North Mara waliokuwa wanahitaji maeneo ya wananchi.
Ndugu zangu ninachotaka
kila jamii inufaike na mali zilizopewa na mungu. Ludewa najua mnataka kunufaika
na miradi ya Mchuchuma na Liganga kama ambavyo Geita wananufaika na Dhahabu,
Shinyanga wananufaika na Almasi, Songea
wananufaika na Makaa ya Mawe, Arusha wananufaika na Tanzanite na Tanga
wananufaika kuhusu vipepeo vya kila aina.” aliongeza Biteko.
Waziri wa Madini Doto Biteko kushoto na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christophher Ole Sendeka wakiwasikiliza wananchi hawapo pichani wakati wa kikao katika kijiji cha Mundindi wilayani Ludewa |
Na
Issa Mtuwa – Ludewa
Kwa upande wake, Mkuu
wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amemshukuru Waziri kwa kutimiza ahadi
yake ya kuja Njombe kwa ajili ya ziara hii na kutembelea maeneo mbalimbali ya
maeneo ya sekta ya madini na kuzungumza na wananchi hasa wa Ludewa ambao wanakilio
kikubwa kutokana na kuchelewa kwa miradi ya Mchuchuma na Liganga.
Diwani wa Kata ya Mundindi,
Wise Mgina, amemweleza Waziri kuwa watu wa Ludewa wanapenda kuona miradi hiyo ikianza
kwa kuwa ni miradi ya muda mrefu na wananchi wake wanashindwa kuendeleza ardhi
hiyo kutokana zuio hivyo wanaiomba serikali miradi hiyo ianze ili iwanufaishe
wananchi wake.
No comments:
Post a Comment